Tuesday, 24 February 2026

FAHARI YA MACHO INAVYOFILISI DUKA

 FAHARI YA MACHO INAPOFILISI DUKA: Mbweni, Maadili na Soko Huria la Unafiki


Kuna msemo wa Kiswahili usemao: “Samaki mkunje angali mbichi.” Lakini sisi tumengoja mpaka samaki awe stockfish wa Norway, kisha tunashangaa kwa nini havunjiki bila nyundo.


Nimeitazama simulizi ya wakaazi wa Mbweni, Zanzibar, wakisimama kidete kupinga baa na kumbi za starehe katika maeneo yao ya makazi. Wakisema wanalinda maadili. Wakisema wanazuia uhalifu. Wakisema wanataka mazingira salama kwa watoto wao. Maneno mazuri. Maneno ya kuvutia. Maneno yanayopata likes na views kwa kasi kuliko sera za ajira.

Lakini kama alivyotuonya Karl Marx, mara nyingi jamii hupenda kushughulika na superstructure—dalili—wakati base ya kiuchumi ndiyo inayozalisha tatizo. Baa siyo mzizi; ni tawi. Kumbi za starehe si chanzo; ni kivuli cha mti uliopandwa zamani kwa mbolea ya utalii, soko huria na uchumi wa huduma.


Tuliposema “karibuni wageni”, tulimaanisha wageni wa aina gani? Tulipofungua milango kwa jina la uwekezaji, tulifikiri mitaji huja na tasbihi? Au tulidhani fedha huingia bila falsafa yake?


Max Weber aliwahi kueleza kuhusu “roho ya ubepari” – ile ari ya kimaslahi inayovaa suti ya maadili lakini moyoni ina hesabu za faida. Leo tunashuhudia roho hiyo ikitembea Mbweni kwa jina la “burudani”, “ajira kwa vijana”, “ukuaji wa uchumi”. Na sasa, wale wale waliopiga makofi wakati majengo yanapanda, wanashika mawe majengo yanapotoa kelele.


Ni vigumu kula keki na kuendelea kuimiliki.

Jamii yetu ilijenga uchumi wa utalii kwa mikono yake miwili. Ikaupa kipaumbele. Ikaufanya uti wa mgongo. Leo tunasema uti huo una maumivu ya maadili. Lakini uti hauwezi kuugua bila mwili mzima kushiriki. Kama alivyosema Émile Durkheim, jamii inapopoteza mwelekeo wa pamoja huingia katika hali ya anomie—mkanganyiko wa maadili. Hapa ndipo tulipo: tunataka soko huria, lakini kwa masharti ya madrasa; tunataka dola ya kisasa, lakini kwa maadili ya kijiji kisichobadilika.


Na tusijidanganye—tatizo si pombe pekee. Tatizo ni mabadiliko yasiyosimamiwa. Ni mipango miji iliyoachwa mikononi mwa tamaa. Ni pengo la ajira linalowasukuma vijana kwenye “uchumi wa usiku”. Ni magari yanayotumika kama vyumba vya siri kwa sababu nyumba hazina faragha na mazungumzo ya ngono ni mwiko mchana lakini biashara usiku.

Tunahukumu matokeo, tunalea sababu.


Wakaazi wa Mbweni wana haki ya kuhoji. Lakini pia lazima tujiulize: Je, tulichelewa? Je, tulipoona mchicha unaota pembeni ya nyumba tulidhani ni mboga ya leo, tusijue kesho utakuwa mbuyu? Tulipoona vibali vinatolewa, tulinyamaza kwa sababu “mwenye nacho” alikuwa amenyoosha mkono?

Hapa ndipo kejeli inapoanza kujicheka yenyewe.


Kwa miaka mingi, Unguja na Pemba vilijulikana kwa utulivu, kwa ustaarabu, kwa elimu na kwa ukarimu. Lakini pia vilijulikana kwa ukimya wa kukubali. Ulikuwa ukimya wa busara au wa woga? Ulikuwa uvumilivu au uzembe wa kimfumo?

Antonio Gramsci alizungumza juu ya hegemony—namna tabaka tawala linavyofanya fikra zake zionekane kama fikra za wote. Leo ukisema “hii ni haki ya kikatiba ya kufanya biashara”, mjadala unafungwa. Ukisema “haya ni maadili ya jamii”, mjadala mwingine unafungwa. Haki dhidi ya maadili. Uchumi dhidi ya utamaduni. Njia panda.

Na njia panda haichagui mwenye haraka.

Wengine wanasema haya ni mabadiliko ya wakati. Sawa. Lakini si kila kinachoitwa maendeleo ni ustaarabu. Na si kila kinachoitwa maadili ni suluhisho. Kijana akija nyumbani uchi kutafuta hifadhi, je, ni “kwenda na wakati” au ni dalili ya mfumo uliomwacha njiani? Swali si la kejeli tu; ni la sera.

Tatizo la Mbweni si Mbweni peke yake. Ni kioo. Leo ni kule, kesho ni Kinuni, keshokutwa ni Nyarugusu. Leo tunapinga baa; kesho tutapinga ajira zinazotokana na baa. Leo tunasema ondokeni; kesho tutasema vijana hawana kazi.

Hii ndiyo paradox ya jamii inayotaka matokeo ya ubepari bila athari zake.

Kuachia yaendelee si busara. Kuyaondoa kwa ghafla ni hatari. Suluhisho si kufunga milango yote, wala si kuacha wazi bila bawaba. Suluhisho ni sera makini, upangaji miji, udhibiti, na zaidi ya yote—uamuzi wa pamoja unaochelewa lakini si “too little too late”.

La sivyo, fahari ya macho itaendelea kufilisi duka la maadili. Tutabaki na mabango ya “mazingira salama” huku usiku ukiendelea kuuza tiketi.

Mimi si mhubiri, wala si mpiga debe wa starehe. Ninasema tu: tusipende kupambana na kivuli cha mti tulioupanda wenyewe. Kama mzizi ni mkubwa kama mbuyu, basi hatuwezi kuuangusha kwa fimbo ya mkutano mmoja wa wananchi.

Tunahitaji shoka la sera, si miayo ya hasira.

Na kama mkono wa kuume una nguvu, basi utumike kwa hekima, si kwa jazba. La sivyo tutajikuta tunasulubiwa na maamuzi yetu wenyewe, tukilia juu ya paa tulilojenga kwa mikopo ya sifa na kulipa kwa riba ya maadili.

Mungu atufanyie wepesi—lakini kabla ya wepesi wa mbinguni, tujifanyie ujasiri wa duniani.


Lakini kabla hatujamaliza kwa dua, labda tuanze na maswali—kwa sababu jamii inayokimbia maswali huishia kuabudu majibu mepesi.

Je, maadili ni kitu kinacholindwa kwa kufunga mlango wa baa, au ni kitu kinachojengwa kwa kufungua mlango wa fursa?

Je, tunapopiga vita pombe, tunapiga vita kemikali au tunapiga vita upweke, ukosefu wa ajira na kukata tamaa?

Je, soko huria linaweza kuvaa kanzu ya utamaduni bila kuacha harufu ya faida?

Je, haki ya kikatiba ya kufanya biashara ina mipaka pale inapoanza kugusa usingizi wa mtoto wa jirani, au haki huwa haina majirani?

Je, jamii inaweza kudai usafi wa maadili huku ikiishi kwa kodi na ajira zinazotokana na kile kile inachokilaani?

Je, tulipofungua milango ya utalii tulijua kwamba wageni huja na mizigo yao ya fikra, au tulidhani mizigo yao huishia uwanja wa ndege?

Je, tunachokipinga leo ni baa, au ni kioo kinachotuonyesha sura yetu tuliyoisahau?

Je, maendeleo ni nini—idadi ya majengo au ubora wa roho?

Na kama maendeleo yanapimwa kwa fedha, je, maadili yanapimwa kwa nini?

Je, tunaposema “zamani haikuwa hivi” tunamaanisha zamani kulikuwa na usafi, au zamani kulikuwa na siri?

Je, kizazi cha leo kimeharibika, au kimeacha kuogopa kusema kile kilichokuwa kikifanyika gizani?

Je, tatizo ni kelele za muziki, au ukimya wa sera?

Je, tukifunga baa zote, tutajenga viwanda?

Na tusipojenga viwanda, tutafunga nini tena ili kujisitiri?

Je, jamii inaweza kubaki kisiwa cha maadili katikati ya bahari ya utandawazi, bila kuogelea wala kuzama?

Na mwisho kabisa—

Je, tunataka kweli suluhisho, au tunataka tu adui wa kumlaumu?

Kwa sababu huenda tatizo si Mbweni.

Huenda tatizo ni sisi.

Na huenda suluhisho si kufukuza kivuli, bali kukubali kwamba mwanga tunaoutafuta lazima uanze ndani yetu.

Wasalam Ramadhan Maqbool.

Thursday, 7 August 2025

NANI AMEUWA MAGEUZI na MARIDHIANO YA SAMIA NA WAPINZANI NCHINI TANZANIA

 Leo nitawakumbusha siku nilipokutana  na RAIS SAMIA  mwaka 2023 na mazungumzo yetu juu ya nia yake ya kuleta MAGEUZI Tanzania  niliondoka pale nikiamini Tanzania mpya inaletwa na mama Mzanzibari na hata agenda kuu ya Uraia pacha ya watu wa diaspora ipo salama kwa wakati muafaka ukifika baada ya uchaguzi wa 2025 kumalizika. Masuali yangu ya kwa Nini ulimueka FREEMAN MBOWE ndani

na kutokubaliana nae na njia yake ya utawala wake wa kuwaeka wapinzani wake Ndani nilimuambia hapa ulikosa busara za hali ya juu na yeye alinieleza tafrani zake alizokumbana nazo Ndani ya CCM ya upinzani wa  watu wanaompinga na wengi  waliokuwa wafuasi wa bosi wake RAIS Magufuli na baadae kina Mbowe kumuongezea tafrani   za kudai katiba mpya alihitaji kufocus  kupanga serikali yake ya watu walio watiifu kwake

Rais Samia alitamani sana kuona Tanzania yenye muelekeo wa serikali ya mseto baada ya uchaguzi wa 2025 kuona hatuoneshani vidole bali wanaionyooshea vidole Taifa la Tanzania na sisi kama Watanzania tunawanyooshea mabeberu vidole kama Watanzania bila kujali tofauti ya vyana vyetu.

Kwa Nini ndoto ya Rais Samia imetekwa NYARA?

Wakati Rais Amani Karume anafanya mazungumzo ya Siri na RAIS wa MOYO WA WAZANZIBARI Maalim SEIF Sheriff HAMAD alipambana na vikwazo vikubwa ndani ya chama chake cha CCM na kuitwa msaliti hadi mitandaoni na mabalozi wetu nje wenye asili ya Zanzibar nikuwa RAIS KARUME anataka kuiuza CCM Zanizbar kwa  chama cha CUF Na huko  CUF kwa hasira nyingi za makovu ya CCM ya huko nyuma ya Komandooo ya muafaka wa ulioanzishwa na katibu wa jumuia ya madola  EMEKA  ANYAOKU . Licha  ya DR SALMIN AMOUR  alieusaliti muafaka no 1.Maalim SEIF na RAIS KARUME walianzisha muafaka no 2 kutengeneza maslahi ya Utulivu wa Zanzibar sio maslahi ya CCM na CUF , lakini Maalim SEIF na yeye alikumbana na mabomu ya wahafidhina wa CUF kuwa  anajipendekeza kwa RAIS KARUME hakuwa salama kwa kushambuliwa kuwa anapigania mafao yake kustaafu ya uwaziri kiongozi yaliokatwa na kunyimwa mafao yake toka alipofukuzwa CCM .Maalim na timu yake ya watu watano walipambana kuhakikisha hakuna kidudu mtu anafanikiwa mara hii kuyakoroga mazungumzo yale .

Baadae wote wawili Maalim SEIF na 'Rais Karume walijua wapo vitani kuwa ndani ya vyama vyao kuna camp za wahafidhina zinazopinga mazungumzo yale kutokana na kambi ya CCM kuhofia kundi fulani maslahi yao kuguswa ikiwa CUF wataingia serkalini na ndani ya CUF makovu ya watu kupigwa risasi kuuliwa mwaka 2001 hadi  Tanzania kuzalisha wakimbizi Mombasa Kenya kitendo ambacho Rais Mkapa aliandika kwenye kitabu chake ndio doa la utawala wake Tanzania kuzalisha wakimbizi nje ya NCHI 

 wakati Tanzania ilikuwa ni  NCHI ya kupokea wakimbizi  wa nje . Maalim na Rais Karume waliafanikiwa mazungumzo yao kwa Kila upande kulegeza kamba na kufikia mauafaka uliiopelekea kuanzishwa Sheria ya kura ya maoni iliowakilishwa kwenye baraza la wawakilishi la Zanzibar

Wazo letu la wengi   la wanadiaspora wengine waliotumia mlango wa nyuma wa diplomasia la kutaka KINA LISSU na LEMA na Kampeni aya Mheshimiwa Mbowe kuachwa na wlaiopo nje warudi nyumbani kuondoa doa la kuwa Tanzania ina wakimbizi wa kisiasa nje ya NCHI alilichukua kwa mikono miwili hata haikufika miezi miwili mama wa KIZANZIBARI nilimuona yupo ubelgiji anakutana na TUNDU LISSU hapo niliamini kabisa kwenye moyo wangu kua SAMIA sasa hatanii bali anataka kuleta mshikamano wa taifa letu kwa nadharia ya Maalim SEIF na kuyaponya yale makovu ya walioumizwa na makovu ya CCM ya tawala zilizopita na makovu ya chaguzi zilizoacha misiba na simanzi nyingi hasa kwa ndugu zake kule Zanzibar roho za watu 29 zilipotea na mamia ya Wazanzibari wenzake kuachwa na ulemavu.

Nafikiri  Wapinzani  wa CHADEMA waliasahau kuwa  wahafidhina wanaompinga mageuzi ndani ya CCM bado wapo .Mfano wa  Kitendo kile kiliniacha na huzuni kubwa  baada ya Kumsikia Makamo wa pili wa RAIS wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed alipendekezwa na Magufuli kuwa Makamo wa RAIS kukanusha kuwa hakuna watu waliouliwa  Zanzibar au kupigwa risasi  yeye hana taarifa hizo na Kila waliojaribu kumkaribia Rais Mwinyi kuwasaidia mayatima waliouliwa ndugu zao  alijieka mbali kwenye kuwakaribia au kuwatembelea kuwafariji kwa misiba waliopata familia hizi 29 waliouliwa ndugu zao na hata majeruhi kama viongozi wa CUF na Waziri wa Afya wa ACT sasa alietekwa na kupigwa na kuumizwa pamoja na mjumbe wa tume ya uchaguzi wa CUF ndugu Ayoub  Bakari ambae sasa hiviamerudfi tena kwenye tume ya uchaguzi wa Zanzibar.















Saturday, 28 June 2025

Kenya Protest one year aniversary

Kenyan governemnet supress peacefull protest.

Thursday, 22 May 2025

East Afrika Kumekucha wiki hii sakata la Mama Samia vs Martha Karua na Boniface Mwangi

Kenya ya thibitisha Tanzania imemuachia Boniface Mwangi kosa kubwa Tanzania haijui nguvu ya ya Mwangi inayoweza kusambaa jeshi a lake la wanaharakati sasa Tanzania .

Alhamisi wiki hii, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Musalia Mudavadi, alithibitisha kuwa Mwangi aliachiwa. Hata hivyo, hakutoa maelezo zaidi kuhusu mazingira ya kuachiliwa kwake, akisema tu kuwa "tumejihusisha kidiplomasia, na ndivyo inavyofanyika."

Gazeti la Daily Nation linaripoti kuwa Mwangi alirudishwa Kenya kwa barabara na kutelekezwa katika mji wa Ukunda, karibu na mpaka wa Tanzania. Alikimbizwa hospitalini kwa uchunguzi, ambapo mkewe, Njeri Mwangi, alisema mumewe amejeruhiwa na miguu yake imevimba.



Secret reason Suluhu deported Karua and why Bongo hates Kenya. Welcome to the latest Kenya news, Kenya politics and more analyzed by veteran Kumekucha Chris for the real inside story; The Martha Karau deportation from Tanzania saga has sent shock waves across the continent. But the truth is that Most Kenyans have never had any idea about this in Tanzania.


  Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Musalia Mudavadi amelithibitishia shirika la habari la AFP leo Alhamisi kwamba mwanaharakati maarufu, Bonifas Mwangi,ameachiliwa huru na maafisa wa Tanzania.