Thursday, 7 February 2013

Mzanzibari awe na VItambulisho Vingapi jee Mtanganyika ?

Leo Najua Kwa wale wafanyabishara wakuwba watafurahia tendo la Tanzania kuwa na ID kwani umuhimu wa Tassisi za kibishara kwa kitambulisho cha taifa na kulinda haki a raia wa Taifa hilo ni kitu kilichokuwa over due 50 yrs ago.Kuanzia Mabenki yalikuwa yakikumbana na tsunami ya fraud na taasisi nyengine nafikri sasa hivi Wafanyabishara wa Taasisi za kifedha watanufaika zaid na Mradi huu. Ila pia mradi huu wa Kitabulisho wa Kitanzania una utata Kwani Nakumbuka miaka mitano iliopita Rais wa Wakati huo Alhaj Karume aliipa Kampun iya Israeil contract ya mlango wa nyuma kutoa Vitambulisho vya utaifa vya Wazanzibari Kwa hili nitampa Shukran Zangu Rais Karume kuilinda haki ya Wazanzibari na hapa naweza kusema aliona Mbali kulinda haki za Wazanzibari japo na yeye alipata 10% yake la kujiuliza tu jee Kitambulisho Cha Mzanzibari kimetimiza mahitaji ya Mzanzibari? kulinda haki zake kama ajira na haki nyengine , leo itafika wakati unanunua ardhi utaambiwa tusibitithishie uraia wako ndio tukupe nyaraka ya ardhi au unapotaka kufungua account bank au kusajili Kampuni au kutaka ajira sio uoneshe degree yako tu bali pia unayo ile haki ya Kufanya kazi nchini. Pia usalama wa Nchi utaimarika kwani sio siri Tanganyika lilikua Shamba la bibi atakae aje kuanzia Mkongo , Mrwanda , Mburundi , Mnigeria , Kila mtu alikua akijipatia kipande chake cha keki na hii serkali ya CCM ilishindwa miaka Hamsini ndio finaly imeweza kupunguza ile issue ya kila mtu Kuwa raia wa Tanzania ila sijui kama hautakua mradi wa watu kila mtu anaengia pale kuuziwa Kichambilisho hichi chembelecho wat u wa Mombasa ! Suala la Pili Nitawauliza Wanasheria wetu wa Tanganyika na Zanzibar Nchi Mbili ila tuna Vitambulisho vya aina Mbili vya Mzanzibari na Mtanzania na Jee kile cha Mtanganyika kiko wapi ? . Kuna wengine watasema Juzi nilimsikia Mwenyekit wia Chadema akisema Wazanzibari wana kila kitu chao Nchi yao ina serikali yao , Bendera yao, Bunge lao , Rais wao na ID yao Jee Mtangayika Chake ni Kipi , kuna Watanganyika watakaosema hawa wanataka chao chao ila cha kwetu chetu shirika imekuaje mambo haya au mfumo mbaya wa Muungano , kwa nini tusiziweke haki za Mtanganyika na Mzanzibari wazi na zile za Utanzania wazi. Hatuoni kuna kizungumkuti hapa au ndio alivyosema Mbowe Watanganyika sisi tumepigwa bao Wazanzibari wanatucheka ? Kwani Nahofia huko usoni itafika siku pale Bongo Mzanzibari ataenda bank kufungua account na kuambiwa lete Kitambulisho chako cha UTAIFA na akitoa cha kitambulisho chake cha Utaifa wa Zanzibar au aende Mombasa kusajili Kampuni ya bishara aambiwe lete Kitambulisho cha Utaifa na atoe cha Zanzibar huku wengine wataona hapa nini nakusudia kuwaamsha watu huko mbele tunakoelekea kwani itakuja kufika siku kuenda Mahakamani mtu kudai haki yake kwa mkanganyiko huu wa VItambulisho vingi which is Which tuelezeni kipi cha Utaifa na kipi kisicho cha utaifa na Kitambulisho Cha Mtanganyika kiko wapi ?
KWA KUMBU KUMBU ZANGU Nakumbuka mwaka 1995 Nilikua pale Jangwani Kumsikiliza Mchungaji Mtikila sikuogopa kuitwa gapacholi kwa vile rangi yangu haikuwa nyeusi ila wakati huo nilikua nakaa Oysterbay na niliwajua baadhi ya vigogo kilichonishangaza ni kuwa walikuja vigogo kwa siri mkutano ule wa Mtikila alipotangaza Kesho Jangwani,tutairudisha serkali ya Tanganyika pia nakumbuka sio kwenye Upinzani tu Utanganyika pia uliwahi kuitikisa serikali ya Mwinyi kina Njelu kasaka wa CCM kabla ya kukimbilia CUF kuatka ubunge aliwika kwa kuirudisha Tanganyika yao na sasa hivi Mbowe amewaahidi Watanganyika serikali yao ni sio Wafuasi wa Utanganyika niliowaona pale Jangwani 1995 na kuambiwa magabacholi wanaitafuna nchi yenu hawakua kidogo ni wana CCM kindaki ndaki leo hii bado na nina hakika Chadema ina wafuasi wasio kidogo na Hoja ya Utanganyika hiijasimama na naamini ina umaarufu mkubwa Pale Wanasiasa watakapoaivalia njuga 2015 kuna Wengine wanakuambia Tangayika yetu itarudi 2015. Jee Kweli Kitambulisho Mtanganyika kitakua mafichoni milele !au kundi hili lili mafichoni tokea 1995 litarudi kwa nguu au mwamvuli wa katiba mpya nafikiri hapa CCM ndipo watakapogonga mwamba ! Nilitaka sana kujua Dhana ya Mtikila kwa nini alikuja na sera ya utangnyika mara ya mwisho nilongea nae wakati akiwatembelea Wakimbizi wa Kizanzibari kule Shimoni Mombasa Kenya nilitaka tukutane nione ni kitu gani kilichomfanya aibue hoja ya injustcie za 1964. Na kwa nini alitaka kututia baharini Wazanziabri tuliwe na samaki tumekosea nini ! Kilichonishangaza ni kuwa Leo viongozi wa Vyama wengine nimewaona wakikabidhiwa Vitambulisho hivi nilichopata wasi wasi wangu tu Mtkila atachukua Kitambulisho cha Utanzani wkati yeye ni muumini wa Utanganyika na Mbowe pia sikumuona kwneye picha za kukabidhiwa kitambulisho cha Utaifa huu kulikoni ?

No comments: