Rais Jakaya Kikwete
--
Bunge hilo litakaloanza mwanzoni mwa mwezi ujao mjini Dodoma, litakuwa na kazi ya kuijadili na kuipitisha Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Desemba 30 mwaka jana.
Wajumbe wengine watakaounda Bunge hilo ni 42 kutoka vyama vya siasa, 358 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na 81 kutoka Baraza la Wawakilishi.
Wajumbe wengine watakaounda Bunge hilo ni 42 kutoka vyama vya siasa, 358 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na 81 kutoka Baraza la Wawakilishi.
Januari 2 mwaka huu, ilikuwa siku ya mwisho kwa Ikulu kupokea majina ya makundi mbalimbali ya kijamii ambayo yaliwasilisha mapendekezo ya majina ya watu ambao wangependa wawe wajumbe wa Bunge hilo. Makundi zaidi ya 50 yaliwasilisha majina yao.
--
MCHANGANUO WA MAPENDEKEZO YALIYOWASILISHWA YA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA
IDADI INAYOTAKIWA KISHERIA
IDADI YA MAPENDEKEZO YALIYOWASILISHWA
IDADI YA MAJINA YALIYOWASILISHWA
NA.
|
AINA YA KIKUNDI/TAASISI
|
IDADI INAYOTAKIWA KISHERIA
|
IDADI YA MAPENDEKEZO YALIYOWASILISHWA
|
IDADI YA MAJINA YALIYOWASILISHWA
|
1. | Taasisi Zisizokuwa za Kiserikali | 20 | 245 | 1185 |
2. | Taasisi za Kidini | 20 | 77 | 277 |
3. | Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu | 42 | 21 | 126 |
4. | Taasisi za Elimu | 20 | 9 | 82 |
5. | Makundi ya Watu wenye Ulemavu | 20 | 24 | 70 |
6. | Vyama vya Wafanyakazi | 19 | 20 | 69 |
7. | Vyama Vinavyowakilisha Wafugaji | 10 | 8 | 43 |
8. | Vyama Vinavyowakilisha Wavuvi | 10 | 7 | 45 |
9. | Vyama vya Wakulima | 20 | 22 | 115 |
10. | Makundi Yenye Malengo Yanayofanana | 20 | 142 | 710 |
JUMLA | 201 | 575 | 2722 |
Kuanza kwa Bunge hilo kunatarajiwa kuwa na mvutano mkali kutokana na msimamo wa baadhi ya makundi hayo, hasa vyama vya siasa ambavyo vimekuwa vikipingana zaidi katika mfumo wa Serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, ilisema kuwa pia majina ya wajumbe wa Bunge la Katiba nayo yatatangazwa katika Gazeti la Serikali kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013. Sheria hiyo inampa madaraka Rais wa Jamhuri ya Muungano kushauriana na Rais wa Zanzibar, kuteua wajumbe 201 wa Bunge la Katiba.

No comments:
Post a Comment