Thursday 30 January 2014

CCM WAENDELEA KUWASHA MOTO KIEMBE SAMAKI


  Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini Mwangi Rajabu Kundya akimnadi mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mahmoud Thabit Kombo katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki zilizofanyika Mbweni Wilaya ya Magharibi Unguja. (Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).
Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki  kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM) Mahmoud Thabit Kombo akiwahutubia wananchi waliofika katika kampeni zake Mbweni Wilaya ya Magharibi Unguja.(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar). Na Miza Kona – Maelezo  Chama cha Mapinduzi ni chama chenye kuleta maendeleo ambacho kinapinga ubaguzi  na kuwatetea wananchi haki zao za msingi  Hayo yameelezwa jana huko Mbweni na Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini Mwangi Rajab Kundya katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki.


Amesema kuwa kuna baadhi ya vyama vya upinzani vinachochea kuleta ubaguzi nchini kwa kisingizio cha kutaka Zanzibar iwe na mamlaka yake kamili kinyume na matakwa yao.Aidha amesema kuwa Zanzibar imeshapata mamlaka yake tangu baada ya Mapinduzi na kuundwa kwa chama cha Afro Shirazi Party ASP ambapo tayari ina viongozi kamili na sifa zake zote za kupata maamlaka hayo. “Mamlaka kamili tayari yamepatikana tangu ilipoundwa ASP hivyo wanataka mamlaka gani tena”, aliuliza Kundya.
Katibu huyo ameeleza kuwa Zanzibar itaendelea kudumisha Muungano ambao unatetea wazanzibar na kuwaletea maendeleo ambayo wananchi wananufaika na matunda yake.Amefahamisha kuwa CCM sio chama chenye kuleta ubaguzi kwa wananchi  kwani kiko makini katika kuwaletea maendeleo ya nchi. Amesema CCM ina viongozi makini ambao ni wataalam wa uongozi hawayumbishwi na watu wasiopenda maendeleo ya nchi.  

“Kiongozi wa watu lazima ajitie katika  makundi ya watu ili aweze kujua shida zao kwa lengo la kutatua matatizo ya watu wao lakini wapinzani hawana utaala huo”, alifahamisha bwana Kundya. Aidha Katibu huyo amewataka wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki kumchagua kiongozi wa CCM kwani ndiye atakaeweza kusimamia Muungano, kupigania haki ya wanzibari  na maendeleo kwa jumla.
Nae mgombea uwakilishi wa chama hicho Mahmoud Thabit Kombo ameahidi kuimarisha matawi ya CCM kwa kinamama na jumuiya za wazazi pamoja na kuwaimarisha na kuwashajihisha vijana katika mambo ya ajira.   

No comments: