Wednesday, 15 April 2015

CCM INAPANGA KUVURUGA UCHAGUZI MKUU

Hofu ya kuahirishwa kwa Uchaguzi Mkuu imezidi kutanda baada ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na wanaharakati kueleza kuwa kuna dalili ndogo za uchaguzi huo kufanyika Oktoba.Lakini mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva amesema viongozi wa kisiasa wasiwajaze wananchi hofu isiyo na sababu kwa kuwa ofisi yake imeongezewa uwezo wa kuandikisha wapigakura na hivyo wana uhakika kazi hiyo itakamilika kabla ya Oktoba.“Vifaa vimeanza kuwasili. Tumeshapata mashine za (Biometric Voters Registration) BVR 248, nyingine 1,600 zinatarajiwa kuwasili wakati wowote kuanzia sasa na Serikali imeshalipia mashine zote,” alisema Jaji Lubuva.
“Kwa hiyo kadri muda unavyokwenda, ndivyo uwezo wetu wa kusajili unavyokuwa mkubwa zaidi na inawezekana tukamaliza kabla ya Julai.” Kuhusu kusimamia kauli yake kuwa Kura ya Maoni ingefanyika kama ilivyopangwa lakini ikahirishwa baadaye, Jaji Lubuva alisema wasingeweza kuahirisha mapema kabla ya kuona ugumu wa kazi yenyewe.Lakini viongozi wa vyama vya upinzani wanaona ahadi hizo ni kama ilivyokuwa kabla ya kuahirishwa kwa Kura ya Maoni na kwamba kasi ndogo ya uandikishaji wapigakura inaweza kusababisha Uchaguzi Mkuu kuahirishwa.Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, mwenyekiti Chadema Freeman Mbowe, mwenyekiti wa NLD Emmanuel Makaidi na mkurugenzi wa asasi ya kiraia ya Concern For Development Initiative in Africa (Fordia), Bubelwa Kaiza, wana hofu ya Uchaguzi Mkuu kuweza kufanyika Oktoba.
Alichosema Lipumba : Akifungua mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF, Profesa Lipumba alisema vifaa vilivyowasili ni vichache kulinganisha na mahitaji ya Tume.
Kuna giza nene
“Hadi sasa daftari la wapigakura halijakamilika hata katika mkoa mmoja na bado vifaa vingi havijawasili nchini,” alisema Lipumba ambaye alidokeza kuwa suala hilo litakuwa ajenda kwenye kikao hicho cha siku mbili.Profesa Lipumba alisema walipokwenda Kenya kwa ajili ya ziara ya mafunzo, walielezwa na Tume ya Uchaguzi ya Kenya kwamba kazi ya uandikishaji wapigakura inatakiwa kuchukua angalau mwaka mmoja.ofesa Lipumba alisema kwa namna ambavyo Jaji Lubuva hayuko huru, Ukawa ina wasiwasi kama mgombea wao wa urais anaweza kutangazwa mshindi iwapo atashinda.Lipumba alisema NEC waliiomba Serikali BVR 15,000 ili kuandikisha wapigakura kwa urahisi, lakini Serikali ikapunguza na kuidhinisha vifaa 8,000.Jumla ya wapigakura milioni 24 wanatarajiwa kujitokeza kujiandikisha kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Mbowe ndiye aliyekuwa wa kwanza kueleza hofu hiyo.
Akizungumza na Mwananchi mwishoni mwa wiki, mwenyekiti wa Chadema, Mbowe alisema inaonekana Serikali ya Awamu ya Nne haijajiandaa kuachia madaraka na hivyo kuna uwezekano wa kuomba iongezewe muda.“Hadi sasa hakuna tunachojua wala kuelezwa. Hofu yetu ni kwamba Serikali inaweza kuomba iongezewe muda kwa kuwa usajili wa wapigakura hautakamilika,” alisema.“Kama uandikishaji wapigakura wa mwaka 2010 ulifanyika mwaka mmoja kabla, hawa watawezaje kukamilisha katika miezi mitano tu tena kwa kuandikisha kwa BVR?”

No comments: