Thursday 30 July 2015

LOWASSA KUHAMIA CHADEMA/UKAWA: NI TAMU NA CHUNGU NA TUVIPOKEE VYOTE:

Na. Julius S. Mtatiro

Faida na hasara zake kwa CHADEMA, UKAWA na Upinzani na LOWASSA kwa ujumla.
A: FAIDA KWA CHADEMA/UKAWA

1. Kupata wanachama wengi kwa makumi elfu kutoka CCM
2. Kupata viongozi wengi wakubwa kutoka CCM, wabunge wa CCM n.k
3. Kupata Mtandao wa ushindi na mbinu za ushindi za CCM kwa sababu mtandao 
wa Lowassa ndiyo ulisimamia ushindi wa kishindo wa JK mwaka 2005 – Hizi zitaisaidia CHADEMA/UKAWA iwe na nguvu ya ziada ya kushinda uchaguzi na kuongoza dola.
4. Kupata msaada mkubwa wa mbinu na mikakati ya usalama wa Taifa ambayo hutumiwa na CCM kushinda uchaguzi na kuitafutia mbinu mahsusi za kuzuia isitendeke kwa sababu siyo siri kuwa huko Usalama wa Taifa LOWASSA anajua kila kinachopangwa.
5. UKAWA kuwa na uwezo au KUSHINDA uchaguzi mkuu wa mwaka huu au kupangua hila zote zinazoweza kukwamisha ushindi wa umoja huo.
B: HASARA KWA CHADEMA/UKAWA
1.Kuwa na kazi kubwa ya kumsafisha Lowassa ambaye huko Nyuma aliwahi kutangazwa kama mmoja wa mafisadi (Huwenda hili likawezekana kwa sababu ya “CHARISMA” (MVUTO) yake kisiasa; yaani kupendwa sana na makundi ya vijana, bodaboda n.k ambayo ni wapiga kura wengi japokuwa kama halitaelezwa vizuri na kueleweka litakuwa na DAMAGE kuwa kwa upinzani.
2.Kuwa na kazi kubwa ya kudhibiti tabia za wanachama, viongozi, wabunge na wapambe wengi wa Lowassa ambao watahamia upinzani ghafla (Hili linaweza kuwa suala la muda mfupi) na kujizatiti kila mara kuwarekebisha bila kuvurugana nao kwa sababu wanahitajika sana.
3.Hatari ya viongozi wengine wa CHADEMA/UKAWA katika ngazi mbalimbali (Matawi, Majimbo, Wilaya, Mikoa, TAIFA n.k.) kukasirishwa na hatua ya KUPOKELEWA KWA LOWASSA na kuamua aidha kususa kampeni zake, kutoshiriki kabisa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kuhama vyama vya UKAWA kuelekea ACT, ADC au CCM (Hili litatokea kwa kasi japo kwa idadi ya kawaida ya DEFECTEORS mara Lowassa atakapopitishwa kuwa mgombea urais) na kuna viongozi wengine wa CHADEMA/UKAWA wenye misimamo wataamua kustaafua kabisa siasa.
4. Hatari ya UPINZANI kutoaminika kwa dhati katika ajenda ya kusimamia ufisadi na rushwa na ajenda hizo zinaweza kupokwa tena na ACT au CCM wakidai wao ndiyo wapingaji wakubwa wa rushwa (Hili linaweza kutokea ikiwa hatua ya kumsafisha LOWASSA itagonga mwamba).
Kesho ntagusa FAIDA na HASARA kwa LOWASSA mwenyewe!
KUMBUKA:
Kila unapofanya uamuzi wowote ule kuna FAIDA na HASARA zake! Na kwenye mchakato wa kusimamia uamuzi huo faida na hasara hizo zinaweza kutokea au kutotokea. Haya nayoyasema hapa yanaweza kutokea au kutotokea.
Jadilini kwa uhuru kabisa! Hii ni nchi yetu sote!
J. Mtatiro 

No comments: