Friday 12 May 2017

SERIKALI YA NCHI YA KUSADIKIKA IMEGEUKA BUCHA YA RAIA WA NCHI YA KUSADIKIKA.

SERIKALI YA NCHI YA KUSADIKIKA IMEGEUKA BUCHA YA RAIA WA NCHI YA KUSADIKIKA.
Taarifa kutoka Pemba zinaeleza kwamba abiria wameshindwa kuendelea na safari kutokana na Barabara ya Changaweni kukatika na kusababisha abiria wanaotoka Mkoani kwenda Chakechake kushindwa kupita, kama picha zinavyoonekana. Na kutoka Mjini kwenda Makunduchi pia njia ipo kama hivyo


Niambieni ikiwa Juzi Muheshimwia Bwege kasema miaka hamsini tunashindwa hata kuwapa raia wa nchi ya kusadikika maji safi na Jana Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi huko Zanzibar kutoka chama tawala kasema tawireni tumeshindwa kuongoza nchi  akiishutumu ofisi ya Makamo wa Rais ,  kuwa inajenga miundo mbinu ilio chini ya Viwango jee bunge na Baraza la nchi yetu ya kusadikika nayo pia yamekumbwa na butwaa la Mafuriko ,


 Zitto Kabwe anasifu kuwa Professor Kitila Mkumbo, sasa maji yatatatiririka hadi Ikwiriri kwenye mashamba .
*****************

Auta continua time will tell 2020 tuombe uhai.Tumejifunza mengi Kuanzia mafuriko ya Mtwara , Kuzama kwa meli ya MV Bukoba , Mafuriko ya Bukoba , Kuzama kwa meli mbili huko Zanzibar na watu kusubiri Jeshi la kutoka Afrika kusini kuokoa maiti sio kuokoa watu walio hai .Hili taifa la kusadikika Nakumbuka lina JESHI LA WANANCHi YA NCHI YA KUSADIKIKA ,Jana NAmsikia Bamkwe asema watu watu laikau anawatizama tu yeye kwa vile wamejenga mabondeni kweli nchi mzima kuanzia huko Tanga , Pemba na Unguja wamejenga Mabondeni na kwa nini tumejenga madaraka na barabara za viwango hafifu , jee Lini tutaunda Idara maalum ya kukabiliana na Majanga ya kitaifa na mabadiliko ya hali ya Hewa ?



 Nakumbuka huko nyuma JEshi hili lilweza kuonesha umahiri wake kuweza anagla kuweka madaraja ya muda kuhakikisha huduma za nchi ya Ria wa kusadikika wanrudi kwenye maisha yao ya kawaida kwa haraka pale yanapotokea majanga .Tukomae Miaka 50 sio bado Taifa changa sio tujisifie tu kwua tunawakamua Raia wa nchi ay kusadikikika kodi nyingi hadi tunawavizia usiku wa manane kwuakamata wasanii walipe kodi kabla ya kuimba nyimbo zao na bila kujua watu wangapi wataenda kuwasikiliza hawa wanamuziki.Kodi hizi tunazojisifia tuzione kwenye kubadilisha maisha ya Rais wa Nchi ya Kusadikika.Tujifunzeni kwa nchi za wenzetu Wanajeshi wao ni Walinzi wa maisha yao ikiwamo kuokoa maisha yao wakati wa dharura sio kuwalinda wakubwa na kuwapigia saluti.Juzi Niliona Taifa likiomboeza watoto wadogo wlaiopotezwa uhai wao lakini kwa nini hatuombolezi 14000 Raia wa Nchi ya kusadikikia waliopoteza maisha yao kwa jali ya barabarani ?



Ningempa Ushauri Rais wangu WAziri wa Mambo ya Ndani na Brigade yake hawafai ,Tafuta Brigedia mmoja aongoze hii Wizara aifumue upya na kustaafisha wengi wasiokidhi maslahi ya taifa hili .Tumkubalie Rais Wiazara hii wapewe Wanajeshi wiajenge upya kwa kuingiza Wataalamu wapya na kuwa na Jeshi dogo lenye kuheshimi haki za Binadamu, Kuwa na Jeshi la Polisi lenye kuvutia hata wawekeza ji wa nje Kuwa nchi ya kusadikika ni nchi ya salama inaweza kulinda raia wake na sisi wageni tuende kuekeza , leo JEshi la Polisi hata kujilinda wenyewe limeshindwa wanauliwa na Majambazi ,Nimshauri Rais kuwa katika sehemu ya uongozi wa nchi hii ya kusadikika iliooza basi ni Wizara ya Mambo ya ndani Fire Fighter(WAZIMA MOTO) hufika baada ya Nyumba kumaliza kuungua na miili ya binadamu kuwa imemaliza kuungua .



Ikiwa Nchi ya kusadikika itahitaji utaalamu au wataalam u kutoka nje ya mipaka yetu kujenga JESHI Jipya La Polisi basi tusione Aibu kuwapa short contract kama alivyofanya Rafiki yetu Kagame hakuchagua Ria wa nchi bali alitafuta Wataalam u ambao kwa mda ule wangesaidia kuleta mabadiliko Serikalini huko Rwanda na Rwanda ndio ikafaika hapa ilipofika leo na Kagame kuonekana ni New Hero wa AFRIKA.

No comments: