Friday, 7 December 2012

Muundo wa Muungano ni Ajenda ya Kitaifa na inawahusu Wazanzibari wote bila kujali vyama vyao

Leo nitawakumbusha CCM jinsi chama cha Republican cha Marekani kilivyoweza Kupoteza madaraka ya uchaguzi uliopita ni kutoweza kukaa na kufikiria nini ajenda muhimu wanachi wanataka irekebishwe katika maisha yao ya kila siku .George Bush aliona vipi ajenda ya uhamiaji ifanyiwe kazi kwa manufaa ya chama chake aliwaita chama cha Upinzani cha Democrat na walikuabaliana na mswada wake wa kurekebisha mswada wa Wahamiaji Haramu lakini la kushangaza Rais alieoko Madarakani Mswada wake ule ulipingwa na wahafidhina wa chama chake . Uchaguzi wa Wabunge uliofuatia wahafidhina wale wote walioupinga mswada wa uhamiaji hawakurudi tena Bungeni kwani wanaotaka mabadiliko walifanay kamepni ya kuhakikisha watu hao hawarudi tena Bungeni. Ingawa utawala wa miaka minane wa Bush lakini wapinzani wake hawakuieka kapuni ajenda hile ilikua katika manifeso ya chama chao. Alipokuja Sanator Maccain alipoapambana na Senator Obama ajenda hii pia ilidharauliwa na kwenye kipindi cha CNN Mshauri wa Sanator Maccain Steve Schimid kuwa Moja lililomuangusha bosi wake ni ajenda ya uhamiaji hakuipa uzito bali na yeye alirudi kwenye historia ya chama chake ya kutaka aonekane ni hafidhina kwa vile alionekana ni hafidhina wa uliberali. Matokeo yake ajenda hii limsaidia Senator Obama kuingia madarakani Obama aliingia madarakani kwa kuipigia debe pia ahadi hii ila ilikua kwenye kipindi kigumu kwake hali ya uchumi wa Marekani ulikua umeanguka na wamarekan wengi wengi mda ule walifikiria vipi Kazi ziongezeke ili wapate mkate wakila siku .Hoja ya uhamiaji iliwekwa kapuni kipindi chake cha kwanza. Uchaguzi uliofuatia Republican wakati wa kupigania nani anateuliwa kukiwakilisha chama hicho kila mmoja aliisahau ajenda hii bali kila mmoja alitaka aonekane yeye ni hafidhina zaidi .Mitt Romney aliswashinda wenzake kwanza kwa kuwa na pesa nyingi zaidi na pia yeye aliweza kuwangusha wenzake kwa umilionea wake na rafiki zake walitoa mchango wa pesa nyingi na kempeni yake ya nguvu ya pesa kwneye vyombo vha Habari ilisaidia kushinda kidedea na kuwa ndio Mshika Bendera wa Chama chicho. Aliekuwa Waziri wa Biashara wa Bush alimuunga mkono Romy Waziri huyu ni Mspaniola Carlos Guterez alifanikiwa kuchangisha milioni $142 kumsaidia Mitt Romney ashinde urais kwa kumuahidi kuwa hoja ya Uhamiaji itashughulikiwa na wafadhili wa Guterez waliokubaliana nae kumuunga mkono amsaidie Romney waligundua kumbe wamefanya makosa kwani Mgombea wao aliidharau hoja hiyo na mwishowe kuipiga Msumari wa Mwisho waliposema wageni haramu waondoke wenyewe yeye akishinda Urais . Matokeo yake yale alioyaona Bush kua jamii ya kilatina imekua kubwa Marekani haiwezi kudharauliwa tena ina kura za kutosha chama chake lazima kibadilike kisiwe cham acha wazungu watupu wahafidhina . Matoeko yake Obama alifanyia kazi na kuiweka kwenye manifesto yake ya Kampeni na matokeo yake .Pia kuna gavana Mmoja wa Jimbo la New Jersey wakat iwa kampeni alimuidhinisha Obama kuliko mbombea wa chama chake ingawa alionekana ni msaliti ila alisema Obama ameonesha uongzi wake shupavu. Yote hapa yaliotokea asubuhi ya ushindi wa Obama wahafidhina wengi maarufu walikwenda kwenye redio na TV kumtaka Obama wafanye kazi pmoja kurekebisha mswada wa uhamiaji baada yakuona ukweli wao wenyewe kuwa uhafidhina hauna nafasi tena ndani ya Marekani na inategewa baada ya kuapishwa Obama mswada huu utarudi bungeni na kuwa na support ya vyama vyote . Lengo Langu leo ni kuwakumbusha CCM wa Zanzibar kuwa musipokubali kubadilika na kumsikiliza Mwandishi Magidd Mjengwa anavyosema ukubali kuenda na wakati ukishindwa kuzisoma alama za nyakati utachukuliwa na mawimbi. Ajenda ya Muungano kwa Wazanzibari ilipingwa toka pale Muungano unaundwa na wengi waliokuwa ndani ya Baraza la Mapinduzi waliona madaraka ya Zanzibar yametekwa nyara na walipiga kelele ila kipindi cha vita Baridi na mfumo wa Chama kimoja waliokuwa wakipinga Muundo wa Muungano huu ni wengi ila hawakuwa na nguvu walisema kichini chini hadi sio siri tena ikawa ndani ya Baraza la Mapinduzi hadi kwenye Bunge Kuu la Dodoma, Mbele ya Mwenyekiti wa Chama hicho cha CCM Mwalimu Nyerere na wa Kwanza kumfunga paka Kengele ndani ya CCM kwa Upande wa Zanzibar alikua ni Rais wa Pili wa Zanzibar Mzee Aboud Jumbe aliweka bayana kutaka mfumo mpya wa sriakli tatu na hata kuajiri wanasheria Kumshauri kuweza kujinasua na Muungano huu aliouona unawadhulumu Wazanzibari matoeko yake CCM walimuondoa kwa guvu ya Bunduki kumlazimsha kujiuzulu na Kufungwa kifungo cha Ndani huko Kigamboni kwa miaka kadhaa ndio kaachiwa kutembea kama raia huru na Aboud Jumbe alimalizia kuandika vitabu kuwalemisha watu atahari za muunagno huu. Likaja Kundi la Mweka Hazina Mkuu wa chama Cha Mapinduzi na Waziri Kiongozi a Zanzibar Seif Sheriff Hamad walipoigusa ajenda hii moto na wo wlaifukuzwa uanachama Kule Kizota Dodoma Kundi hili walikuamo Mbunge wa wawi Hamad Rashid na , Mzee almarhum Shaban Mloo , Sud Yussuf Mgeni na Viongozi kadhaa w seriakli wlaitolewa kwa kuonekan hawa ni maadui wa muungano. Wengine walitupwa Jela na wengine kukimbilia nje uliporudi mfumo wa vyama Vingi Harakati za chin iwka chini zilikuja dhahir na Kamati ya KAMAHURU ikazaliwa na matoeko yake Chama cha CUF kikaundwa Kwani mwalimu aliliona Wignu la mabadiliko la Zanzibar linakuja ndio akaja na njia ya kusema kuwa Vyama viwe vya Kitaifa lakini KAMAHURU WAalihakikisha kigingi hichi wanakichupa waliweza kumpata Mapalala na CCW kuuunganisha na Kamahuru na kupatikana CUF leo ajenda iliokuwa siri imerudi tena uwanjani kwa style mpya .Nilifikiri CCM mda wote huu watakua wamepata somo nilifikrii ile dana dana yao ya vikao vya kuuzungumzia matatizo ya Muungano imewachosha Wananchi na matokeo ya hivi karibuni ya Jumuia za kidini kama Uamsho walipoizungumzia ajenda ya muungano ilileta muamko au mripuko Kwenye jamii na kuweza kusababisha Serikali ya CCM kuwatia ndani viongozi wa Uamsho kwa kiwewe cha woga . Ila hoja hii ya Muungano inaonekana imeshika kasi Zanzibar hasa Kwenye mchakato wa Katiba Wazanzibari wengi wameonesha kuirudisha tena ajenda hii hewani hata Kumshangaza Jaji Warioba na kubaki kushika tama kila anaetoa maoni huko Zanzibar anataka Muungano wa Mkataba tofauti na huu na pia Chama cha Upinzani cha CUF kuja nacho kimeiteka nyara hoja hii kwa style ya upepo unavyoenda kwani chama hichi huko nyuma kilikua na sera yake ya Serikali tatu na sasa Katibu mkuu Wa Chama hicho ameonekana kuja na msimamo wa watu walio wengi kuunga mkono Muundo wa Mkataba wa serikali mbili za Mkataba na Kujitangaza Rasmi yeye ni muumini wa Muungano wa Mkataba . Lakini la Kufurahisha ni kuwa yale yale yaliowakuta Republican kina Senator Martinez wa FLorida kutaka ajenda ya uhamiaji ipewe Kipaumbele ndani ya chama chao kudharauliwa . Hata kwenye CCM Zanzibar wako Walioona athari ya ajenda hii ya Muungano kuwa itawanufaisha Wapinzani tu Wako walioona umuhimu kujitoa muhanga kukiokoa Chama chao Mfano Mzuri ni kina Mzee Hassan Nassor Moyo Waanzilishi wa Chama hichi waliokuwa wazi na kutaka Mfumo wa Muungano ubadilike na kusema vijana wa Kizanzibari leo wamesoma na hawdanganyiki tena waacheni warekebisho makosa ya Muungano huu na Waziri Mansour Yussuf Himidi hawa ndio watoto wa Wanapinduzi tunavyoambiwa ila wamejitoa muhanga Kuyalinda Mapinduzi kwa kukubaliana na Muundo wa Mkataba na matokeo yake Waziri huyo alitolewa kwenye nafasi yake ya uwaziri kwa kutoa msimamo wa kukitaka chama chake kikubali mabadiliko ya mfumo wa Muungano na Juzi tumesikia Waziri aliekuwa katika Serikali ya Karume Mwana CCM alieidhinisha maoni yake kwa kutaka mfumo wa Muugano ubadilke. Labda tungewaomba walio na ajenda hii waongze kuwalemisha Raia juu ya Muundo mpya wa Muungano utolewe Waraka Rasmi unaeleza Muungano wa Mkataba ili wafuasi wawe wengi zaidi na Harakati za kuwataka watu watoe maoni kwa wingi kabla ya kusubiri Kura ya maoni. Nawakumbusha CCM tu kuwa Matatizo ya Muungano ni ajenda ya kitaifa sio ya kichama nilitegemea vugu vugu la karibuni la kudai serikali mbili za Mkataba nilitegemea CCM wangekuja wazi na kusema hii ajenda ya serikali mbili ni yetu na tutakubali kufanya muungano waMkataba wa serikali mbili lakini la wameshindwa ku catch the moment of the truth .Mabadiliko ya kisiasa ukishindwa kuyaona yanakuja mawimbi yake yatakuzoa kama Moi , Kaunda na karibuni Gadafi na wenzake Wengine wa Egypt na Tunisia. Wazungu wakaipa jina Arab Spring. Ajenda hii CCM wangekua makini vugu vugu la mabadiliko lingekua kimya kwani wangekuwa pamoja na Wazanzibari na kuonesha wamesikia kilio cha Wazanzibari lakini wameonesha kukosa kusoma lama za nyakati. Nimpongeze Karume kwa Kuweza kuwa Mkweli na kuonesha msimamo wake hata ukiwa hautampa umaarufu lakini una umuhimu wa mustakabali wa Kitaifa alikikuta chama chake vipande vipande kwa mgawanyo aliouleta Komandoo Visiwani na Visasi vya kisiasa na kuleta Vifo visivyokuwa vya lazima kwa utawala wake wa Mabavu na kuwanyanyasa Wapemba wazi wazi kwa kuwatoa makazini kisa Wapemba ni CUF na wao ndio waliomungusha kwenye utawala wa Mwaka 1995 aliaoangushwa ilibidi Mwalimu Nyerere ahubiri mseto na kumsihi Salmin aunde serikali ya Mseto kwa vile ilijulikana wazi CCM Zanzibar walianguka kwenye uchaguzi ule na Mwalimu aliisoma hali ya ZNZ na kujua kuwa Chama chake hakina tena uwezo wa Kuwaongoza Wazanzibari bila ya CUFimechukua miaka kumi na tano ndio serikali ya Mseto kuundwa Visiwani. Nitawaeleza vipi Karume aliweza kupunguza upinzani wa Mgawanyiko Zanzibar kwani ilikua inaonekana wazi na Wapemba wote waliamini hivyo ile kauli za wazi wazi za Wanamapinduzi kua Mpemba hawezi kupewa nafasi ya juu kuongoza serikali ya Mapinduzi hasa baada ya aliekuwa Waziri kiongozi kutolewa na kufukuzwa CCM baada ya kumshinda Mpinzani wake ndan i ya uchaguzi wa CCM wa wakati huo baina ya Seif Sheriff Hamad na Mzee Abdul Wakil Nombe lakini Karume ameizika dhana hii kwa kuhakikisha Ris anaemrithi anakua Mpemba alikubali kubadilika kama Walivyokubali kuwa na Rais Mkatoliki J .F Kenedy au Wamarekani kukubali kuwa Rais Mweusi Barak Obama hapa Karume alitumia Kura za kisisasa ipasavyo kama alivyofanya Odinga kumuangusha Uhuru Kenyata kuhakikisha Wahafidhina wa CCM waliomuhofia Kijana Seif Sheriff Hamad ya CCM na kuenda Dodoma Kumlazimisha Mwalimu Nyerere awafukuze kundi linaloibuka kuwa na nguvu ya wananchi Vijana wasomi wa Zanzibar linalodai mabadiliko,kama leo wanavyomhofia Kijana Mansour Yussuf Himidi kudai mabadiliko hayo yalikuapo kweli ndio ajenda hii hii inayoitwa ya UAMSHO ajenda hii hii iliotiwa kapuni ya Muungano ila iligeuzwa siku hizo Kamba ya kuwanyonga wale waliotaka mabadiliko. Mpasuko ule wa CCM wa kuwafukuza kina Hamad na kundi lake uliipa CCM Mpasuko mkubwa ndio huu tunauona leo umekua CUF chama pinzani kwa upande wa Zanzibar na sijui CCM itakubali kuwa na mipasuko mingapi ya kisiasa ndio isome au iwasikilize Wazanzibari au itakumbwa na kundi la Mabadiliko.

No comments: