Saturday 5 October 2013

UMOJA WA UPINZANI TANZANIA WAMTIA KIWEWE KIKWETE NA CHAMA CHAKE AWAITA IKULU WAPINZANI KWA MAJADILIANO.

NGUVU YA UMMA YA UMOJA WA UPINZANI TANZANIA   ILIMTIA KIWEWE RAIS KIKWETE ALIPORUDI MAREKANI , ASALIMU AMRI AWAITA WAPINZANI IKULU NA KUSEMA KILA KITU KINAZUNGUMZIKA NA MUSWADA WA KATIBA URUDISHWE BUNGENI UPYA !




Huu ni Ushindi wa Kishindo Kwa Umoja wa Vyama vya upinzani  Tanzania leo Imefika wakati Rais kuwaomba na kuwanyenyekea wasiendelee kuibomoa CCM nje ya Bunge kweli Upinzani ukisimama as one block CCM inapata Kiwewe. Wale Wahafidhina wa CCM waliosema Kikwete akirudi Marekani asaini Mswada wa Katiba uliopitishwa karibuni na Wabunge wa CCM tu  wamepigwa na chini na wale wana CCM waliothubutu kusema RAS Kikwete asipousaini atakuwa amevunja katiba sasa tuwasikie kwenye majukwa wamlaani Rais amevunja katiba kuurudisha bungeni mswada huu ! , Upinzani hata nje ya bunge unaweza kuleta mabadiliko huu ni mfano tosha wingi wa CCM ndani ya bunge sio Wamiliki wa Katiba Mpya , Rais Kikwete amewajibu kwenye hotuba yake Katiba hii sio ya chama fulani  , pia niwapongeze Wazanzibari waliosimama kuitetea Zanzibar madai ya Zanzibar hayatorudi nyuma ndani ya bunge na nje ya Bunge watakaojaribu kuibeza Zanzibar madai yake maana yake hawautakii mema Muunagno huu  . ! sikiliza hotuba hii ya karibuni ya Kikwete wahafidhina mutapata majibu



No comments: