Tuesday, 18 February 2014

KIFICHO NDIO CHAGUO LA WAHAFIDHINA WA CCM KWENYE BUNGE LA KATIBA

Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Yahya Hamad Khamis, akitowa maelezo ya kumpata Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba  huko DODOMA ili kuwezesha kupata Kanuni za kuendesha Bunge hilo wakati wa Kikao chake baada ya kufanyika Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge hilo na Makamo Mwenyekiti wake. Na kutaja Wajumbe waliojitikeza kuomba Nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Muda waliojitokeza ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho, , Mhe, Magdelina Rubangira, na Profesa Costa Mahalu. ndio walioomba nafasi hiyo ya muda.  Zoezi la Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Tanzania wakiendelea nazoezi hilo la upigaji wa kura kumchagua Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo huko katika ukumbi wa bunge Dodoma jioni hii. Katika zoezi hilo jumla ya Wajumbe watatu wawania  nafasi hiyo, uchaguzi wa kwanza umeahirishwa kutokana na Wajumbe wake kuzii baada ya kupigwa kura kutokana na baadhi ya Wajumbe wamekuwa nje ya Ukumbi na kutohesabiwa wakati zoezi hilo likifanyika.  
                                                                                          
ilibidi zoezi hilo kurudiwa tena baada ya kuingia wajumbe watano na kufungwa milango ya ukumbi kuweza kuaza zoezi hilo ili kama Mjumbe yuko nje asiigie na kuzidisha idadi itakayohesabiwa wakati wa kugawa kura.
Mshindi wa Kura za kumtafuta Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Maalum la Katiba Tanzania Mhe. Pandu Ameir Kificho, akiongoza Mkutano wa Maandalizi ya kuandaa Kanuni za Bunge hilo. Baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo kwa ushindi wa kishindo wa kura 393.sawa  asilimia 69.19. Mhe Pandu Ameir Kificho, akitowa shukrani kwa wajumbe wa Bunge Maalum kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo 

Katibu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Thomas, akitangaza matokeo ya Uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba Tanzania, Katika zoezi hilo la uchaguzi lililofanyika katika ukumbi huo limemchagua Mhe. Pandu Ameir Kificho kwa kura 393, dhidi ya wapizani wake walioibuka na kura 84 kila mmoja Profesa Costa Mahalu amepata kura 84 na Mhe Magdelina amepata pia kura 84, katika uchaguzi huo uliowashirikisha Wajumbe wa Bunge hilo leo jioni. 

No comments: