Saturday, 1 November 2014
MAFUNZO YA BUKINAFASO
Kuiyondoa madarakani serikali ilipo,haya ni maamuzi ya wanachi kumtaka rais wa nchi hio Bwana Compaore aondoke madarakani mara moja,na jengine zaidi wananchi hao kupinga kwa kubadilishwa katiba ya nchi hiyo ili rais huyo andelee kutawala.Compaore ameingia madarakani katika koloni hilo la zamani la Ufaransa hapo mwaka 1987 kwa njia ya mapinduzi.Alimuuwa kiongozi mashuhuri Thomas Sankara ambaye aliziteka nyoyo za watu kwa unyenyekevu wake na msimamo wake wa kimapinduzi.Baada ya kuuwawa kwa Sankara na wengine walioitwa “wasaliti”,Compaore alijitawaza kama mlezi halisi wa “mapinduzi ya kidemokrasia ya wananchi”. Lakini licha ya kuwa madarakani kwa miaka 27 aliendelea kutuhumiwa kuwa dikteta licha ya kuruhusu vyama vingi na vyombo vya habari nchini humo.Hapo mwaka 2000 aliruhusu katiba ifanyiwe marekebisho kwa mara ya kwanza ili aweze kuendelea kubakia madarakani.Mara kwa mara amekuwa akiyavunja kwa kutumia nguvu maandamano ya kisiasa na kijamii mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 2011.
Ingawa bwana Compaore alijaribu kuwazima wapinzani wake, lakini kila jambo lina mwisho wako,vijana hivi sasa wameamka, alivikiria wale vijana wa miaka hio alio pindua atawaburuza zaidi ya miaka inavyokwenda, ukiangalia katika mapinduzi haya ya umma, ni vijana ambao chini ya umri wa miaka 30, ambao wamezaliwa baada au kabla ya mapinduzi ya bwana Compaore, hii ni funzo tosha kwa viongozi wa africa kutambua kwamba Vijana wa miaka ya sasa hivi ni nguvu na jeshi la kazi ambalo halijali lolote wala woga wowote.
Tuje kwetu Tanzania/Tanganyika na Zanzibar.
Tumeshuhudia katiba bunge la katiba miezi iliyopita jinsi ya viongozi wa zanzibar wakihubiri mapinduzi na ubaguzi, walitamka hadharani ya kwamba zanzibar tumepindua na nchi haitotolewa kwa karatasi or papers, wamesahau kwamba vijana wa leo, sio waoga, ila tuna ustarabu flani na uvumilivu, lakini wafahamu viongozi hawa siku vijana wakichoshwa na uvumilivu ,nchi haitatawalika, na mapinduzi mapiya yatapatikana. Tukianza sisi zanzibar Tanganyika wanamaliza, wakianza Tanganyika zanzibar tunamaliza.Viongozi hawa walio hubiri mapinduzi daima ,kamwe hawatotoa nchi kwa paper,wafahamu ya kwamba pale vijana wakiamua na kuchoshwa na viongozi na ukiritimba wa viongozi na dhulma juu yao,viongzi hawa wajue kuwa hawatasalimika, wajifunze nchi zilizo fanywa mapinduzi, kama Libya,Tunisia,Egypt na hivi karibuni Burkina faso, tumeshuhudia wananchi wenye hasira wakivamia nyumba za viongozi, ndugu zao viongozi, na kuharibu mali zao ambazo zimetokana na rasilimali za nchi yao kwa dhulma, hivyo hawa wote hapa zanzibar na huko tanganyika wasijidanganye kabisa, siku 40 zao zikifika, hayo makasri yao watayakimbia, watahama nchi wenyewe, tunawatahadharisha waachee mara moja kuhubiri mapinduzi, kwani mapinduzi hayana mwisho, wala mwisho mwema, hayachagui.
Mpango wa kubadilisha katiba ya zanzibar na kupitisha rasimu ya vijisenti.
Hivi sasa tunafahamu ya kwamba ccm ipo katika mikakati yao ya kufanya uchakachuaji ili kuahakikisha rasimu ya ya vijisenti inakubalika kwa nguvu zote, hasa hapa kwetu zanzibar kwenye upinzani mkubwa, ccm tayari wameshaandaa hilo,tuna watahadharisha sana sisi wananchi,kama wana planing hizo wawache mara moja ,kama nchi yetu wanaitakia mema, nawahakikishia mara hii,kama munafikiria mutafanya kama yale mulio fanya huko katika bunge la katiba na chaguzi zilizo pita, mufahamu kuwa nchi haitatawalika, na kama munataka kujaribu jaribuni.
Tunafahamu jengine la kutaka kupunguza majimbo ya Pemba pia na kuongeza Unguja ,ili katika uchaguzi 2015 muyaibe majimbo ya unguja mengi,kuweza kupata theluthi mbili ndani ya baraza la wakilishi, theluthi mbili hii muweze kuitumia katika kuvibadilisha vifungu vya katiba yetu, ambayo inatamka kuwa ni nchi na mipaka yake, rais kugawa mikoa, kuondoa kifungu cha kura ya maoni.
Tunawapa tahadhari sisi wananchi wa zanzibar kamwe mara hii hatutakubali,na kwa umoja wetu, tuko tayari kwa lolote,lakini tutahakikisha kwamba zanzibar inapata heshima yake, na kuheshimiwa katiba yetu, muache kujidanganya madaraka yenu, na kudhani kwamba hatuwezi kuwawajibisha, sisi wananchi tukiamua waajibisha tutawajibisha kwa mikono yetu, na sio mahakama zenu za ukanda
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment