Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na viongozi wa majimbo pamoja na wagombea wateule wa chama hicho kwa majimbo ya Unguja, katika mkutano maalum wa kuwatambulisha wagombea uliofanyika hoteli ya Bwawani.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui, akizungumza na viongozi wa majimbo pamoja na wagombea wateule wa chama hicho kwa majimbo ya Unguja, katika mkutano maalum wa kuwatambulisha wagombea uliofanyika hoteli ya Bwawani.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ametoa wito kwa wanachama waliochaguliwa kugombea nafasi za Ubunge na Uwakilishi kupitia chama hicho, kushirikiana na wale wasiopata uteuzi pamoja na wanachama wote, ili kujenga mazingira bora ya ushindi katika uchaguzi mkuu ujao.
Maalim Seif ametoa nasaha hizo huko hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar, katika kikao maalum cha kuwatambulisha wagombea wateule wa chama hicho kwa nafasi za Ubunge na Uwakilishi kwa majimbo ya Unguja.
Amesema wakati wa kugawana makundi umepita, na kwamba sasa ni wakati wa kuendeleza mshikamano ndani ya chama kwa lengo la kukiimarisha chama kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Baadhi ya viongozi wa majimbo ya Unguja (CUF) pamoja na wagombea wateule wa majimbo hayo, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, huko hoteli ya Bwawanmefahamisha kuwa chama hicho ngazi ya Taifa kupitia Baraza Kuu la Uongozi, tayari kimeshafanya maamuzi ya wagombea kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na kuwataka wale wasioteuliwa kutovunjika moyo, na badala yake waungane na wateule hao katika kukipatia ushindi chama hicho.
Akizungumzia kuhusu wagombea wa Jimbo la Rahaleo, Maalim Seif amesema kulibainika kasoro kadhaa kwenye uchaguzi wake, na hivyo Baraza Kuu likaamua kurejewa kwa uchaguzi huo katika siku chache zijazo.
Amewapongeza wagombea wateule hao wa nafasi za Ubunge na Uwakilishi kwa kuteuliwa kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao, na kuwataka kufanya kazi ya ziada ya kukitafutia ushindi katika ngazi zote.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui, amewatahadharisha walioteuliwa kuwa bado hawajashinda, na kwamba Chama ndicho kilichoshinda kwa kufanikiwa kupata wagombea hao.
Amesema hatua inayofuata sasa ni kwa wateule hao kufuata maagizo ya chama na kuyafanyia kazi kikamilifu kwa lengo la kukiwezesha kutimiza malengo yake.
“Sote ni wamoja, sote ni wanachama wa CUF, hakuna mshindi wale aliyeshindwa bali kilichoshinda ni chama chetu, turejeshe imani zetu kwa chama na kwa hao waliopata uteuzi”, alisisitiza Mazrui ambaye pia ni mgombea mteule wa nafasi ya uwakilishi jimbo la Mtoni.
Baadhi ya viongozi wa majimbo ya Unguja (CUF) pamoja na wagombea wateule wa majimbo hayo, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, huko hoteli ya Bwawani. (Picha na Salmin Said, OMKR)
No comments:
Post a Comment