Monday, 26 October 2015

Matoeko ya uchaguzi yaliotanganzwa na tume ya uchaguzi



17:33
MATOKEO UBUNGE: Anthony Mavunde (CCM) ametangazwa kuwa mshindi wa ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Joram Hongoli (CCM) akishinda Jimbo la Njombe Kaskazini, Edwin Sanda (CCM) ametangazwa mshindi Jimbo la Kondoa Mjini na Dotto Biteko (CCM) ameshinda ubunge Jimbo la Bukombe.

17:30
MATOKEO YA UBUNGE: Esther Bulaya (Chadema) ameshinda ubunge Jimbo la Bunda Mjini na kumuangusha Steven Wasira, huku Jaffar Michael akishinda ubunge kwa tiketi ya Chadema Jimbo la Moshi Mjini.

16:54
MATOKEO YA UBUNGE: Jumanne Kishimba (CCM) ameshinda Jimbo la Kahama Mjini, Steven Masele ameshinda Jimbo la Shinyanga Mjini, Hussein Bashe ameshinda Jimbo la Nzega Mjini na Silvestry Koka ameshinda Jimbo la Kibaha Mjini.

16:52
MATOKEO YA UBUNGE: Jimbo la Monduli limechukuliwa na Julius Kalanga (Chadema), Joshua Nassar ameshinda tena Arumeru Mashariki, Jimbo la Serengeti limekwenda kwa Marwa Ryoba (Chadema)

16:02
WANANCHI wa Manispaa ya Musoma wakishangilia ushindi wa mbunge mteule wa jimbo hilo, Vedastus Mathayo



15:47
UCHAGUZI TANZANIA: Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewataka wanachama wake wapuuze matokeo yanayotangazwa kwenye mitandao ya kuijamii na vyombo amabayo havina mamlaka

15:43
KUTOKA ZANZIBAR: Kumekuwa na hali tete kwenye baadhi ya maeneo visiwani Zanzibar baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwawanaongoza kwenye matokeo ya urais, juhudi za kuipata Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuzungumzia jambo hilo zinaendelea. Tutaendelea kuwajuza.

15:29
UCHAGUZI TANZANIA: Mgombea ubunge wa Chadema jimbo Shinyanga Patrobas Katambi amegoma kuendelea kusikiliza kutangazwa kwa matokeo na msimamizi wa uchaguzi Kalinjuna Lewis, kwa madai kuwa hana imani na matokeo hayo na kuamua kutoka ukumbini na wapambe wake wakati matokeo ya kila kituo yakiendelea kusomwa. Hadi sasa bado hajatangazwa mshindi

14:46
UCHAGUZI TANZANIA: Jeshi la polisi mkoani Mtwara wilaya ya Tandahimba linawashikilia watu 8 kwa tuhuma za kuvamia na kubomoa nyumba ya msimamizi wa uchaguzi jimbo la Nanyamba.

14:42
UKONGA: Askari wa kutuliza ghasia wameongezwa kituo cha majumuisho ya kura jimbo la Ukonga baada ya zoezi la kuhesabu kura kurudiwa tena.

14:16
Wanachama wa CUF wakiwa wamekusanyika katika eneo la Mtendeni mjini Unguja, Zanzibar wakisubiri kutangaziwa mshindi wa kiti cha Urais katika Uchaguzi MKuu uliofanyika jana nchi nzima. Picha na Salim Shao




13:56
UCHAGUZI TANZANIA: Mgombea ubunge wa Chadema Bilago Samson amefanikiwa kunyakua Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kwa kura 23041. Jimbo hilo lilikuwa chini ya CCM kupitia Waziri Christopher Chiza aliyepata kura 22934.Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Kakonko, Jaina Msangi ametangaza matokeo hayo


13:46
Jimbo Buyungu
Ubunge: Bilago Samson Chadema), 23,041 na Christopher Chiza(CCM) 22,934

13:21
Jimbo la Siha
Ubunge: Dk Godwin Mollel (Chadema) 22,746 na Aggrey Mwanry (CCM) 18,584.
Msimamizi wa Uchaguzi, Rashid Kitambulio amemtangaza Dk Mollel kuwa mshindi wa jimbo hilo ambalo mbunge wake alikuwa ni Aggrey Mwanry (CCM).

12:25
Baadhi ya masanduku ya kura yakiwa yanaendelea kufikishwa katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Mvomero kutoka katika vituo.



12:06
Baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi jimbo la Kilombero wakibeba maboksi yenye kura wakati wa tukio la kujumlisha kura kutoka kata mbalimbali. Maboksi ya kura yanakusanywa ukumbi wa Halmashauri ya wilaya Kilombero mkoani Morogoro.



11:57
Jimbo la Tarime Mjini
Ubunge: Ester Matiko(Chadema) 20,017, Michael Kembaki(CCM), 14, 025, Deogratias Meck(ACT-Wazalendo) 356.

Msimamizi mkuu wa Uchaguzi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Juma Mwajombe amemtangaza Matiko kuwa mshindi katika Jimbo hilo

11:54
Jimbo la Tunduma

Ubunge: Mwakajoka Frank (Chadema) 32,442, Frank Sichalwe (CCM) 17,220, James Mwakalonge(TLP) 85, Reddy Makuba (ACT Wazalendo) , 319.

Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Tunduma, Halima Mpita ametangaza matokeo hayo.

11:49
Wakazi wa Tabata Mawenzi wakitafuta majina yao walipokwenda kupiga kura katika kituo kilichopo katika ofisi ya Serikali za Mitaa ya Kimanga Daraja, Dar es Salaam jana. Picha na Edwin Mjwahuzi



11:19
UCHAGUZI TANZANIA: Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Magu, Ntiniki Paul akiendelea kupokea matokeo kutoka kata za wilaya hiyo katika ukumbi wa halmashauri ya Magu.



11:10
Kura za baadhi ya kata za Handeni mjini zikishushwa asubuhi hii ili kujumlishwa.



11:06
UCHAGUZI TANZANIA: Matokeo ya jumla ya uchaguzi jimbo la Longido mkoani Arusha yanatarajiwa kutangazwa majira ya saa tisa mchana kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi Felix Kimario.

10:42
UCHAGUZI TANZANIA: Nec yatoa matokeo ya awali ya urais katika majimbo ya Paje Kusini, Makunduchi na Lulindi. Mgombea wa CCM, Dk John Magufuli anaongoza.

10:40
IRINGA: Matokeo ya awali Iringa mjini ubunge Mchungaji Peter Msigwa kashinda.

10:37
Msimamizi wa uchaguzi Arumeru Magharibi akizungumza na waangalizi wa EU.



10:28
Wapiga kura wakiwa kituo cha majumuisho ya kura kwa ZEC na NEC (Gombani Stadium) wakisubiri kutangaziwa matokeo ya majimbo matano ya wilaya ya Chake Chake.



10:15
UCHAGUZI TANZANIA: Tume ya Taifa ya Uchaguzi yaanza kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi

10:03
MWANZA: Barabara ya jiji la Mwanza yafungwa asubuhi hii huku polisi wakiendelea kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya watu wanaofuatilia matokeo.

09:39
Mtu mwenye ulemavu akipata msaada kuingia katika kituo cha kupiga kura N.I.T Mabibo jijini Dar es Salaam jana. Azam TV

09:17
UCHAGUZI TANZANIA: Maduka yakiwa yamefungwa eneo la Soko Kuu, Kata ya Pamba jijini Mwanza kutokana na Uchaguzi Mkuu uliofanyika jana nchi nzima. Picha na Michael Jamson



09:06
UCHAGUZI TANZANIA: Mpigakura Kandido Mnemela akiweka karatasi kwenye sanduku la kura katika Kituo cha Majengo, Mpwapwa mkoani Dodoma jana. Picha na Habel Chidawali



08:38
KIGOMA: Matokeo ya awali Kigoma Mjini: Mgombea ubunge wa ACT, Zitto Kabwe anaongoza, Urais: John Magufuli wa CCM anaongoza.

08:16
KIMARA: Wananchi vituo vya EDP Royal Kimara Stop Over A na B, Dar waanza kupiga kura leo asubuhi baada ya kuahirishwa jana kutokana na upungufu wa vifaa

07:50
UCHAGUZI 2015: Matokeo ya uchaguzi ngazi ya Rais yataanza kutangazwa kwa awamu ya kwanza saa tatu asubuhi, saa sita mchana, saa tisa na saa 12 jioni.

07:45
UCHAGUZI 2015: Wagombea urais wa vyama vya CCM na Chadema wanachuana vikali kwa mujibu wa matokeo ya awali yanayotangazwa kwenye vituo mbalimbali nchini

04:41
MATOKEO URAIS Z'BAR: Kwa mujibu wa NEC, Dk Shein (CCM) ameongoza katika jimbo la Kiembesamaki kwa kura 4,413 dhidi ya 2,986 za Maalim Seif (CUF)

02:00
MATOKEO URAIS Z'BAR: Hadi sasa ZEC imetangaza matokeo ya urais katika majimbo ya Fuoni na Kiembesamaki na Shein (CCM) anaongoza dhidi ya Maalim Seif (CUF)

01:49
MATOKEO URAIS Z’BAR: ZEC yatangaza kuwa Jimbo la Fuoni; Dk Shein (CCM) amepata kura 889 wakati Maalim Seif (CUF) akiwa na kura 429. Waliojiandikisha kupiga kura jimbo katika jimbo hilo ni 1,822, waliopiga kura ni 1,397.

Matokeo ya kura za Udiwani katika kata za Bukoba Mjini kwa mujibu wa blogu ya BukobaWadau ni kama ifuatafyo:-
  1. Kata Buhembe - CCM 
  2. Kata Mafumbo - CHADEMA 
  3. Kata Miembeni - CCM 
  4. Kata Kagondo - NCCR Mageuzi
  5. Kata Bilele - CUF
  6. Kata Nshambya - CHADEMA 
  7. Kata Bakoba - CHADEMA 
  8. Kata Rwamishenye - CCM 
  9. Kata Nyanga - CCM 
  10. Kata Kibeta - CHADEMA 
  11. Kata Kashai - CHADEMA 
  12. Kata Kitendaguro - CHADEMA
  13. Kata Hamugembe - CHADEMA 
  14. Kata Ijuganyundo - CCM

No comments: