Sunday, 25 October 2015

Wagombea uraisi wapiga kura. Tanganyika na Zanzibar



















Mheshimwia ALi Karume na Dr Salmin Amour




Mgombea kupitia tiketi ya chadema na anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA), amepiga kura, Monduli - Arusha. Katika mazungumzo yake na Azam Tv mara tu baada ya kupiga kura amesisitiza suala la amani na utulivu.

Mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli amepiga kura, Chato- mkoani Geita #kituochakochauchaguzi. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitimiza wajibu wake wa kupiga kura kwa ajili ya kuchagua Rais, Mbunge, Mwakilishi, na Diwani  kwenye kituo cha kupigia kura  namba 7 katika Shule ya Sekondari ya Kiembesamaki Zanzibar, kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaofanyika leo Octoba 25, 2015



Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiwasili katika Kituo cha Wapiga Kura cha Garagara Mtoni Zanzibar kwa ajili ya kupiga Kura leo mchana


Dk Shein apiga kura kituo cha Bungi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akitumbukiza kura katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Bungi msingi wilaya ya kati  Mkoa wa Kusini Unguja, [Picha na Ikulu.]
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akitumbukiza kura katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Bungi msingi wilaya ya kati  Mkoa wa Kusini Unguja, [Picha na Ikulu.]
 Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein akitumbukiza kura katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Bungi msingi wilaya ya kati  Mkoa wa Kusini Unguja,

No comments: