Monday, 23 December 2013

SURA MPYA ZA BARAZA LA KIKWETE

WANAOTAJWA KUINGIA
Habari zinadai kuwa katika fumuafumua inayotarajiwa kufanyika ndani ya baraza hilo, baadhi ya wabunge na manaibu waziri wanatajwa kuingia kwenye baraza hilo.
Dk. Asha-Rose Mitengeti Migiro (Mb kuteuliwa). Jee atachukua Nafasi ya Pinda 
Wanaotajwa ni Dk. Asha-Rose Mitengeti Migiro (Mb kuteuliwa) kuwa waziri, Mh. Januari Makamba (naibu waziri wa sayansi, teknolojia na elimu ya juu) kuwa waziri kamili, Mh. Amos Makalla  (Mb) kuwa waziri kamili, Mh. Mwiguru Nchemba (Mb) kuwa waziri, Mh. Peter Serukamba (Mb) kuwa waziri, Mh. Faustine Ndungulile (Mb) kuwa waziri na Mh. Jenister Joachim Mhagama (Mb) kuwa waziri.
Naibu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, Januari Makamba. < Kuchukua Nafasi ya Membe ?

Mheshimiwa Ramadhan Muombwa Kutokea Zanzibar. Kupewa Wizara ya Mambo ya Ndani ?
UTABIRI UMETIMIA
Kuondoka kwa mawaziri hao kunatimiza utabiri uliowahi kuanikwa mapema Aprili mwaka huu na mtabiri maarufu nchini, Maalim Hassan Yahya Hussein ambaye ni mrithi wa kazi za marehemu Yahya Hussein.
Mtabiri huyo aliwahi kutabiri kuwa, JK kwa mwaka huu atafanya maamuzi magumu ambayo yatashangaza wengi, hata kwa mataifa ya nje na hivyo kuandika historia.

No comments: