Saturday, 25 January 2014

RAIS KIKWETE AONGOZA WANANCHI WA MIONO KATIKA MAZIKO YA ALIYEKUWA MBUNGE WA CHALINZE,

RAIS KIKWETE AONGOZA WANANCHI WA MIONO KATIKA MAZIKO YA ALIYEKUWA MBUNGE WA CHALINZE, RAMADHAN BWANAMDOGO

 Rais Jakaya Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu Ramadhan Bwanamdogo, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Miono leo wakati wa shughuli za maziko.
 Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwaongoza waombolezaji kuswalia mwili wa marehemu Ramadhan Bwanamdogo, aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, aliyefariki juzi. Mazishi ya mbunge huyo yamefanyika leo kijijini kwao Miono.
  Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na kiuongozi wa kambi ya upinzani bungeni na Mwenyekiti wa Chadema, Mhe Freeman Mbowe (kushoto) na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, na Mbunge wa Monduli Mhe Edward Lowassa, wakati wakiwa katika maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi.
 Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwasili makaburini
 Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwaongoza waombolezaji katika mazishi ya marehemu Saidi Ramadhan Bwanamdogo,
 Sehemu ya waombolezaji
 Sehemu ya waombolezaji kinamama
 Baadhi ya waomboilezaji akiwemo Mbunge Mtarajiwa wa Chalinze Mheshimiwa Ridhwan Kikwete kuanza kuonesha nyota yake ya Siasa kwa kupitia Mgongo wa Baba .

No comments: