Thursday 30 January 2014

CUF YAWASHA MOTO KIEMBESAMAKI

KURUGENZI wa CUF – Haki za Binadamu, Habari na Uenezi, Salim Biman amesema Jimbo la Kiembe Samaki, kamwe halitarudi kwa CCM, hata wakidhikiri uchi.Pia, Bimani amesema wananchi wa Jimbo hilo wataendelea kumuunga mkono Muwakilishi wao wa zamani, Mansour Yussuf Himid kwa kumchagua Abdul Malik mgombea wa CUF, pamoja na kukabiliwa na vitisho vya CCM.Salim Bimani aliyasema hayo jana kwenye uwanja wa kwa Abdalla Rashid katika mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo.Alisema katika uchaguzi huo Wazanzibari wote wataendelea kumuunga mkono Mansour, licha ya kwamba watakabiliana na vitisho vya CCM:“Wazanzibari wote tutaendelea kumuunga mkono Mansour Yussuf Himid…Tutaendelea kupiga kampeni nyumba kwa nyumba licha ya kuwa CCM hawataki na wanataka wahamasishaji wetu wakamatwe,” alisema na kuongeza


MKURUGENZI wa CUF – Haki za Binadamu, Habari na Uenezi, Salim Biman amesema Jimbo la Kiembe Samaki, kamwe halitarudi kwa CCM, hata wakidhikiri uchi.Pia, Bimani amesema wananchi wa Jimbo hilo wataendelea kumuunga mkono Muwakilishi wao wa zamani, Mansour Yussuf Himid kwa kumchagua Abdul Malik mgombea wa CUF, pamoja na kukabiliwa na vitisho vya CCM.Salim Bimani aliyasema hayo jana kwenye uwanja wa kwa Abdalla Rashid katika mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo.Alisema katika uchaguzi huo Wazanzibari wote wataendelea kumuunga mkono Mansour, licha ya kwamba watakabiliana na vitisho vya CCM:“Wazanzibari wote tutaendelea kumuunga mkono Mansour Yussuf Himid…Tutaendelea kupiga kampeni nyumba kwa nyumba licha ya kuwa CCM hawataki na wanataka wahamasishaji wetu wakamatwe,” alisema na kuongeza:
“Kwanini tusifanye kampeni…kwanini tusishinde wakati nia yetu ni kuwatetea Wazanzibari. Nitashangaa Kiembe Samaki akishinda Mahmoud asiyeitakia mema Zanzibar,” alisema Bimani.Alisema CCM wameanza kuchanganyikiwa wanapoona msisimko wa watu katika mikutano ya kampeni za CUF: “Eti tunaotaka Mamlaka Kamili tusubiri ‘PEPONI’ sisi tunawambia hatusubiri ‘PEPONI’ ni hapa hapa Zanzibar,” alisema Bimani.Alisema anawashangaa CCM na kauli zao zilizokosa mashiko:”Nashangaa na kauli zao wanzozitoa…wanasema tayari tuna Mamlaka Yetu…wakati hatuwezi kuamua lolote ndani ya nchi yetu,” alisema Bimani.
Mkurugenzi huyo wa CUF alisema Wazanzibari waliyowengi wanaomba hata leo kupewa fursa ya kuamua mustakabali wa nchi yao:“Wazanzibari waliyowengi wanataka leo hii waletewe kura ya maoni waamue mustakabali wa nchi yao,” alisema Bimani.Bimani, aliwasihi vijana wa Kiembe Samaki, kutokufanya kosa kwa vitisho vya CCM na wahakikishe wanamchagua mgombea kupitia CUF, ili kuendeleza madai ya Zanzibar, yaliyoanzishwa na Mansour. Alisema kufanya hivyo, itakuwa ni kumuunga mkono na kumuheshimu, Mansour:“Wakaazi wote wa Kiembe Samaki wanaomuheshimu na kumuenzi Mansour…basi wampe kura Abdul Malik, ili akaendeleze alioyadai Mansour,” alisema Bimani.
Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembe Samaki, Unguja utafanyika Jumapili mwishoni mwa wiki hii. Mvutano mkali upo kwa mgombea wa CCM, Mahmoud Thabit Kombo na Abdul Malik wa CUF.Siku za karibuni Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba ‘wanaotaka mamlaka kamili ya Zanzibar, wahame’.Kauli hii ndani na nje ya Zanzibar, imetafsiriwa kuwa ni kauli ya woga, kiongozi dhaifu, asiye na dira na aliyekosa busara za kusoma wakati na mawazo ya anaowaongoza.Anaelezwa ni kiongozo wa kwanza Zanzibar, kuwashambulia raia wake kwa maneno ya kejeli na dharau. Dk Shein, hana hati miliki ya Zanzibar, huku hata uchaguzi mkuu uliyopita, hakupiga kura.Hata hivyo, kwa mujibu wa Rasimu ya Pili ya Mabadiliko ya Katiba, asilimia zaidi ya 60 walipendekeza muundo wa Muungano wa mkataba na asilimia 34 ndiyo waliyopendekeza serikali mbili..

No comments: