Tuesday, 28 January 2014

WAHAFIDHINA WA CCM WACHANGANYIKIWA ZANZIBAR

Kamati ya Warioba yawatoa machozi wahafidhina wa Zanzibar baada ya asilimia 61 %ya Wazanzibari kukataa sera za CCM ambacho kinabaki madarakani kimabavu hakina tena uwezo wa kuwatawala kwa mabavu isipokua Nguuvu ya Tanganyika ndio inawafanya wabaki Kuiba kura na kubaki madarakani kwa kulazimisha bila ya ridhaa ya Wazanziibari.
 Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. AliMohamed Shein, akimtambulisha Mgombea wa CCM wa Jimbola Kiembesamaki wakati wa uzinduzi wa sherehe za miaka 37 ya CCM,Kiataifa yamefanyika katika viwanja vya Mpira Kiembesamaki Zanzibar.  
 Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wanachama wa Chama cha Mapinduzi katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa sherehe za kuzaliwa kwa CCM na kutimia miaka 37, uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya mpira kiembesamaki.
 Mgombea wa CCM Jimbo la Kiembesamaki katika uchaguzi mdogo,Ndg Mahmoud Thabit Kombo Jecha, akiwasalimia WanaCCM, wakati wa mkutano wa Uzinduzi wa sherehe za CCM kutimia miaka 37, katika viwanja vya Kiembesamaki.

Katibu Mkuu wa CCM  Mhe. Ibrahim Kinana, akihutubia katika mkutano huo wa uzinduzi wa sherehe za CCM kutimia miaka 37 , uliofanyika katika viwanja vya Kiembesamaki Zanzibar. 

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe. Vuai Ali Vuai, akizungumza katika mkutano huo wa Uzinduzi wa sherehe za CCM.



  Viongozi wa CCM wakimsikiliza Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika mkutano wa Uzinduzi wa sherehe za miaka 37 ya CCM tangu kuzaliwa kwake katika viwanja vya Amaan. 
 Wanachama wa CCM wakifuatilia uzinduzi huo ulioambatana na kumjulisha Mgombea wa CCM wa Jimbo la Kiembesamaki katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao tarehe 2, Febuari
 Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakimsikiliza Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa uzinduzi wa sherehe za kuzaliwa CCM kutimia miaka 37. 
 Vijana wa UVCCM wakiwa na picha  za Viongozi wakati wa kuimba wimbo maalum na kuzionesha juu. 
 Vijana wa UVCCM wakiimba wimbo maalum wa kuunganisha Vyama wakati wa Uzinduzi wa sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja vya mpira kiembesamaki Wilaya ya Magharibi Unguja.
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa Uzinduzi wa sherehe za miaka 37 ya CCM kuzaliwa kwake baada ya kuunganisha Vyama vya ASP na TAviwanja vya uwanja wa Amaan Zanzibar.

No comments: