Sunday 9 February 2014

MTOTO WA ALIEKUWA WAZIRI WA FEDHA DR MGIMWA ASHINDA KURA YA MAONI

w741 37218
Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa Marehemu Dkt William Mgimwa, akiongea kwa niaba ya familia wakati wa mazishi kijijini Magunga jimbo la Kalenga mkoani Iringa
Matokeo ya kura za maoni ndani ya CCM yametangazwa usiku wa kuamkia leo mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Godfrey Mgimwa akishinda kwa kishindo katika nafasi hiyo huku Jackson Kiswaga akifuatia katika matokeo hayo.
Mtoto wa Mgimwa amepata kushinda kwa kura 342 huku Kiswaga akipata kura 170 na mkuu wa wilya ya Pangani Hafsa Mtasiwa akiambulia kura 42 .
Matokeo hayo yametangazwa katika ukumbi wa shule ya sekondari Mwembetogwa Manispaa ya Iringa huku mgombea Peter Mtisi akipata kura 33 ,Msafiri Pangagira kura 8,Bryson Kibasa kura 7,Edward Mtakimwa kura 3 na Thomas Mwiluka akiambulia kura 2. Chanzo: Francis Godwin

No comments: