Monday, 17 February 2014

VITUKO VYA CCM DODOMA

Nape akwahutubia wandishi kuwaambia kuwa CCM sera yake ni serkali mdili zilizoboreshwa !


Wimbo huu wa CCM si kejeli kwa Warioba na tume yake?.Rais kikwete amewasili uwanja wa ndege wa Dodoma jioni na kupokelewa kwa shamra shamra za aina yake ikiwemo band na ngoma zilizoandaliwa na vijana waliokuwa wamevaa sare za chama cha mapinduzi.Miongoni mwa watu waliokuwepo uwanjani kumpokea Kikwete ni pamoja na katibu mkuu wa CCM,bwana Kinana,katibu wa uenezi wa CCM,bwana Nape Nnauye na viongozi wengine wa chama hicho.

Hata hivyo,kilichonishitua ni wimbo wa mapokezi uliondaliwa mahususi kumpokea JK hapa air port wenye maneno yafuatayo;CCM hatuko tayari kukubali serikali 3,katika wimbo huo pia wanakejeli eti kama wake wawili wamekushinda(yaani serikali mbili), je, ukiongeza mke wa tatu(yaani kuwa na serikali 3) utaweza?,pia kuna maneno kama tunaapa kutetea serikali mbili,kuna nchi gani duniani ina maraisi wa tatu n.k Sasa swali,hivi katiba ya nchi inaamuliwa na chama siasa au ni maamuzi ya wananchi wenyewe?!Wakuu,kwa mwendo huu,katiba mpya ni ndoto au CCM inajichimbia Kaburi kukataa maoni ya watanzania walio wengi 

No comments: