Monday 10 March 2014

CHALINZE KUWASHWA MOTO ,RIDHWANI KIKWETE KUPINGWA NA VYAMA VITATU

ALIYEKUWA MSHINDANI WA RAIS JAKAYA KIKWETE KATIKA UCHAGUZI WA JIMBO LA CHALINZE MWAKA 2000 KWA TIKETI YA CHAMA CHA WANANCHI (CUF), FABIAN LEONARD ATAPAMBANA NA MTOTO WA RAIS HUYO, RIDHIWANI KIKWETE KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO HILO UTAKAOFANYIKA APRILI 6, MWAKA HUU.

 MWENYEKITI WA CHAMA CHA CUF IBRAHIM RIPUMBA

Aliyekuwa mshindani wa Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi wa Jimbo la Chalinze mwaka 2000 kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (Cuf), Fabian Leonard atapambana na mtoto wa rais huyo, Ridhiwani Kikwete katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo utakaofanyika Aprili 6, mwaka huu
Chama hicho, kikimtangaza mgombea huyo Makao Makuu ya Cuf yaliyopo Buguruni Dar es Salaam jana, kilisema kinakwenda kulichukua jimbo hilo kutokana na wananchi wake kuendelea kuishi maisha magumu wakati rais wa nchi anatokea jimbo hilo.
Uchaguzi huo unafanyika kujaza nafasi iliyobaki wazi baada ya aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo, Said Bwanamdogo kufariki dunia. Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Abdul Kambaya akimtambulisha mgombea huyo alisema, Leonard alipambana na Rais Kikwete mwaka 2000 wakati huo Rais Kikwete akiwa Waziri wa Mambo ya Nje.
“Huyu Leonard ni mzaliwa wa Chalinze anayajua matatizo ya wanachalinze, alipambana na Rais Kikwete lakini kutokana na sababu mbalimbali alishindwa, sasa ni zamu yake kumpambana na mwana,”alisema Kambaya
Leonard alisema, jimbo hilo limekuwa nyuma kimaendeleo huku likiwa na kiongozi wa nchi ndani yake, hivyo endapo baba alishindwa hata mtoto naye hataweza. 

Alisema Mkoa wa Pwani katika matokeo ya kidato cha Nne mwaka jana imekuwa ya tatu kutoka mwisho, huduma za afya duni na barabara hazifai. “Nimejipanga, nilipambana na baba yake sasa kama napambana na mtoto ni dhahiri ushindi upo hadharani”alisema Leonard.

No comments: