Tuesday 11 March 2014

LINI CCM ITAJIFUNZA AU KUJIKWAA SIO KUANGUKA !



*****************************************************************

MAISHA NA NYAKATI ZA ABOUD JUMBE MWINYI  SEHEMU YA KWANZA MIAKA 30 YA DHORUBA .
MIAKA 30 iliyopita, Januari 1984, Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), iliyoketi mjini Dodoma kwa dharura, ilimvua (ilimpindua?) nafasi zote za uongozi, Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar, Alhaj Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi kwa kutenda ‘dhambi kuu’ ya kuhoji muundo wa sasa wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Nyadhifa alizovuliwa kiongozi huyo na kubakia kuwa raia wa kawaida na kuwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani kwake kwa kipindi kadhaa, ni pamoja na urais wa Zanzibar, uenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, umakamu wa Rais wa Tanzania na umakamu Mwenyekiti wa CCM Taifa.









Mkutano huo ulitawaliwa na kampeni chafu dhidi ya Jumbe, huku kambi mbili za Zanzibar zikiumana, kwa kambi moja kuunda tuhuma dhidi yake na nyingine kujibu mapigo, na hivyo kuchonga ufa na uhasama mkubwa miongoni mwa viongozi wa Zanzibar kati ya kambi mbili hizo kinzani; kambi iliyojiita ya ‘Wakombozi’ (Liberators), iliyoundwa na waliojiona kama watetezi halisi wa Mapinduzi ya 1964 na ile ya kambi ya ‘Wanamstari wa mbele’ (Front liners), iliyotaka mabadiliko ya sera visiwani. Jumbe alikuwa mrithi wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, aliyeuawa hapo Aprili 7, 1972. Kabla ya hapo, Jumbe alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, akishughulikia mambo ya Muungano.

 uandike kwa ufupi Historia ya Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, Ukurasa umeonelea utimize ombi hilo kwa kueleza kwa ufupi juu ya Maisha na Nyakati za Nguli huyu wa siasa za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hivyo basi, Mtiririko huu ni Ufunguo juu ya Masimulizi ya Waandishi mbalimbali wa Ukurasa huu juu ya Maisha ya Mzee Jumbe na dhoruba alizokumbana nazo takriban miaka 30 sasa tangu akae nje ya mfumo rasmi wa siasa za Tanzania. 


Mzee Aboud Jumbe alitufungulia njia kutuuundia Katiba Wazanzibari baada ya Kuongozwa Kijeshi kwa miaka nenda na kuekwa Kwenye Mahakama za Kangaroo na Maelfu ya Wazanziabri kuikimbia nchi yao bila kupenda na kuenda kuwa Wakimbizi kila kona ya Dunia Leo hatutorudi nyuma kupigania Haki za Zanzibar.

**************************************************************

No comments: