Maalim Seif:Wananchi jiandaeni kuipa CUF ushindi mkubwa 2015
Wananchi wa Zanzibar wametakiwa kujiandaa kikamilifu ili kushiriki katika uchaguzi mkuu unaofuata wa mwaka 2015 na hatimae kukipa chama cha Wananchi CUF ushindi mkubwa.
Kauli hio imetolewa na Katibu mkuu wa Chama hicho ambae pia ni Makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad wakati alipokuwa akizungumza na wana Barza ya Coman welth iliopo michenzani Mkoa wa mjini magharib Unguja.Aliwataka wananchi hao kujua kuwa siri ya ushindi katika uchaguzi ni kuwa na wapiga kura wengi pamoja na kulinda kura zao, hivo ni wajibu wa wananchi kuhakikisha kila mmoja anapata haki ya kupiga kura ifikapo mwaka 2015 ili kuiondoa CCM madarakani.
Alieza kuwa ana jua kwa makusudi masheha wa shehi mbali mbali wamekuwa wakiagizwa kwa makusudi kutokutoa baruza za vitambulisho kwa lengo la kupunguza idadi ya kura za CUF lakini amewanasihi wananchi hao kutokuvunjika moyo na waendelee kufatilia mpaka pale watakapoipata haki yao.‘’Ni lazima tuhangaike ili kupata vitambulisho hivi ikiwa tunataka kuiondoa CCM na hatimae kila mtu apewe haki yake stahiki kwa mujibu wa katiba’’alieleza Hamad.
Akizungumzia suala la ajira kwa
vijana wa Zanzibar Maalim Seif amesikitishwa na uwepo wa ubaguzi wa hali ya juu katika suala ala ajira ambapo wamekuwa wakiajiriwa watu kwa kubaguliwa ndani ya Zanzibar.‘’Ni wajibu wetu kupambana kuhakikisha tunaiondoa CCM ili kila mwenye haki yake Apewe’’aliendelea kueleza.Akizungumzia kuhusu suala la Katiba mpya Hamad alieleza kwamba rasimu ya tatu ya katiba mpya imelazimishwa pamoja na kuwekwa kando maoni ya wananchi yaliokushanywa kwa ufanisi mkubwa na Tume ya Jaji Warioba.
Aliwataka Wazanzibar kushikamana iwapo CCM wataitisha kupigiwa kura juu ya katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu basi kwa umoja wao waikatae katiba hio kwani ina lengo la kuizika kabisa anzibar.Aidha Maalim Seif aliendelea kwa kufafanua kwamba katiba ni suala la maridhiano ya wananchi wenyewe pamoja na kuzingatiwa kwa maoni yao hivo katiba isiokuwa na ridhaa ya wananchi wenyewe haiwezi kukubalika.
Pamoja na hayo aliwanasihi wazanzibar kutokukubali rasilimali zao ikiwemo mafuta kuchukuliwa na wengine wasiokuwa wazanzibar.Wakitoa shukrani zao wajumbe wa Barza hio walimshukuru Maalim Seif kwa kuwa mlezi wa barza hio pamoja na kukubali wito wao.Pia wamemuhakikisha kuyafanyia kazi yale yote aliyowaagiza ikiwemo kuhakikisha kwamba kila mmoja anapata haki ya kupiga kura kwa ajili ya kukipa ushindi mkubwa chama hicho ifikapo mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment