Saturday, 11 October 2014

SURA YA SITA URAIA KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO KWENYE KATIBA YA VIJISENTI

SURA YA SITA YA KATIBA YA VITISENTI AKA ANDREW CHENGE
Uraia wa Jamhuri ya Muungano
68.-(1) Mtu ambaye, kabla ya Katiba hii kuanza kutumika, ni raia wa  Jamhuri ya Muungano ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano. (2) Uraia wa Jamhuri ya Muungano ni wa aina mbili na utapatikana kwa njia ya kuzaliwa au kuandikishwa. Haki ya uraia 69. Kila raia ana haki ya kutambuliwa uraia wake na kwa madhumuni haya, mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria
utakaowezesha raia kupata hati ya kuzaliwa, kitambulisho cha uraia wake bila ya upendeleo na ubaguzi wa aina yoyote, na pale inapohitajika, nyaraka za kumwezesha kusafiri.
Uraia wa kuzaliwa 70.-(1) Kila mtu aliyezaliwa Tanzania Bara au Zanzibar atakuwa raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano iwapo, wakati wa kuzaliwa, mama au baba yake ni, au alikuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.(2) Kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, mtu aliyezaliwa nje ya
Tanzania atakuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa kuanzia tarehe ya kuzaliwa kwake ikiwa mama au baba yake ni raia wa Jamhuri ya Muungano.
(3) Endapo mmoja kati ya wazazi wake alifariki kabla ya mtu huyo kuzaliwa, uraia wa mzazi huyo wakati wa kifo chake utatumika kwa madhumuni ya kutambua uraia wa mtu huyo aliyezaliwa baada ya mzazi aliyefariki kana kwamba mzazi huyo alikuwa anaishi hadi kuzaliwa kwa mtu
huyo.
(4) Mtoto mwenye umri chini ya miaka saba akikutwa ndani ya eneo la Jamhuri ya Muungano katika mazingira ambayo wazazi wake hawajulikani, atachukuliwa kuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa.
(5) Endapo uraia wa wazazi wa mtoto aliyepewa uraia chini ya masharti ya ibara ndogo ya (4) utabainika kuwa si uraia wa Jamhuri ya Muungano, uraia wa mtoto huyo utasita.
(6) Bila kuathiri masharti ya Ibara hii, Bunge litatunga sheria ambayo itaweka masharti na utaratibu wake:

SURA YA SABA

MUUNDO WA JAMHURI YA MUUNGANO
Muundo wa Muungano
73. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na muundo wa Serikali
mbili ambazo ni:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano; na
(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi
74.-(1) Shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katika Jamhuri ya Muungano   zitatekelezwa na udhibitiwa na vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji,  vyombo viwili vyenye mamlaka ya utoaji haki, na pia vyombo viwili vyenye  mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma.25
(2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni Serikali ya  Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; vyombo vyenye  mamlaka ya utoaji haki vitakuwa ni Mahakama ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama Kuu ya Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni Bunge na Baraza la Wawakilishi. (3) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za umma katika Jamhuri ya Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa katika Ibara hii, kutakuwa na Mambo ya Muungano kama yalivyoorodheshwa katika Nyongeza ya Kwanza ya Katiba hii na pia kutakuwa na mambo yasiyo ya Muungano, ambayo ni mambo mengine yote yasiyo ya Muungano.
(4) Kila chombo kilichotajwa katika Ibara hii kitaundwa na kutekeleza
majukumu yake kwa kufuata masharti mengine yaliyomo katika Katiba hii.
Mamlaka ya  Serikali ya Jamhuri ya Muungano
75. Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na mamlaka ya utekelezaji
katika Jamhuri ya Muungano kwa Mambo ya Muungano na kwa mambo yote
yasiyo ya Muungano yanayohusu Tanzania Bara.
Mamlaka ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mambo yasiyo ya
Muungano
76.-(1) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka na haki
juu ya mambo yasiyo ya Muungano yanayohusu Zanzibar.
(2) Bila kuathiri mipaka iliyowekwa na Katiba hii, katika kutekeleza
mamlaka yake chini ya ibara ndogo ya (1), Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
itakuwa na uwezo na uhuru wa kuanzisha uhusiano au ushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa.
(3) Endapo, katika kutekeleza mamlaka na majukumu yake kwa mujibu
wa Ibara hii, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahitaji kupata ushirikiano kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kufanikisha uhusiano au
ushirikiano na jumuiya au taasisi ya kikanda au kimataifa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza kufanikisha uhusiano au ushirikiano huo kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na sheria itakayotungwa na Bunge.
(4) Kwa madhumuni ya Ibara hii, Bunge litatunga sheria itakayoainisha
na kufafanua:
(a) majukumu na mipaka ya utekelezaji wa mamlaka ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu
uhusiano au ushirikiano wa kikanda au kimataifa;
(b) utaratibu wa kushughulikia athari zinazotokana na uhusiano au
ushirikiano wa kikanda au kimataifa;
(c) utaratibu wa utafutaji na upatikanaji wa mikopo na misaada
kutokana na uhusiano au ushirikano huo;
(d) utaratibu au masharti ya kuvunja au kuimarisha uhusiano au
ushirikiano huo;
(e) utaratibu wa mawasiliano na mashauriano kati ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu
uhusiano au ushirikiano wa kikanda au kimataifa;
(f) utaratibu wa utekelezaji wa masharti ya Ibara hii; na 26
(g) mambo mengine yatakayohusu uhusiano au ushirikiano wa kikanda
au kimataifa chini ya Ibara hii.
Mahusiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya
Mapinduzi ya
Zanzibar
77.-(1) Katika kutekeleza majukumu yake katika maeneo mbalimbali,
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itazingatia misingi ya
kushirikiana na kushauriana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa lengo la
kukuza na kulinda maslahi ya Taifa na maendeleo ya wananchi.
(2) Kwa madhumuni ya kukuza umoja na uhusiano, Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, zinaweza
kushauriana na kushirikiana katika mambo yanayohusu uongozi, utawala,
vyombo vya uwakilishi na mahakama.
(3) Utendaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar au chombo chochote cha Serikali hizo utatekelezwa kwa kuzingatia
umoja wa Jamhuri ya Muungano na wajibu wa kukuza utaifa.
(4) Bila kuathiri masharti ya Ibara hii, Serikali ya Jamhuri ya Muungano,
kwa makubaliano maalum baina yake na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
inaweza kutekeleza jambo lolote lililo chini ya mamlaka ya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa mujibu wa makubaliano hayo.
Wajibu wa
viongozi wakuu
kulinda Muungano
78.-(1) Bila kuathiri wajibu wa kila raia uliotajwa katika Katiba hii, kila
kiongozi mkuu mwenye mamlaka ya utendaji katika Jamhuri ya Muungano
aliyetajwa katika ibara ndogo ya (3) atakuwa na wajibu, katika kutekeleza
madaraka aliyopewa kwa mujibu wa Katiba hii, kuhakikisha kuwa anatetea,
analinda, anaimarisha na kudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
(2) Kwa madhumuni ya masharti ya ibara ndogo ya (1) kila kiongozi
mkuu aliyetajwa katika ibara ndogo ya (3), kabla ya kushika madaraka yake,
ataapa kuutetea, kuulinda na kuudumisha Muungano kwa mujibu wa Katiba hii.
(3) Viongozi wakuu wanaohusika na masharti ya Ibara hii ni:
(a) Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(b) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(c) Rais wa Zanzibar;
(d) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano; na
(e) Makamu wa Rais wa Zanzibar.

No comments: