Ndugu wanahabari, Kama mjuavyo leo ni siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji katika taifa letu. Chama chetu cha ACT-Tanzania kimeshiriki uchaguzi huo ukiwa ndio uchaguzi wetu wa kwanza kushiriki tangu chama kipate usajili wa kudumu hapo Mei 5, 2014. Chama kimesimamisha wagombea wapatao 2,202 nchi nzima katika mikoa karibu yote ya Tanzania bara ambayo ndiyo inayoshiriki uchaguzi huo. Wakati zoezi hilo likiendelea wakati huu, kama chama tunapenda kusema yafuatayo kuhusiana na uchaguzi huu:
1. Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa watanzania kwa kutupokea na kutukubali na hata kutuwezesha kupata wagombea 2,202. Si jambo la kawaida kwa kwa chama kilichosajiliwa miezi 7 iliyopita kupata idadi hiyo ya wagombea. Miongoni mwa wagombea hao 2,202 tayari chama chetu kimeshapata ushindi kwa mgombea mmoja aliyepita bila kupingwa. Nafurahi kumtangaza Mwenyekiti wa kwanza wa Serikali ya Kitongoji kupitia ACT-Tanzania ambaye ni ndugu Ndugu Justin Kahonga Mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji cha Songambele , Kijiji cha Masigo katika Kata ya Ilela wilayani Mlele Mkoa wa Katavi.

No comments:
Post a Comment