Wednesday 17 December 2014

PINDA KWAHERI YA KUONANA KAZI IMEKUSHINDA !

Tofauti na wengi wanavyodhani, mzee wangu Pinda ulishaonyesha dalili za wazi ikiwa kweli unamudu vyema nafasi ya uwaziri mkuu. Kuna mengi tu yaliyofanya baadhi yetu tutilie shaka umahiri wako lakini hii skandali ya Tegeta/escrow imefunga mjadala!

Unakumbuka uliposema na wapigwe tu? Liwalo na liwe!
Wakumbuka ile kauli ya tumechoka?
Wakumbuka mgomo wa madaktari?
Je wakumbuka kauli yenye utata “anayeua albino na yeye auwawe”?
Lakini wajua namna “mchwa” katika baadhi ya halmashauri wanavyotafuna fedha za wananchi?

Tegeta/Escrowni hitimisho la yote haya, mzee wangu Pinda mtoto wa kulima, let it go! Jiuzulu, mpe fursa rais Kikwete aunde baraza jipya la mawaziri, urais unaweza kutafutwa hata nje ya uwaziri mkuu!

Ukiwa mwanasheria utanielewa vizuri naposema hoja si ikiwa unahusika au la! Hili si muhimu sana, hoja hapa ni dhamana ya uongozi kusimamia shughuli za serikali ilishindwa kutumika kunusuru “skandali”hii.

Kiongozi waumma “kutuhumiwa” si jambo jema, tuhuma pekee zinatosha kukufanya ubwage manyanga “resigning does not mean you are weak, but sometimes it means you are strong enough to let it go”

Achia ofisi ya umma kwa manufaa ya walala hoi wa Tanzania, kiongozi wa umma umetuhumiwa kutosimama kidete kuzuia uozo huu kabla, kauli za “kila mtu atabeba msalaba wake” si za kulisaidia taifa, ni kauli inayoashiria hamu ya mtawala asiyependa kuwajibika, anayetaka kung’ang’ania madaraka! Haifai kabisa, busara inakutaka kuwajibika kama mtangulizi wako Edward Ngoyai Lowassa, kumbuka “Caesar’s wife must be above suspicion’’
 President Jakaya Kikwete risks ending his presidency on a bad note if he will not sack Prime Minister Mizengo Pinda and the minister for Local Government, Ms Hawa Ghasia, for failing to properly oversee local government elections, the Civic United Front (CUF) chairman Prof Ibrahim Lipumba said yesterday.
CUF also wants the Head of State to punish all city council directors who were given funds to coordinate and administer the process in their respective areas but failed to do so.
But on Monday, Ms Ghasia while admitting that the exercise was marred in at least 14 regions, defended her office from blame and said individual council officers will shoulder the burden of the bangled elections. The minister ordered for an investigation into the shortcomings.
Prof Lipumba told reporters yesterday duringf a press conference in Dar es Salaam that the elections were marred by serious irregularities due to the fact that the prime minister’s office openly showed that it was not ready to oversee the exercise.
His appeal was similar to those made by Chadema on Monday to pile pressure on government after the elections were bungled up in many areas due to poor management and serious ommissions now being blamed on partisan politics.

No comments: