Wednesday 19 August 2015

Aliyekuwa Mbunge wa viti maalum CCM Lindi ajiunga na CUF


Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akimpokea Mbunge wa CCM, Riziki Rurida aliyekihama chama hicho na kujiunga na CUF. Kulia ni Mbunge wa Lindi Mjini, Salum Barwan.


Na Khamis Haji OMKR

Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi kutoka mkoa wa Lindi, Riziki Said Rurida amekihama chama hicho na kuhamia Chama cha Wananchi CUF.

Rurida alitangaza kukihama chama hicho na kukabidhiwa kadi ya CUF na Katibu Mkuu wa chama hicho, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad katika mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika jana Mchinga, Lindi vijijini.

Katika mkutano huo ambapo pia wanachama 650 wa CCM walitangaza kukihama chama hicho ns kujiunga na CUF, Mbunge huyo ambaye ametumikiwa wadhifa huo kwa vipindi viwili alisema kuwa anajisikia mwenye furaha kubwa baada ya kukabidhiwa kadi na kuwa mwanachama wa CUF.

Mbunge huyo alikuwa ni miongoni mwa wanachama wa CCM waliowania nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo na kuangushwa na Mbunge wa sasa, Said Mtanda baada ya kushika nafasi ya pili, ambapo alilalamika kuwa uchaguzi huo ulitawaliwa na mizengwe.

Akikaribisha katika chama cha CUF, Maalim Seif alisema wimbi la mabadiliko nchini Tanzania linaloongozwa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa ni kubwa na atakaye jaribu kulizuia ajiandae kupasuka kifua.  

“Hili wimbi ni kubwa mnasikia vigogo wa CCM wanaendelea kuporomoka na kujiunga na wapinzani, atakaye jaribu kupingana na wimbi hili atapasuka kifua”, alisema Katibu Mkuu wa CUF ambaye piia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.   

Alisema CUF pamoja na vyama vyengne vinavyounda Ukawa vitaendelea kuwapokea viongozi na wanachama wanaojiunga na vya mna hivyo kutoka CCM na mara wanapokuwa wanachama wa vyama hivyo wanakuwa na haki sawa na wanachama waliojiunga muda mrefu uliopita.

Maalim Seif alikemea tabia ya baadhi ya viongozi na askari Polisi kuwazuia wananchi wasitumie haki yao ya kidemokrasia ikiwemo kufanya maandamano na kuwahimiza wafuate sheria na wajieopushe na uvunjifu wa haki za binaadamu.

“Polisi nchini kote fuateni sheria, hamtakiwi kuingia kwenye siasa, lakini kama kuna kiongozi wa Jeshi anajiona ni CCM kuliko hao CCM wenyewe, basi avue magwanda aje tupambane kwenye majukaa ya siasa”, alionya Maalim Seif.

Katika mkutano huo, Mbunge wa Lindi Mjini Salum Barwan alisema wananchi wa mikoa ya Kuisni mwa Tanzania wana kila sababu ya kukikimbia chama cha Mapinduzi kutokana na Sera zake mbovu ambazo hazijawasaidia wala kuwapa matumaini yoyote wananchi katika mikoa hiyo.

Alisema kutokana na hali ya umasikini iliyosababishwa na utawala wa CCM kwa muda wa miaka 50, alisema wananchi wa mikoa ya Kuisni wanaingia katika uchaguzi mkuu wakiwa na ajenda yao ambayo ni Mgawanyo rasmi wa rasilimali zilizomo katika eneo hilo.

Barwan alisema mikoa hiyo inazo rasilimiali za kutosha lakini wananchi wake wameendeleaa kuwa masikini wa kjutupwa na ukweli CCM haina sera thabiti za kusaisdia wananchi wa mikoa hiyo

No comments: