Sunday, 27 September 2015

Lowasa kupunguza kero cha huduma za jamii

Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEM anayewakilisha UKAWA Edward Lowassa amesema akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano atahakikisha kuwa serikali yake inaanzisha kituo maalum cha jamii 'one stop centre' kitakachokuwa kikitoa huduma kwa umma sehemu moja ili kupunguza urasimu katika kupata huduma hizo.

Lowassa akiwa katika mkoa wa 20 wa mikutano ya kampeni ya kuomba ridhaa ya watanzania kumchagua kuwa rais wa awamu ya tano leo akitumia njia ya barabara katika azma yake ya kuwafikia wananchi wote hata wa vijijini, alifanya mikutano mitano -- Kata za Rundugai, Shirimatunda, Machame Mkwakwasi, Masama Mula na baadaye kuzindua kampeni katika mkutano uliofanyika Boma Mjini. -- katika Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro ikiwa na lengo la kuzindua kampeni za mgombea ubunge wa jimbo hilo Freeman Mbowe. [taarifa via ChannelTEN]


Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokelewa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakati alipowasili eneo la Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira wa Machame, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.


Picha zote tumeshirikishwa na Othman Michuzi/Michuzi Jr2/Mtaa kwa Mtaa blog.


Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira wa Machame, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, Mh. James Mbatia akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwa amembeba Mtoto Sayuni Nassary, mara baada ya Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015. Kushoto ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakiwapungia wananchi wa mji wa Bomang'ombe, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015.

No comments: