Zanzibar: Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF),Maalim Seif Sharif Hamad, amesema chini ya uongozi wake atahakikisha anamjengea uwezo mkulima, kwa lengo la kumwezesha kuinuka kiuchumi.Maalim Seif alisema, atahakikisha wakulima wa Zanzibar wanalima kilimo cha kisasa cha umwagiliaji, ili kuzalisha kwa wingi kwa ajili ya biashara.Alisema, kilimo ambacho kinahitaji mkakati wa makusudi kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama chake ni zao la mpunga, kwani wali ndio chakula kikuu cha Zanzibar, ili pia kupunguza gharama ya fedha za kuagiza mchele kutoka nje.Maalim Seif aliyasema hayo katika mkutano wa kampeni za majimbo kupitia Chama hicho, uliofanyika katika Kiwanja cha Polisi Konde, Wilaya ya Micheweni,Mkoa wa Kaskazini Pemba.Alisema, imekuwa jambo la kawaida kwa mkulima hasa wa Zanzibar kuonekana mtu wa mwisho katika jamii, hivyo serikali yake itamuangalia kama wafanyakazi wengine.“Kwa asilimia 90 chakula tunachokula kinatoka mikononi mwa mkulima, lakini cha kushangaza hadi sasa serikali iliyopo madarakani haijamuona mkulima huyo anayeendelea kudhoofika”, alisema Maalim Seif.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment