Tuesday, 29 September 2015

Nani ataiongoza Tanzania







(CCM) kushinda uchaguzi mkuu ujao ni lazima kwa vyovyote vile, kulingana na kauli ya afisa mwandamizi wa chama hicho. UKAWA nayo yasema iko tayari kupambana na chama tawala.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara hivi karibuni juu ya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, afisa huyo alitamka kuwa chama kiko tayari kushinda hata ikibidi kufunga goli kwa mkono.
Tamko lake liliwashtua wasikilizaji lakini vyama vya upinzani vikalichukua kama kauli mbiu ya CCM kwa uchaguzi. Watu wengine wakaliona tamko la afisa huyo kama halifai katika uongozi ingawa lililenga kuhamasisha kampeni za uchaguzi mkuu. “Wamekuwa wakifanya hivyo daima,” alisema rafiki yangu ambaye hana ushabiki wa kisiasa, lakini nilipomtaka afafanue kauli yake, alisema CCM inataka kudumisha uhai wake uzeeni na kwamba “sasa ambapo uchaguzi unakaribia, ipo haja kupima upya maadili na dhana zake kama chama.”

Tanzania imebadilika
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na mgombea wa urais wa CCM, John Magufuli Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete na mgombea wa urais wa CCM, John Magufuli
Wakati huu Tanzania ni nchi tofauti na wakati CCM ilipozaliwa. Ina kizazi kipya cha vyama vya siasa na viongozi. Kila chama kinatengeneza vyombo vyake vya kukifikisha kwenye malengo yake kupitia uchaguzi wa kura.
Uchaguzi ujao utakuwa na idadi kubwa ambayo haijapata kutokea ya wapiga kura nchini, yaani zaidi ya milioni 24, na wote wana nia ya kupiga kura kupitia vyama hivyo. Kila chama kinafanya linalowezekana kuvutia wanachama wapya, lakini itategemea maono ya ubunifu na watu wenye bidii kufanikisha malengo yao. Katika miaka yake ya mwanzo kama chama pekee nchini, CCM ilikua kutegemea maono na ari ya viongozi wake waanzilishi. Kiliwavutia wanachama wapya lakini siyo watu wote. Kilikumbwa na maumivu ya ukuaji na kikafanikiwa kupita hali ya utu uzima huku kikikamilisha malengo yake kwa ufahari mkubwa.
CCM tayari kupambana na UKAWA


Edward Lowassa atapeperusha bendera ya UKAWA katika uchaguzi mkuu
Hapana shaka kuwa chama hiki kimegusa maisha ya Watanzania pamoja na siasa zao. Lakini katika mazingira yanayobadilika ya nchini na ulimwengu kwa jumla, msimamo wa chama unazua maswali na kukabiliwa na changamoto kutoka kwa vijana wanachama na wasiokuwa wanachama.
CCM sasa iko tayari kukabili mtihani katika uchaguzi wa Oktoba dhidi ya Umoja wa Watetezi wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao umeunganisha vyama vinne vya upinzani, yaani Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD. Vyama vingine vidogo vimeamua kupambana kwa nguvu zao wenyewe.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya demokrasia ya Tanzanuia, vyama vya upinzani vimeona nguvu katika umoja wao na vinataka kudhihirisha nia yao ya kuibwaga CCM.
Wakati fulani katika maisha yao ya kisiasa, viongozi wengi na wafuasi wa vyama hivi walikuwa na uhusiano na CCM lakini ilifika wakati wakaona msimamo wa chama hicho haukuwapa njia ya kusonga mbele. Kwa upande wake CCM iliwaona kama waasi.
Wananchi wataka kiongozi mwenye maono
Katika vyama vipya hao wanaoitwa waasi wa CCM wamepata nafasi kutangaza maono na ubunifu wao kwa umma. Na wamevutia misururu ya watu wengi kuwaunga mkono.
Mshika bendera ya Ukawa katika uchaguzi wa rais, ambaye amehama karibuni kutoka CCM, Edward Lowasa, anategemewa kuchochea upepo mpya wakati huu inapoanza kampeni ya uchaguzi aliyoiita “Safari ya Mabadiliko, Nje ya CCM” ikiongozwa na “Ukawa – Chombo cha Matumaini”.
Lakini wakati huo huo, Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alianzisha safari ya mgombea urais wa CCM, John Pombe Magufuli akisema: CCM ina uzoefu, ina mbinu na uwezo wa kushinda.
Wanachotaka wapiga kura siyo umaarufu wa wagombea urais, bali ni kiongozi mwenye maono ya kweli na uwezo wa kutekeleza wajibu wake.
sauce Deustche Welle

No comments: