Monday 26 October 2015

Upigaji Kura dar kwa maeneo yaliokosa karatasi za kupigia kura jana .



Wananchi katika kituo cha kupigia kura cha Kimara Stop Over A na B mjini Dar es Salaam wanaendelea kupiga kura baada ya kuahirishwa kwa shughuli hiyo hapo jana kutokana na upungufu wa vifaa.Hatua hiyo inajiri baada ya maafisa walioteuliwa na tume ya uchaguzi kusimamia kituo hicho kutofautiana kuhusu nyongeza ya marupurupu yao na hivyobasi kuchoma makaratasi ya kupigia kura pamoja na sajili zake.Lakini kufikia mapema leo maafisa wa tume ya uchaguzi walipeleka vifaa vyengine vya shughuli hiyo na kukubaliana na maafisa hao.
Image captionShughuli ya upiganji kura
Awali wakaazi walikasirishwa na kucheleweshwa kwa shughuli hiyo wakilazimika kusubiri kabla ya zoezi hilo kuanza.
Kabla ya kuanza kwa shughuli hiyo maajenti waliyakagua masanduku ya kura ili kuhakikisha kuwa hakuna udanganyifu wowote unaoendelea .

No comments: