Friday 13 November 2015

Magufuli anapochemsha, wiki ya Pili pale Ikulu

Topic: Ikulu na Wizara ya Afya lugha zagongana

Juzi rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza Muhimbili na kumwondoa mkurugenzi na bodi ingawa bodi ilishamaliza muda wake na mkurugenz kahamishiwa wizarani tu wala hajafukuzwa.

Ikulu ikadai Magufuli alikasirishwa sana kukuta mashine za MRI hazifanyikazi ndio maana kaisimanisha bodi,
Lakini jana kupitia Azam Tv Katibu mkuu wizara ya Afya Bw.Mbando alisema mashine haikutengenezwa kwa sababu Magufuli alisema bali ilikuwa tu kwamba akivyotenbekea pale mchakato wa kuikarabati mashine ulishakamilika.

Alisema tatizo lililokuwepo ni kwamba Phillips wanaidai serikali zaidi ya bil 7 ndio maana waligoma kuitengeneza hiyo nashine.

Sasa mchakato wa kupunguza deni ndio ulikuwa unaendelea na zilishapatikana bil3 kutoka hazina walizolipwa juzi hao Phillips ndipo wakakubali kuja kuifanyia mashine ukarabati.

Na hili linaleta maana zaidi kwa sababu wizara haiwezi kutoa bil3 ghafla tu bila kuwa zilikuwa kwenye mchakato.

Kwa hiyo hapa ikulu ilifanya usanii wa hali ya juu kuwaaminisha watanzania kwamba kulikuwa na uzembe pale muhimbili wakati uzembe ulikuwa serikalini. Serikali ilishindwa kulipa deni kwa wakati.

Na inasemeka hili jambo halikumfurahisha Kikwete kwa sababu lilipeleka picha kwamba serkali yake ilikuwa goigoi.

Wakati yeye anasema amefanya juhudi kubwa kuiboresha Muhimbili. Na kwamba tatizo km la juzi linajulikana kwamba ni ukata na ufinyu wa bajeti ndio kikwazo.

Kikwete amedaiwa kuiambia kamati kuu jana kwamba si lazima kudhalilisha uongozi uliopita ili kuonesha tu kwamba mtu anafanya kazi. Ndio maana sasa Magufuli amesitisha zile ziara za kushtukiza ili ajipange kwanza nini cha kuzungumza kuepuka kudhalilisha uongozi uliopita.

Haya ndio madhara ya Maigizo na kulazimisha kupendwa! Ikulu kuweni makini! Mwongozeni rais vizuri!

No comments: