Friday 13 November 2015

Maoni juu ya anguko la CCM Zanzibar

ANAYEPIGA HESABU ZA ZANZIBAR AJUE ZINAWEZA KUISHIA KWENYE BALAA!

Na. Mtatiro. J

CHANZO CHA MGOGORO

Matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar kuonesha dhahiri kuwa mgombea wa CUF/UKAWA, Maalim Seif Sharif Hamad anaelekea kushinda kwa zaidi ya kura 20,000 dhidi ya Dkt. Mohammed Shein wa CCM.

Inaonekana vyombo vya dola ndani ya serikali ya Zanzibar/Tanzania kwa maelekezo ya chama tawala CCM, viliingilia mchakato huo na kumuagiza mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) atangaze kufuta uchaguzi huo na matokeo yake.

NINI KIMEJIRI: Misimamo ya pande zote mbili.

MSIMAMO WA CUF: Matokeo ya urais wa Zanzibar yaendelee kutangazwa na mshindi halali atangazwe.

MSIMAMO WA CCM: Uchaguzi urudiwe kwa mujibu wa tangazo la mwenyekiti wa tume.

KUNA MAZUNGUMZO YANAENDELEA: Nini kinaweza kuwa kinazungumzwa,

1. Uwezekano wa kutatua mgogoro huo kwa amani

2. Pande zote mbili zikubaliane njia bora za kumaliza mgogoro husika.

NINI INAWEZA KUWA MSIMAMO WA CUF KWENYE MAZUNGUMZO;

1. Uchaguzi umekuwa halali

2. Matokeo yaendelee kutangazwa na mshindi atangazwe,

3. Sitisho la kutangaza matokeo la Mwenyekiti wa ZEC ni batili kwa mujibu wa katiba na sheria.

NINI INAWEZA KUWA MSIMAMO WA CCM KWENYE MAZUNGUMZO;

1. Uchaguzi umekuwa si halali ndiyo maana mwenyekiti wa tume ametangaza kuufuta

2. Uchaguzi urudiwe kwa mujibu wa maamuzi ya mwenyekiti wa tume

SULUHU INAWEZA KUWAJE;

1. CCM wanaweza kubaki kwenye msimamo wao, kwamba uchaguzi lazima urudiwe na kuwaomba CUF wakubali.

2. CUF wanaweza kubaki kwenye msimamo wao, kwamba matokeo yaendelee kutangazwa na kwamba mwenyekiti wa ZEC hana mamlaka ya kisheria na kikatiba kufuta uchaguzi husika na kwamba wao hawako tayari kurudia uchaguzi.

MISIMAMO MIKALI:

1. CUF itasimama kwenye msimamo wake kwa sababu hakuna namna ya kuondoka kwenye hali halisi kuwa chama hicho kimeshinda uchaguzi wa Zanzibar na kwamba CCM inajaribu kuchakachua uchaguzi huo.

2. CCM inaweza kusimama kwenye msimamo feki (usio halisi) na tena ikisaidiwa na vyombo vya dola kwamba uchaguzi haukuwa huru na kwamba anayepaswa kusikilizwa ni mwenyekiti za ZEC.

NINI KINAWEZA KUTOKEA SULUHISHO NA HAKI VIKIKOSEKANA:

1.     SMZ italazimisha kufanya uchaguzi wa Rais Zanzibar, CUF itakataa kushiriki uchaguzi huo.

2. Vyama kadhaa vya upinzani kikiwemo kile cha wakulima (AFP) kitashiriki uchaguzi husika ili kuiunga mkono CCM na uchakachuaji,

3. Vyama kadhaa vya upinzani ikiwemo vitakataa kushiriki kwenye uchaguzi huu ili kuungana na CUF kutetea sauti za wazanzibari,

4. Uchaguzi utafanyika chini ya ulinzi mkali na watakaoenda kupiga kura ni wanachama wa CCM tu,

5. Dkt. Shein atatangazwa kuwa mshindi kwa kura zaidi ya 200,000,

6. Zanzibar itarudi kwenye mgogoro mkubwa, mara hii mgogoro utakuwa mkubwa kuliko ilivyowahi kutokea huko nyuma.

Popote pale ulipo na kila unapomuomba Mungu, iombee Zanzibar – Haki itendeke, vinginevyo sote tutaumizwa na kinachoweza kutokea.

Unaweza kuyaita ni maoni yangu, maono au ushauri, lakini nataka kukwambia kuwa hiyo ndiyo CALCULATION ya kile nachokiona Zanzibar.

Mtatiro J,
Dar.

No comments: