Professor Jay ni mwana Hiphop kitambo sana hapa Tanzania, lakini jina lake lina uzito wake wa nguvu kabisa kiasi cha kwamba watoto, vijana, wazee na watu wazima walilifahamu jina lake… lakini 2015 inamalizika huku akiwa na kofia nyingine kichwani, ni kofia ya Ubunge wa Jimbo la Mikumi Morogoro a.k.a Mji kasoro bahari !!
Prof. Jay kaanza kazi na kathibitisha kwamba ndani ya siku 20 anaweza kufanya kitu na kikaonekana… nakumbuka Mbunge huyo, Joseph Haule alikuwa mmoja ya Wabunge walioapishwa siku ya November 18 2015 Bungeni Dodoma.
Kazi imeanza, amenithibitishia kwamba ameanza na ukarabati wa barabara kati ya Kata ya Kidodi na Kata ya Vidunda ambapo barabara hiyo itakuwa kwenye hali nzuri ya kupitika tofauti na hali ilivyo sasa, imeharibika vibaya kutokana na mvua.
Kingine ni kwamba Professor Jay amesema kipaumbele chake ni kwenye mambo manne makubwa, kuhakikisha upatikanaji wa maji, ukarabati wa barabara, uboreshaji wa elimu na huduma bora za afya… barabara aliyoanza nayo kwa sasa ina umbali wa kama kilometa saba hivi.
No comments:
Post a Comment