Wednesday 23 December 2015

Wazanzibari: Uamuzi wa ZEC/ Jecha wapingwa na Katiba yetu


Fatma Amani Karume
Fatma Amani Abeid Karume
Na Fatma Karume (Jr).

Mwanasheria Mwandamizi Fatma Karume amesema kisheria uchaguzi haujafutwa (Shall be null and void ad initio)

Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar ya mwaka 1984 (Zanzibar Election Act No. 11 of 1984) kwa kuhusisha na issue ya ufutwaji wa matokeo ya uchaguzi kama ilivyotangazwa  na Mkiti wa ZEC Ndg. Jecha Salim Jecha. Katika uchambuzi huu nitajenga hoja 6 za kisheria zinazoonesha kuwa uamuzi huo ni batili na unafaa kupuuzwa kama ifuatavyo;

ZEC wanasema kuna vijana walipeleka kura za mgombea fulani kwa kutumia fujo.
SHERIA INASEMAJE? Ukisoma kifungu cha 74 chasheria hiyo kinaeleza kuwa “zikitokea fujo kwenye kituo cha kupigia kura, uchaguzi unaweza kuhairishwa mpaka siku inayofuata na Ofisa wa tume katika kituo hicho lazima atoe taarifa kwa tume”.

ZEC WAMEFANYAJE?

ZEC wamefanya kinyume na sheria inavyotaka. Hakuna wakala aliyelalamika kwamba kulikua na fujo ktk kituo chake wala hakuna ofisa wa tume aliyeripoti fujo hizo. Hat waangalizi wa ndani na nje wanasema uchaguzi ulikuwa huru na haki. Sasa ZEC imejuaje kulikuwa na Fujo?

Pili hata kama zingefanyika fujo isingekua kigezo cha uchaguzi kufutwa. Sheria inasema vituo vilivyoonesha fujo ingebidi zoezi la upigaji kura lisimame na liendelee kesho yake baada ya ulinzi kuimarishwa. Lakini hili halikufanyika hivyo tume imevunja sheria.


ZEC wamesema kulitokea fujo lakini hazikuripotiwa.
SHERIA INASEMAJE? Kifungu no.76 cha sheria hiyo kinatoa fursa kwa wakala kuwasilisha malalamiko kabla ya kufunga kituo. Swali la kujiuliza je kuna fomu za mawakala kutoa hayo malalamiko zimejazwa!? Jibu ni hakuna. Kwahiyo ZEC wamejitungia hiyo sababu ili kuhalalisha ufutaji wa matoeo. ZEC wamevunja sheria.

ZEC wanasema idadi ya kura ilizidi idadi ya wapiga kura walioandikishwa.
SHERIA INASEMAJE? Kifungu cha 86 cha sheria hiyo kinatoa fursa kwa mawakala kujaza fomu maalumu ya malalamiko ikiwa wataona udanganyifu wowote ikiwa ni pamoja na kura kuzidi idadi ya waliojiandikisa.
Na ikitokea hivyo ZEC haina Mamlaka ya kubatilisha matokeo bali kutoa barua kwa mgombea aliyewasilisha malalamiko ili aende mahakamani kupinga matokeo (isipkua ya Rais). Lakini Zbar haikufanyika hivyo so ZEC imevunja sheria.

ZEC wanasema matokeo yalijaa udanganyifu hivyo wameamua kufuta uchaguzi wote.
SHERIA INASEMAJE? Kwa mujibu wa vifungu 85 na 86 vya Sheria hiyo, ZEC haina mamlaka ya “kuchallenge” matokeo kwa sababu ZEC sio sehemu ya mgogoro ktk hilo shauri (part of dispute).

Anayetakiwa “kuchallenge” matokeo ni mgombea au chama chake sio ZEC. Na anatakiwa apeleke shauri lake mahakamani. Mahakama ndiyo itafanya maamuzi baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote. Kwa hiyo ZEC kufuta uchaguzi wa Zbar ni kinyume cha sheria.

ZEC wnasema kulikua na kura hewa. Yani hakukuwa na ulinganifu wa kura za kwenye maboxi na idadi iliyojazwa kwenye fomu.
SHERIA INASEMAJE? Kifungu 84 cha sheria hiyo kinasema “ikiwa kura zimehesabiwa kituoni na mawakala na wasimamizi wa uchaguzi wakakubaliana kuwa hakukuwa na dosari katika zoezi la kuhesabu kura, basi kura hizo zitahesabika kuwa halali”

Hivyo basi kitendo cha ZEC kufanya uamzi wa kukataa kura zilizokwishakubaliwa na wasimamizi ni kuvunja sheria.

Mwenyekiti wa ZEC alisema “Tume imeamua kufuta matokeo yote ya Zbar na hivyo uchaguzi utarudiwa ndani ya siku 90..”
SHERIA INASEMAJE? Sheria no.9 ya uanzishwaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ya mwaka 1992 (Zanzibar Electro Commission Act, 1992), inazungumzia uanzishwaji wa ZEC na malaka yake kisheria (Establishment and Mandate).

Kifungu no.119 (1) cha Sheria hiyo kinasema “maamuzi yoyote ya Tume yatapata uhalali ikiwa mbili ya tatu (2/3) ya wajumbe watakuwa wameridhia.”

KILICHOFANYIKA. Mwenyekiti wa Tume hakushirikisha wajumbe wenzie katika kufanya maamuzi ya kufuta matokeo. Maamuzi hayo aliyafanya peke yake kinyume na sheria inavyotaka. Hivyo basi maamuzi hayo ni batili na hayatambuliki kisheria.

HITIMISHO;
Uamzi wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar kubatilisha uchaguzi hauna msingi wowote wa kisheria. Ni uamuzi uliofanywa kwa matakwa binafsi ili kulinda maslahi ya watawala. Uamuzi huu ni batili tangu mwanzo (null and void ab initio).

Hauwezi kufuta uchaguzi kirahisi kama kufuta ubao. Hata Umiss wa Sitti Mtemvu haukufutwa kirahisi namna hiyo. Kwa kuwa Mwenyekiti wa ZEC Ndg.Jecha Salim Jecha alitoa uamuzi wa kufuta uchaguzi huo bila kushirikisha wajumbe wenzie, ni vizuri ieleweke kuwa Mwenyekiti alitoa maoni yake tu na sio msimamo wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (

No comments: