Monday, 11 January 2016

Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar yalivyotumiwa Kuwagawa na kuwabagua watu kwa rangi zao na jinsia zao.

Ikiwa leo imetimia miaka 52 Wazanzibari wamechoka kugawiwa kwa matabaka yao na ubini wao ao asili yao .Mwaka 2015 ni Mwaka Pekee ulioonesha sura ya CCM Zanzibar juu ya kuwa haikuwa na njia ya kujificha baada ya Chama cha CUF kuendelea kupata ushindi mnono wa asilimia 53% dhidi wa 46% wa CCM .


Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia Vijana wa Umoja wa Vijana UVCCM walioshiriki matembezi ya kuadhimisha Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyomalizia leo katika Viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja na kupolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,[ Picha na Ikulu.]



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa Vijana wa Umoja wa Vijana UVCCM walioshiriki matembezi ya kuadhimisha Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyomalizia leo katika Viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja(kulia) Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan,na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Taifa Sadifa Juma Khamis(kushoto) Spika wa Baraza la Wawakilishi PPandu Ameir

No comments: