Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Moh’d Shein akipakwa wino maalum na Msimamizi wa kituo mara baada ya kumaliza zoezi zima la upigaji wa kura katika kituo cha Kibele nje kidogo ya mji wa Zanzibar tarehe 25.10.2015.
Wapiga Kura wakihakiki majina yao katika daftari la kudumu la wapiga kura kabla ya kwenda katika vituo vyao vya kupigia Kura.
Afisa wa kituo Nam 2 shehia ya Tumbatu Gomani Ndg. Ali Kombo Machano akionesha Sanduku Tupu la Kupigia Kura kwa wapiga kura wa kituo hicho ikiwa ni hatua ya ufunguaji wa kituo cha kupigia kura tarehe25/10/2015.
Mapema tarehe 25/10/2015 wanakijiji cha Tumbatu wakiwa wamejipanga mstari kwa utulivu kusubiri zoezi la kupiga Kura.
Mpiga kura akitumbukiza karatasi yake ya kura ndani ya sanduku la kura za udiwani baada ya kukamilisha hatua za kupiga kura.Zoezi la Upigaji kura Unguja na Pemba limefanyika katika hali ya Amani na utulivu mkubwa huku wananchi wakijitokeza kwa wingi katika vituo vya kupiga kura.
Uchaguzi ya Zanzibar, uchaguzi ambao ulimpa Rais Dr Sheni asilimia 46% ya kura na Makamo wa Rais Maalim Seif Kupata asilimia 52.87 ushindi alioshinda Mgombea wa CCM kwa zaidi ya kura 25136..Hii ni kumbu kumbu inayofaa kuhifadhiwa kwa vizazi vijavyo.
MWENYEKITI WA ZEC ATANGAZA MATOEKO YA KURA
MAALIM SEIF ATOA MAJUMUISHO YA KURA ZAKE UTULIVU UMETAWALA KATIKA VITUO VYA KUHESABIA KURA.
Afisa wa kituo cha kupigia akibandika bango linaloonesha kuwa ni kituo cha kuhesabia kura baada ya kukamilika kwa zoezi la upigaji kura tarehe 25/10/2015.
Afisa wa kituo cha kuhesabia kura akikata vifungio vya sanduku la kura huku akishuhudiwa na mawakala wa vyama vya siasa kwa ajili ya kuanza zoezi la kuhesabu kura.
Mawakala wa vyama vya siasa vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu wakishuhudia kwa makini zoezi la kuhesabu kura baada ya kukamilika kwa upigaji wa kura shehia ya Malind Mjini Zanzibar tarehe 25/10/2015.
Afisa wa kituo cha kuhesabia kura Malindi akizimwaga chini Karatasi za kura kwa ajili ya kuanza zoezi la kuhesabu kura.
Maafisa wa kituo cha kuhesabia kura wakihesabu kura za raisi Kwa jumla kabla ya kuzigawanya kwa mujibu wa vyama.
Maafisa wa kituo cha kuhesabia kura shehia ya Saateni wakihesabu kura kwa kuzigawa kwa kila mgombea kwa mujibu wa alivyopata.
MWENYEKITI WA ZEC ATANGAZA MATOEKO YA KURA
BAADA YA MSHTUKO WA MAALIM KUTANGAZA KURA ZAKE MWENYE KITI WA TUME YA UCHAGUZI ATOWEKA NA KUTOKEZEA MAFICHONI KUTANGAZA UCHAGUZI UMEFUTWA.
CCM ZANZIBAR WACHANGANYIKIWA
JANUARY ,MAKAMBA AZUNGUMZIA UCHAGUZI WA ZANZIBAR
VIPI SERIKALI YA MUUNGANO ILISHIRIKI KUHALALISHA UFUTAJI WA MATOKEO YA UCHAGUZI WA ZANZIBAR BAADA YA MWENYEKITI WA ZANZIBAR KUFUTA USHINDI WA CUF .MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA JAJI LUBUVA HARAKA HARAKA ALITOKEZEA KWENYE TV KUSEMA KURA ZA MUUNGANO HAZIMO KWENYE UFUTAJI NI ZA ZANZIABR TU.
JAMES MBATIA AZUNGUMZIA UCHAGZUI WA ZANZIBAR
aLIEKUWA MWENYEKITI WA CUF lIPUMBA AZUNGUMZIA UFUTAJI WA UCHAGUZI WA ZANZIBAR
WANASHERIA WA ZANZIBAR WAZUNGUMZIA UFUTAJI WA UCHAGUZI NA UHALALI WAKE
ALIEKWUA MWANASHERIA MKUUU WA ZANZIBAR AELEZA KATIBA ILIVYOKIUKWA
WAZANZIBARI DUNIANI WAANDAMANA KUPINGA UAMUZI WA TUME
RAIS KIKWETE AKUTANA NA MSHINDI WA URAIS WA ZANZIBAR SIKU MOJA KABLA YA KUMALIZA URAIS WAKE
MSHINDI WA URAIS WA ZANZIBAR AKUTANA NA RAIS MAGUFULI
No comments:
Post a Comment