THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)
DIRECTORATE OF INFORMATION, PUBLICITY AND PUBLIC RELATION
P.O.BOX 10979 DAR ES SALAAM
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Imetolewa leo Tarehe 23/11/2016
Na Mbarala Maharagande- K/Naibu Mkurugenzi Habari.
KUHUSU MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI ALIOFANYA
MAGDALENA SAKAYA LEO BUGURUNI DAR ES SALAAM:
Tumepata taarifa ya kufanyika kwa mkutano na waandishi wa habari leo Buguruni katika ofisi za Chama zilizovamiwa na wahuni wachache wanaolazimisha kutaka kuendelea kutambulika kuwa ni viongozi bila ya kufuata matakwa ya kikatiba. Waandishi kadhaa wametupigia simu kutaka kujua tunazungumzia kauli hizo alizozisema katika mkutano huo. Kwa maslahi mapana ya kukidhi hitajio la waandishi, wanaCUF makini na wananchi kwa ujumla tumeonelea kutoa taarifa rasmi kama ifuatavyo;
Magdalena Sakaya anasema kuzuiliwa kwa Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad na Jeshi la Polisi kufanya kikao cha ndani kilichoandaliwa na JUVICUF –Mtwara ni jambo la sawa na kwamba asitafute mchawi kwa kuwa amekiuka taratibu za kuandaa ziara hiyo kwa kuwatumia viongozi wasiotambulika na Chama akiwemo yeye kutokuwa na taarifa.
Tunapenda kufafanua kwa mukhtasari suala hilo kama ifuatavyo;
1. Juzi Jumatatu ya tarehe 21/11/2016 Katibu Mkuu Maalim Seif aliitisha kikao cha viongozi wa kitaifa na wadau mbalimbali wa CUF kufanya tathmini ya kilichotokea katika ziara ya Mtwara na Lindi na kuazimia kuchukuliwa kwa hatua kadhaa na wakati muafaka ukifika tutatoa taarifa hizo kwa ukamilifu wake kwa Umma.
2. Magdalena Sakaya (na wenzake 8) Maftaha Nachuma, Abdul Kambaya, Masudi Omari Mhina, Thomas Malima, Kapasha H. Kapasha, Musa Haji Kombo, Habibu Mnyaa, Na Haroub Shamis. Walisimamishwa uanachama na Baraza Kuu la Uongozi Taifa katika kikao chake cha tarehe 28/8/2016 wakati Shashu Lugeye na Ibrahim Lipumba walifukuzwa uanachama katika kikao cha Baraza Kuu kilichofanyika tarehe 27/9/2016. Kwa hatua hizo ndio kumekuwepo kwa shauri na 23/2016 linaloendelea katika Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam.
3. Magdalena Sakaya ni kibaraka wa CCM anayetumiwa kama wenzake kwa muda mrefu na ameshachukuliwa hatua za kinidhamu na ngazi ya Chama yenye mamlaka nae. Kwa hiyo hatushuhulishwi nae kwa namna yeyote ile zaidi ya kumpuuza na kuthibitisha muendelezo wa kile tunachokiamini muda mrefu.
4. Taratibu zote za maandalizi ya ziara ya Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad zilifuatwa na kwamba hata kama Magdalena Sakaya angekuwa kiongozi halali wa CUF hana mamlaka ya kumzuia Boss wake wa kazi kufanya shughuli zake yeye alipaswa kutumwa na Maalim Seif na siyo kumpangia vipi atekeleze majukumu yake.
5. Wananchi wa Kusini Mtwara na Lindi na Watanzania wote kwa ujumla wameshatambua ni jinsi gani Magdalena Sakaya na genge lake la wahuni wazoataka, wavuta bangi, wanywa viroba, na vikaragosi wenzao wote kwamba wanatumika na CCM kutaka kuivuruga CUF na nguvu ya Upinzani nchini ambayo imekuwa tishio kubwa kwa uhai wa CCM na serikali zake kutokana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana mbali na wengine wanaodai kujenga Chama leo walikimbia kampeni za kuiondoa CCM madarakani Oktoba mwaka na leo hii ndio wamekuwa vipenzi wa Jeshi la Polisi na serikali ya CCM.
The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi) kinawataka wanaCUF wote makini na watanzania wapenda mabadiliko kwa ujumla kuendelea kuwapuuza vibaraka hawa na taarifa zao wanazozitoa. Tuungane pamoja kujenga umoja na upinzani Imara kuiondoa madarakani Serikali ya CCM inayoelekea kushindwa vibaya kuwatumikia watanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa imeweza kuharibu uchumi wa nchi, Mabenki kufilisika, Ajira kukosekana, madawa hospitali hakuna, gharama za maisha zimepanda, amani na utulivu kwa watendaji wa serikali na sekta binafsi imeondoka na wananchi wanaishi kwa khofu kubwa. Tuwapuuze wao na wale wote waliokula rambirambi za wananchi wa kagera. Tunamtaka Magdalena Sakaya na Mwenzake wajiandae kisaikolojia kujiunga na kundi la Mzee Stephen Wasira. Ndani ya CUF hawana na wala hawatakuwa na nafasi tena.
CUF NI TAASISI IMARA, HAKI SAWA KWA WOTE
____________________________________
MBARALA MAHARAGANDE
K/NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI
NA MAHUSIANO NA UMMA
MAWASILIANO: Airtel-0784 001 408
Vodacom: 0767 062 577
Tigo: 0715 062 577
email:maharagande@gmail.com
No comments:
Post a Comment