Saturday 27 June 2020


Hakika katiba zetu zote mbili zinampa kila mmoja wetu  uhuru wa kutafakari na kuamua kuchagua au kuchaguliwa. Na ukienda  ndani zaidi nazo katiba  za vyama vyetu zimetupa nafasi hii.
Hakika ni heshima kwetu sote kama Taifa na ni heshima kwenye uwanja wa kimataifa.
Tuvishukuru vyama vyetu kwa kutupa  fursa hizi ambazo zimetolewa na katiba mama ya Taifa.

Vyama vyetu  viendelee kutoa nafasi hii ili kila mmoja mwenye uwezo wa kuisaidia nchi yetu aweze kujitokeza na kuisaidia Zanzibar.
Pamoja na haki hizo zilizo tolewa na katiba zote pamoja na zile za vyama vyetu kwa kila raia na kila mwana chama kwa chama chake, na anza kupata mashaka na utitiri au na matumizi ya haki hii ya kikatiba na unanifanya nianze kutafakari mbali zaidi pamoja na uchanga wangu wa Siasa. Ila kwa vile nimetoka ndani ya mifupa wa wana siasa tena hasa wa Zanzibar, hakika napata mashaka makubwa na naomba nieleze hapa na niko tayari kukosolewa na ikibidi niko tayari kubadilishana mawazo na wajuzi. Kubwa zaidi ni kupata ukweli juu ya nia na dhamira ya walio wengi ambao kwa haraka haraka wame onyesha nia ya kutaka kupewa ridhaa na Chama chetu ya kuwa wagombea kupita CCM
Mashaka yangu ni kama Haya yafuatayo.
1. Idadi ya watia nia walio jitokeza ambao hadi jana tarehe 26/06/2020 wamefikia thelathini (30) na Naamini wengine bado wako njiani wanakuja.
Hapa najiuliza maswali Haya yafuatayo. Hivi ni nini maana ya tukio hili? Jee ni kweli haya ni mapenzi na ukereketwa kwa chama chetu au kuna nini nyuma ya pazia.
Jee watu hawa wameona nini kime pungua au kokosekana Katika awamu hii ya Dr. Ali Mohammed Shein.
Kwangu mimi hili naona ni uthibitisho wa ombwe la uongozi na hakika nina mashaka na wengi wa watia nia na huko mbele nita eleza khofu yangu kwa wengi wa watia nia hawa.
Ila kubwa naomba chama chetu na Serikali zetu hasa hii ya Zanzibar Ijitathmini, mana kwangu huu sio muhamasiko wa kawaida Bali lipo jambo kubwa na inawezekana liko nje ya chama ila ndani ya Serikali, lakini pia inawezekana liko ndani ya chama na ndani ya Serikali. Sioni na sikubali kwamba hawa wote wame hamasika wenyewe na kwa bahati mbaya.
Na Siamini na Wala sikubali kwamba wote hawa ni watia nia ya dhati lakini bado naendelea kutafakari na kwamba jawabu litapatikana mapema iwezekanavyo. Maana kila dalili zina onyesha hapa lipo tatizo na kubwa kuliko yote ninalo liona ni hamasa iliyo tengenezwa kwa makusudi ikiwa na dhamira maalum ambayo khasa ni kuharibu mchakato huu kwa kuutia doa na hatimae kuyumbisha vikao na hasa kumyumbisha Mwenyekiti wetu ambae katika hili naomba nimuombe kwamba bado anahitaji sana kuwa sikiliza wazee wetu hasa wale ambao wamepitia katika nafasi mbali mbali  za ki uongozi na ambao hawana maslahi binafsi. Kama vile Dr SALMIN AMOUR, Dr Bilal.Dr Salim Ahmed Salim na baadhi ya wazee wanao Ifahamu  vyema ccm na hatua za mapambano ya ushindi na namna tutakavyo ingia kwenye vita ya upinzani baada ya kukamilika, kwa mchakato wetu wa ndani ya ccm.
2. Ubora/Quality ya watia nia.
Napata tabu sana na wengi wa watia nia walio jitokeza. Siamini na sikubali kwamba wengi wa hawa kama kweli wanao uwezo  wa  kutuongoza na kutufikisha tunako fikiria kwenda kama Nchi.
Ninapo sema Ubora nina maana nyingi kubwa kuliko zote ni uwezo wa kutambua matatizo yetu kama Nchi na uwezo wa kuyapatia ufumbuzi wa kudumu matatizo yetu. Baya zaidi sio wengi kati ya watia nia hawa ambao wanaelewa hata maana ya neno njaa au kukosa mlo mmoja na hata kuelewa nini maana ya neno umasikini.
Ipo haja ya kutafakari sana juu ya hili mana sisi raia wa kawaida tunayo matumaini makubwa na kiongozi atakae teuliwa kutuongoza, tukiamini imefanyika kazi kubwa sana ya kumtafuta, kumchekecha na hatimae kumleta kama mgombea wetu. Kazi hii tuna iacha kwa chama chetu na kwa public mana Mitazamo inatofautiana.
3. Uasili na uelewa wa historia ya chama na nchi yetu. Nime tafuta na kupitia taarifa za watia nia wengi ambao kwa mtazamo wa haraka haraka wengi wao ni kushindanisha elimu zao na hasa kwa sababu elimu ndio kigezo kikubwa kinacho angaliwa kwa imani kwamba ndio wenye uwezo wa kutusogeza hatua kubwa moja mbele kutoka hapa tulipo. Ila Mimi kwa upande wangu naomba kumnukuu Muasisi wetu wa Mapinduzi ya Zanzibar Babu yetu Karume senior ambae aliwahi kusema "Tumesoma hatukutambua, tumejifunza tumejuwa." Hii maana yake ni kwamba elimu sio kigezo kikubwa katika kufikia malengo ya Taifa ila ni sehemu ya Sifa ya ziada katika kuongoza Taifa. Hivyo naomba tafakuri yakinifu ifanyike hasa kuelewa historia ya kila mtia nia na nini mchango wake kwa Chama chetu na Taifa letu. Sio lazima kila mmoja awe mwana Mapinduzi kwa umri, lakini awe mwana Mapinduzi kwa vitendo na dhamira na hasa katika kuhakikisha anaelewa safari yetu ilipo anzia na wapi tunafikiria kufika na kulifikisha Taifa. Naomba hapa pawe ndio msingi wa tathmini yetu mana wasomi wetu wengi wametufikisha pabaya hadi kuiingiza nchi kwenye mikataba ya hovyo huku tukiwa tuna waamini na hadi kufikia kuuza baadhi ya tunu zetu za Taifa na ambazo kwa kweli haikuwa sawa na wala haikuwa busara na mfano mmoja mdogo sana ni kuuzwa kwa jengo la Mambo msiige ambalo moral responsibility inakataa. Bado wasomi wali shawishi na kusimamia mchakato na hadi sasa tulipo fika tunaelewa hakuna maelezo wala hakuna pesa iliyo ingia kwenye Mfuko mkuu wa Serikali. Maana yake haya ni matumizi mabaya ya ofisi na taaluma za wasomi wetu.
Kufanya manunuzi ya hovyo na ya kifisadi hadi kuiingizia hasara nchi yetu kama vile kununua meli mbili mbovu kwa gharama kubwa na hadi sasa hakuna anae toa majibu na maelezo yoyote mana meli tunazo zizungumza kila mmoja anaelewa kwamba hazina hata miaka mitatu na zote sasa  ni mbovu.
Kushiriki kukihujumu chama chetu hadi kushiriki kwenye kuiba mali za chama chetu na taarifa zote zina onyesha na kuwataja wazi wazi juu ya ushiriki wao kwenye matendo haya maovu. Chama chetu kwenye vikao na taarifa vilifikia makubaliano juu ya nani alishiriki na kwa kiwango gani, pamoja na maelekezo ya vikao  kutolewa, bado kwa upande wa Zanzibar hakuna lililo fanyika na hakuna aliye chukuliwa hatua yoyote.
Hawa ndio vijana na wasomi wetu ambao tuliamini kwamba  watatumia taaluma zao kulisaidia Taifa na Chama chetu, lakini wao ndio vinara wa uchafu huu mkubwa ambao ni aibu hata kuamini kwamba wao ndio watrnndaji wa haya.
Kwa ufupi ni mengi machafu na ya hovyo yamefanywa na wasomi wetu. Bado naamini sio wote lakini taaluma za wasomi wetu hazijawa msaada kwa Taifa na chama chetu na hivyo bado  haijawa na wala sio kigezo cha kukitegemea.
Tunahitaji wenye kuji elewa na kuamini kwamba tunaweza kujikwamua sote kama Taifa na hasa ukizingatia kwa mazingira na wingi wetu bado tunayo nafasi kubwa ya kujikwamua na sio vyenginevyo.
4. Imani na Muungano na Mapinduzi yetu mtukufu. Kwa Mtizamo wangu wengi wa watia nia wetu sio waumini wa kweli wa Muungano na
Mapinduzi yetu matukufu. Kubwa ni tabia ya kuamini na kuaminishwa kwamba Mapinduzi haya hayakuwa muafaka na kwamba Muungano ndio tatizo letu. Aidha ni mjengeko wa tabia za vijana na wasomi wetu kupenda kutaka kuwa aminisha mataifa ya nje kwamba wao ni watu wa mrengo wa kati(liberal) na kwamba watasimamia haki, usawa na kuangalia mbele bila ya kuelewa kwamba tatizo letu moja kubwa ni kwa baadhi ya mataifa haya yange penda kutuondoa katika misimamo yetu kama Taifa na tufuate matakwa yao.
Hivyo wasomi wetu wengi ni wepesi sana katika kutetea kwa uwazi Muungano na Mapinduzi yetu. .
5. Kujitolea kwa maslahi ya Taifa. Si wengi miongoni mwa watia nia wetu ambao wame jionyesha na kujipambanua kwamba wao ni wenye kujitolea kwa maslahi ya Taifa na watu wake. Zaidi ni kutengeneza matukio ambayo kwa juu yata onyesha kwamba wao ni wazalendo ila kwa undani hakuna zaidi ya kujenga image na Umimi
6. Kuamini katika kuendeleza dynasty.
Hapa nakusudia wengi ya walio jitokeza mambo yafuatayo ndio makubwa yanayo jitokeza.
a. Kulinda uongozi wa kifamilia na hasa kwamba uongozi umetokana na family kwa hivyo ipo haja ya kuendeleza jina la family na sio kukerwa na kukereketwa na matatizo ya wanyonge walio wengi na hasa kwa vile wao sio sehemu ya wanyonge hao na wengi hawaelewi unyonge ni nini.
b. Kulinda maslahi, mali zao, kazi na vipato vilivyo patikana kwa njia zisizo sahihi. Hapa naweza kuwa na kosea , ila dalili na viashiria kwa wengi walio jitokeza ni kutaka ama kujilinda wao na walivyo vichuma au kutumika kuwalinda wengine kupitia wao ili wasipate mashaka na mali na maisha yao. Hivyo wametumika ili kuwa ni ngao ya kuficha maovu ya wanao wataka kuwalinda.
c. Kushiri na kushirikiana na wafanya biashara waovu. Hili hali hitaji tochi. Wengi wa walio jitokeza, lengo ni kushirikiana na wafanya biashara waovu kwa maslahi yao. Hili ni wakati ndio utakao amua. Ila dalili zipo wazi.
d. Ufakhari wa kuchukua form kwa mana ya kuchukua. Miongoni mwa walio chukua form za kuomba ridhaa  si kweli kwamba ni wao wenyewe wanao uwezo au wanayo dhamira ya kweli ya kuisaidia Zanzibar na Taifa, Bali ni tabia ya sasa iliyo jengeka na inayo endelea kuota mizizi ya watu kutaka kujionyesha mbele ya jamii kwamba mimi nipo na nimethubutu. Hii ime jionyesha kwa kiwango kikubwa na inaleta mashaka kwa wengi kujiuliza kama kweli Taifa lime fikia hapa. Na kama kweli tunaweza kusonga mbele endapo hatuku tengeneza mfumo bora na imara wa kuwa pata watia nia ya kuongoza Nchi.
e. Kupambana na kuhakikisha wana uondoa Muungano wakiwa ndani ya ccm na Serikali yake.
Hapa Hatuhitaji kuwa wataalamu wa nuclear au rocket science kuliona hili. Ila ukweli ni kwamba maandalizi ya kuifanya ccm ishindwe yalianza kipindi cha pili cha Rais Amani Karume na kila jitihada zilifanyika pia  kwenye  kipindi cha pili cha Rais Dr. Shein cha kuiondoa Serikali ya ccm madarakani. Na wengi wa viongozi waandamizi  ndani ya Serikali na ndani ya ccm walisha andaliwa na kuaminishwa kwamba ccm ndio imefikia mwisho na wengi wao walijitolea kusaidia mchakato huo. Wengine walisha ahidiwa nafasi za uongozi katika Serikali mpya. Hivyo pamoja na jitihada zile ku shindikana bado hazija sita. Na kwa mtizamo wangu, bado viongozi hawa waandamizi walio ndani ya Serikali na Chama na wengine walio staafu ndio vinara wa kuhakikisha ccm Inaondolewa madarakani na lengo lao  kubwa likiwa ni kuendelea kujaribu kuiondoa ccm madarakani, huku wao wakiwa ndio wahandisi wa mchakato huu lakini wakiwa ni viongozi na watendaji ndani ya Serikali na ccm. Kubwa lijalo ni kupeleka mswada kwenye baraza la kwanza la wawakilishi la Serikali ijayo wa kuto kuwa na imani na Muungano na hivyo kupitishwa kwa hoja ya kuitishwa kwa kura ya maoni ili kukubali au kuukataa MUUNGANO.
Tuna wafahamu na tuna fahamu vikao vinakaa usiku na mchana na sasa kwa asilimia kubwa vikao vime hamia Karume Airport Zanzibar pamoja na nyumbani kwa kigogo Mstaafu  ambapo mipango mingi hufanyika. Hapa taarifa zina sema hata Mkulu aliyeko madarakani sasa nae hushiriki kwenye baadhi ya vikao nyumbani kwa mtangulizi wake.
Kama mtakubali watu wameanza kumkimbia Dr. Shein hadi siku ya kufunga baraza la wawakilishi wali kimbia hadi kupiga picha nae na kukimbilia vikao vyao airport kwa vile kwa sasa Dr. Shein hana jipya na wao lazima maisha yasonge.(Tafuteni nani hakupiga picha nae ukiacha wale walio kuwa wana wahi ndege ya Pemba)
Hitimisho.
Naomba niseme haya ni maono na maoni  yangu kama Mtanzania, Mzanzibari na mwana ccm ambae naiangalia ccm na Zanzibar, lakini naliangalia Taifa la Tanzania kwa miaka Mia moja ijayo bila ya kumuonea wala kumbagua mwana ccm yoyote na hasa tunapo ongelea watia nia wetu. Kubwa kwangu mimi ni kutafakari nia ya kweli na Madhumuni ya utitiri huu ulio jitokeza na unao endelea kujitokeza kwa Jina la uhuru wa kikatiba na upenzi na upendo kwa CCM.
 Naomba chama chetu kipate muda wa kutosha kuwachambua wagombea wote kwa kina kuanzia maisha yao hadi sasa na mchango wao kwa chama chetu  na Taifa na kuona  wame kifanyia nini chama chetu na Taifa kwa ujumla.
Hapa hatuna nafasi ya kukimbia wala kukimbilia. Hatuna nafasi ya kuendelea wala kuongea, hatuna nafasi ya kulipa fadhila wala kumuona Haya mtu yeyote kwa sababu ni rafiki yetu, ni mtoto wa mkubwa wala kwa sabsbu tukipata fadhila kutoka kwake.
Tuna zungumza Taifa na khatma ya chama chetu. Lakini pia Chsma chetu kisisahau hapa tuna chagua mshika bendera ya chama chetu ambae hatimae tuta msimamisha kupambana na vyama vyengine vyote. Maana yake hii ni vita ya ccm dhidi ya vyama vyote. Tusi sahau, ni punda walio badilishwa soji. Maana yangu ni kwamba watu ni wale wale ila wamehama kutoka chama kimoja kwenda chengine. Wote hawa ni washindani wetu na kwa sasa ni mapambano ya kufa na kupona.
Chama kuhakikisha hatutoi nafasi na kazi kubwa ya kuanza kuwa shawishi wanachama wetu juu ya Ubora wa chaguo la chama, Bali iwe ni kazi yetu sote kupambana baada ya chaguo letu na wala sio chaguo la KUNDI fulani.
Hatuhitaji urithi wala ufalme. Tunahitaji Rais wa wanyonge na ambae anaelewa nini maana ya umasikini na nini maana ya kushinda na njaa na akerwe na umasikini wetu na maendeleo duni. Hakika tusimtazame mtu machoni Bali moyoni na tujiridhishe bila ya chembe ya mashaka kwamba huyu ndiye chaguo la wengi na abebe bendera yetu na sote tuwe team moja ya mapambano dhidi ya upinzani. Vyenginevyo mwaka huu matokeo ya kura yata tolewa saa4 asubuhi baada ya kufunguliwa vituo vya kupiga kura.
Bado mimi nasema
NAMI NATAK HUO URAISII WA ZANZIBAR

No comments: