Sunday, 9 August 2020
MAPOKEZI YA MAALIM SEIF ZANZIBAR SUNDAY AUGUST 7/2020
TAFAKURI YANGU JUU YA MAPOKEZI YA MAALIM SEIF - ZANZIBAR.
1) Wazanzibar wameithibitishia Dola, CCM na Dunia nzima kuwa licha ya Figisu zoote zilizofanywa kukandamiza Demokrasia ya Vyama vya Upinzani, kukiua chama cha CUF, bado Wazanzibar hawajotolewa kwenye DHAMIRA yao ya KUIONDOSHA CCM MADARAKANI, na kuijengea Heshma Zanzibar ambapo hilo ndio lengo lao KUU.
2) UMMA umechoka na siasa za Ubaguzi, siasa za Uunguja na Upemba ukusini na Ukaskazin, WAMECHOKA nazo, ndio maana jana watu wa pande zote za Unguja walihudhuria, WAZANZIBAR wanahitaji kuwa kitu Kimoja kwa Maslahi ya Taifa lao na kizazi chao.
3) Jeshi la Polisi kujaribu kuzuia watu wasipite barabara ya Michenzani na Umma ku react kw Nguvu zao zote, ni ishara ya hatari kwa Taifa endapo huko mbele Jeshi la Polisi litaendelea kuonesha Siasa za Upendeleo wa waziwazi na siasa za Ubaguzi kwa kuwaruhusu CCM wajifarague lakini wapinzani wawabane hilo LITAHATARISHA Amani ya Nchi, maana Vijana wameshachoka na wameshafika kikomo katika kuvumilia UONEVU wa Jeshi la Polisi.
4) Licha ya Umma mkubwa uliojitokeza barabarani jana, hakuna hatta karatasi ya CCM iliobanduliwa achilia mbali Bendera lakini hii imekuwa kinyume chake mara zote pale CCM wanapokuwa na mikusanyiko yao licha ya kuwa na watu wachache barabarani lakini Fujo na Ugomvi wa makusudi kwa kupachua Bendera za ACT - WAZALENDO au kuvunja vibaraza vya ACT - WAZALENDO imekuwa ni ADA kwao, huku vyombo vya Dola vikiwaangalia tu pasi na kuchukua hatua yoyote dhidi ya Uchokozi huo wa Makusudi.
5) SIASA SAFI, SIASA ZA KIUSTAARABU, na SIASA za AMANI, Zinawezekana kabbisa kufanyika pale tu Jeshi la Polisi linapotenda HAKI kwa pande zote.
By; MAHMOUD A. MAHINDA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment