Thursday, 14 February 2013

Kenya Wana ukabila je sisi tuna nini kama sio udini ?

Wakenya wameamua kuwachukua wakuu wao wa Tume ya Uchaguzi kuwapeleka Kigali Rwanda kuwoanesha athari ya mauaji ya Halaiki Kule Rwanda Kabla ya kumalizika uchaguzi na kuaonya kuwa Haki Ikikosekana au Uongozi Mbovu ukiwekwa kwa nguvu hapo March 4th kuna khatari kubwa ya Kenya kuingia kwenye Vurugu zisizoweza kuzimika.Nilikua Kwenye Party ya New Year Hapa Washington na Mtanzania Mmoja ameowa Mkikuyu wa Kenya Nilimuulizahuyu dada Mkikuyu ulikua na Furaha Kaka yako aliposhinda Urais wa Marekani alinimbia mimi sio Mpumbavu Siwezi kumpigia kura Adui wa Wakikuyu Nilimpigia Mzungu sikumpigia kura Obama .Kuanzia hapo Kichwa changu kiliona athari ya ukabila na kuona Wahamaiji wote wa Afrika Walivyokuwa kifua mbele Kuwa wamepata Kiongozi mwenye asili ya Bara Lao ila Mkikuyu huyu alinipa shock kubwa . Mgogoro wa Udini ulikua makapuni kuanzia 1950 Pale Waingereza Walipokua Wanaiongoza Tanganyika Waislamu wa Kilosa Waliadamana kupinga kujengewa Bucha Za nguruwe Kwenye maeneo wanayoishi na Muingereza aliweka sheria kuhakikisha kuwa Hak iza Waislamu zinaheshimiwa kwani zinagusa hsiia za kidini, Mwaka 1998 Pale Mwembe Chai Magomeni Dar na Bucha za Nguruw zilivamiwa na kuvunjwa , Jioni ya siku ya Pili Mzee Ruksa aliamkia Unguja na kutoa Khutba Kali Kuwa wanaotaka kula Hata Chura wale ni Ruksa ! Na Kule Unguja tumesikia mara nyingi kuanzia 2003 hadi leo Vilabu vya Pombe kwenye Makazi ya Waislamu kwua ni kero ilioifanya Jamii kuchukua sheria mikononi kwa vile Mamlaka inayohusika imeshindwa kueka sheria za kuwaridhisha Waumin i wa Dini zote Mbili ni kama Vile Mubarak wa Egypt na Gadafi wa Libya na leo ASad wa Syria kua hao ni wahuni tu wanaoleta fujo ila Kiukweli kuahirisha matatizo Yapo yako mvunguni tu .Kule Zanzibar Vialbu vingi vya Pombe ni vya wageni na hawajali Mila za wakazi wao wanatoa rushwa Manispaa wanapata Leseni Pombe inauzwa na utalii unakua na faida kebe kebe ila Kiukweli Tatizo liko pale pale. Tatizo la Upangaji wa Miji yetu na nguvu ya Wananchi kwetu ni Mwiko .Nitawapa Mfano Mara Moja nilialikwa kwenye panel ya Baraza la Mtaa mmoja wa Washington na Kampuni ninayotumikia na kufuatana na Wakili wa Kampuni yetu na Viongozi wa juu wa Kampuni yetu kwangu ilikua ni learning Lesson .Kampuni yetu ilikua ifungue tawi la kuuza vitu na Pombe ila watu wa Eneo lile wote Walipinga Duka hili kuuza Pombe na waliopinga wote Walikua ni Wakristo ni mimi peke yangu niliekuwa Muislamu pale.Leseni ya Duka ilitolewa ila Leseni ya Kileo ilipingwa na Wakazi wa eneo lile , Hawakuidhika kuwa maeneo ya makazi yao kuekwe sehemu ya kuuza Pombe .Tuwaulize wat uwa Manispaa zetu wanawauliza watu wa maeneo haya kuwa wanataka Vilabu vya Pombe au Bucha za Nguruwe kwenye maeneo yao.Demokrasi ni kitu Kizuri.Ushauri wangu ni Manispaaa zetu ni Kurudisha haki ya Wananchi kujiongoza wenyewe sio Kuongozwa na Rushwa. Hatuwezi ndio kua na Bucha za Waislamu na Wakristo , itafika siku tutasema tuwe na Bucha tofauti , Shule tofauti , migahawa tofauti na mitaa ya Wasialmu na Wakristo .Kinachotakiwa ni kuongeza Interfaith activities baina ya dini hizi mbili , Kueka mjadala au Kuunda tume ya Kusikiliza madai ya Waislamuna Kwuaweka Pamoja Makadinali na Ma sheikh wetu Vipi Tuishi kwa kuheshimiana bila ya kufikia kuuwana nani achinje nyama , Rafiki zangu wengine ni Wakristo huwaalika Nyama choma na hawaniulizi Umeichinja vipi ila Najua vipi wao dini yao inawafunza .Pia nilibahatika kutoa huduma Kwa jamii ya kiyahudi Hapa Marekani na kuona wasivyoaaamini Wakristo Kuhakikisha haki yao ya Kidini inavyoheshimiwa ( Kosher FOOD) sisi tuna Halal Food hata label za Vyakula hapa mareakani na Ulaya vinaatambua haki za Wayahudi na Waislamu na sasa imekua ni market strategy nani anaheshimu dini hizi zaidi kuhusu Vyakula Vyao CCM iache ubabe irudi KWa wananchi Kbla ya nchi kuwa vipande Vipande . USipoziba Ufa utajenga Ukuta Namalizia hapa kwa leo .Tyari Kule jamii forum na kwengineko matusi ya kwua watauche tule nguruwe wetu na waache kujenga Bucha maneo yetu ni Hatari ilioko mbele yetu .Kama Watawala Wamelala Please Amkeni sifike ilivyofikia kuuwana kwa Nyama si hivyo tutatue tatizo Litangazieni Tiafa no more meat wote tuwe Vegetarian no more Meat ! Machafuko makubwa yametokea katika kijiji cha Buseresere Wilayani Chato Mkoani Geita kati ya waislam na wakristu na kupelekea watu 10 kujeruhiwa vibaya kwa mapanga huku mchungaji wa kanisa la Pentekoste Assemblies of God Mathayo Kachila (45) akipoteza maisha kwa kuchinjwa na watu wanaodaiwa ni waumini wadini ya kiislam kisha mwili wake kutelekezwa kwenye vibanda vya maduka ambavyo vilikuwa jirani na eneo hilo. Habari za kaminika eneo la tukio hilo lililotokea majira ya asubuhi zimeeleza kuwa chanzo cha machafuko hayo ni watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wadini ya kiislam kuvamia bucha lililokuwa likiwauzia nyama wakristo wa kijiji hicho waliokuwa wamepanga foleni kwa wingi kusubili huduma hiyo. Imeelezwa kuwa Wakristu hao walikuwa wamechinjia ng'ombe mmoja na mbuzi wawili eneo la Kanisani kabla ya kuleta nyama hiyo katika bucha hilo lililopo eneo la Buselesele Sokoni na ndipo walipokumbana na kadhia hiyo ya waislamu. Tukio hilo lilianza majira ya saa 2 asubuhi muda mfupi baada ya nyama kuwasili katika bucha hilo la wakristu kwa ajili ya kuuzwa jambo linalodaiwa liliwakera waislam ambao waliivamia bucha hiyo kwa lengo la kuifunga. Wakati wakristo wakitafakari uwepo wa waislam kwenye bucha lao lililpambwa kwa maandishi BWANA YESU ASIFIWE,YESU NI BWANA, ndipo waislam ambao kwa wakati huo walikuwa wametapakaa mtaani kwa lengo la kuhamasishana waliongezeka eneo lilipo bucha hilo na kisha kuimwagia nyama iliyokuwa kwenye bucha hilo vitu vinavyodaiwa kuwa ni sumu. Kutokana na hali hiyo wakiristo walionekana kukerwa na kitendo cha waislam kuimwagia nyama hiyo vitu hivyo na kisha mapambano yalianza baina ya wakristu na waislam ambapo mbali na wakristu kutumia mawe waislamu wao walitumia mapanga na majambia. Hata hivyo wakati mapambano hayo yakiendelea mchungaji huyo ambaye kwa sasa ni marehemu alifika eneo la tukio ili kujua kulikoni na ndipo naye alipojikuta akishambuliwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za kichwa chake na alifia njiani wakati akikimbizwa katika hospital ya Wilaya ya Geita kwa matibabu zaidi. Mbali na mchungaji huyo kupoteza maisha,wengine waliojeruhiwa ni pamoja na Said Ntahompagaze(45),Sadick Yahaya(40),Yasin Rajab(56),Vicent Damon(22),wote wakazi wa Buselesele na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Ramadhani ambaye yuko mahututi katika wodi namba nane katika hospital ya wilaya ya Geita. Hata hivyo watu wengine watano ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja walitibiwa na kuruhusiwa kutokana na hali zao kuwa nzuri. Jeshi la polisi Wilayani Chato na Geita lilifika eneo la tukio hilo majira ya saa 4:30 na kukuta uharibifu mkubwa umekwishafanyika ikiwa ni pamoja na kukuta duka la Mwenyekiti wa BAKWATA wilaya ya Chato Yusuph Idd linalotumika kwa biashara ya M-Pesa na vinywaji baridi likiwa linateketea kwa moto uliodaiwa kuwashwa na waumini wa dini ya kiislam. Mkuu wa Wilaya ya Chato Ludorick Mpogolo aliyefika eneo la tukio muda mfupi baada ya polisi kuwasili eneo hilo mbali na kusikitishwa na kitendo hicho aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati serikali ikiangalia njia sahihi za kutatua mgogoro huo ambao unakuwa kwa kasi kila kukicha. Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula mbali na kuthibitisha kuwepo kwa tukio hilo, alionyesha kukerwa na watu ambao wanafurahia vurugu zisizo na msingi na kuonya kuwashughulikia wale wote watakaobainika ni wachochezi wa masuala ya kidini.

No comments: