Thursday 2 January 2014

HATIMA YA ZITTO NA WENZAKE KUJULIKANA KESHO !

Kutokana na maswali kutoka kwa wanahabari wa vyumba mbalimbali vya habari juu ya agenda za kikao cha Kamati Kuu kesho,Chama kimetoa kauli ifuatayo; Ni kweli kutakuwa na mkutano maalum wa Kamati Kuu ya chama kesho tarehe 3 Januari 2014 Jijini Dar Es Salaam. Ajenda kuu katika mkutano huo ni tatu;

Mosi: Kupokea taarifa kuhusu mchakato na maudhui ya mabadiliko ya katiba Kamati Kuu itapokea taarifa juu yakupitishwa kwa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba 2013, kupitishwa kwa muswada wa kura ya maoni wa 2013, uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum na kutolewa kwa Rasimu ya Katiba Mpya.
Pili: Kupokea utetezi (wa mdomo) wa wanachama watatu kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwao.

Wanachama hao walishajulishwa makosa yao kwa maandishi na wamewasilisha utetezi wao wa maandishi. Wataitwa kwenye kikao kwa kuzingatia matakwa ya kanuni 6.5.2 (b) na 6.5.2 (d) kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.

Tatu: Mpango Kazi wa Chama kwa mwaka 2014

Mpango Kazi wa chama ni sehemu ya hatua za utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Chama wenye dhima ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya chama na taifa.

John Mnyika
Mkurugenzi wa Mawasiliano



Wakati huo huo Mheshimiwa Zitto amezuia kikao hicho kumjadili ameomba mahakama kuzuia kamati kuu ya chama changu kunijadili mpaka rufaa yangu isikilizwe na Baraza Kuu la chama. Sijaomba kuzuia kamati kuu kuendelea na kikao chake. Nimeomba kamati isinijadili maana nina rufaa kwenda Baraza Kuu kwa jambo hilo hilo ambalo kamati kuu inataka kuliamulia. Wakili wa chama Tundu lissu aliweka mapingamizi akisema mahakama haina mamlaka kujadili masuala ya vyama na wanachama wao.
Jaji John Utumwa katupilia mbali mapingamizi yote yaliyowekwa na Tundu Lissu.  Mahakama ndio Chombo cha kutoa haki. Asante Wakili Albert Msando.
Haki itatendeka…

No comments: