Friday 10 May 2013

JEE URIPUAJI WA ARUSHA SI UGAIDI KIGEZO GANI ? MAUAJI YA PADRI ZANZIBAR KUITWA UGAIDI.



Kikwete akiwaaga Wanajesh iwa Tanzania kuelekea Congo kulinda Amani, uchaguzi ujao si hasha ukawa kama Kenya usalama wa ndani ilikua ajenda ya uchaguzi 2015 au Waziri NChimbi ajiuluzulu ameshindwa kulinda raia na mali zao !

Watanzania tusiwe Polisi wa Dunia kama Marekani tusigeuke Wajenzi banda lake kuvuja !

Imefika Wakati Serikali ya CCM ifikirie kujenga utamaduni wa kulinda Ulinzi wa ndani kwanza ndio serkali yetu ijenge jina la Kimataifa kulinda amani ya mataifa mengine.
Tunajua kuwa wanajeshi wetu wako Lebanon , Darfu Sudan na Seraleone na bado . ila La kujiuliza jee CCM kwa nini iemshidwa kueka Ulinzi wa kuwalinda Raia wetu leo Watu wanaweza kutumia silaha Kumuuwa PAdri kule Zanzibar na kumfanya Waziri wetu wa Mambo wa Ndani kuitangazia Zanzibar Kuna ugaidi lakini suali langu jee Miripuko ya Kanisa Arusha Kwa nini hakutoa Kauli na Kusema umeingiliwa na Ugaidi ?

Hii double standard Ya Kuwa mauaji ya mtu mmoja Zanzibar yawe ugaidi ila mauaji na majeruhi kadhaa Arusha tunaambiwa Serikali inashughulikia ila huu si ugaidi , lakini raia wa mataifa ya nje wamekamatwa lakini sio ugaidi yale mauaji ya Zanzibar yaliokuwa hayakuhusisha wageni yalivikwa koti la Ugaidi na kutangaziwa Dunia CIA na FBI wa Marekani watafika Zanzibar kuwakamata magaidi na Makomnadoo hawa Marekani walishtukia harufu ya siasa kutaka kutumiwa Zanzibar na kuamua kutimua zao hadi leo kimyaaa !!
Hata tukio hili la Arusha limezusha vichwa vingi vya habari nchi za magahribi kuwa Wakristo na Viongozi wao hasa Zanzibar wako hatarini la kujiuliza jee Habari hii ya Arusha kwan ini iunganishwe tena na tukio la juzi la ARUSHA kama sio ajenda ya siri !

Jee Huu ni Uungwana Ndugu Zangu Ugaid iwa East Afrika una formula gani kuitwa Ugaidi?


MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amewaasa watanzania kuacha dhana ya kulihusisha tukio la mripuko unaodhaniwa kuwa ni bomu uliotokea katika Kanisa katoliki Wilayani Arumeru Mkaoni Arusha lisihushishwe na masuala ya kidini wala kisiasa.

Balozi Seif alitoa kauli hiyo alipofanya ziara fupi ya kuangalia majeruhi wa mripuko huo waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha pamoja na kuwapa pole Viongozi pamoja na waumini wa Kanisa lililopata maafa hayo.

Balozi Seif alisema tukio hilo ambalo lina dalili zote za Kigaidi limeshitua Taifa na kuwakera wananchi wote Tanzania Bara na Zanzibar na linafaa kulaaniwa na wapenda amani wote popote walipo.

Alifahamisha kwamba hiyo ni fitna inayojengwa katika kuleta chuki baina ya Serikali na wananchi hasa waumini. Hivyo aliwanasihi Watanzania kuendelea kutulia na wala hakuna haja ya kuanza kutuhumiana ndani ya kipindi hichi kigumu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea haja yake kufuatia vyombo vya ulinzi kufanikiwa kuwakamata baadhi ya wahusika wa mripuko huo wapatao 10 hadi hivi sasa ambao kati yao wanne ni raia wa Saudi Arabia na mmoja raia wa Kenya.

Balozi Seif aliwahakikishia wananchi wote pamoja na waumini walioathirika na tukio hilo kwamba Serikali itahakikisha inawashikilia wale wote waliohusika na njama hizo na kuwachukulia hatua za kisheria kutokana na udhalimu wao huo.

“ Tungeliomba jambo hili baya lisitokezee tena katika nchi yetu kwani linaonesha kuleta fitna kati ya Serikali na wananchi wake “ alisisitiza Balozi Seif.

Akizungumzia suala la kidini, Balozi Seif alisema Serikali zote mbili zimetoa uhuru wa kuabudu ambao umo ndani ya katiba na kamwe haitavumilia kuona uhuru huo unaingiliwa na watu wachache.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas.

Hali ya kutafuta jibu la mlipuko wa bomu huko Arusha bado ni tete watuhumiwa zaidi wakamatwa ungana na gazeti la Nipashe kupata hali ilivyo mpaka sasa.

Idadi ya watuhumiwa wa tukio la kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, mkoani Arusha Jumapili iliyopita, imeongezeka kutoka tisa hadi 12.

Watuhumiwa hao wametajwa na Jeshi la Polisi kuwa ni Victor Ambrose Kalisti (20) na Joseph Yusuph Lomayani (18), ambao wote ni waendesha bodaboda wakazi wa Kwa Mrombo, mkoani Arusha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha alhamisi, aliwataja watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa kuwa ni George Batholomeo Silayo (23), ambaye ni mfanyabishara na mkazi wa Olasiti; Mohamed Sulemani Said (38) mkazi wa Ilala, mkoani Dar es Salaam, ambaye polisi imemtaja kuwa ni mwenyeji wa watuhumiwa raia wa Uarabuni na kwamba ndiye aliyewafuata kwa gari binafsi uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam na kuwachukua hadi Arusha katika hoteli moja iliyoko karibu na kituo kikuu cha mabasi yaendayo mkoani humo na nje ya mkoa.Kusoma zaidi bofya

Wengine wanaoshikiliwa ni Said Abdallah Said (28), ambaye ni raia wa Falme za Kiarabu, katika mji wa Abudhabi; Abdulaziz Mubarak (30), ambaye ni mkazi wa Saudi Arabia; Jassini Mbarak (29), ambaye ni mkazi wa Bondeni Arusha; Foud Saleem Ahmed (28), ambaye ni raia wa Falme za Kiarabu na Said Mohsen, ambaye ni mkazi wa Najran Falme za Kiarabu.

IGP ATOA BINGO YA SH. MILIONI 50
Aidha, Jeshi la Polisi nchini kupitia Mkuu wake, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema, limetangaza donge nono la Sh. milioni 50
kwa mtu yeyote atakayefanikisha kufichua mtandao wa kigaidi nchini.

Kamanda Sabasi alisema hayo alipokuwa akitoa taarifa kuhusu hatua zilizochukuliwa tangu kutokea kwa mlipuko wa bomu hilo Jumapili saa 4.30 asubuhi kwenye kanisa hilo.

Kamanda huyo ambaye jana alizungumzia tukio hilo kwa mara ya kwanza, alisema siku ya tukio kulikuwa na uzinduzi wa kanisa hilo na mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Francisco Padilla, na alipokuwa akijiandaa kukata utepe kama ishara ya uzinduzi, ghafla mtu mmoja aliyejificha kwenye choo cha jirani, upande wa Kaskazini, alirusha kitu kizito.

Kamanda Sabas alisema kitu hicho kilirushwa umbali wa mita 20 na kilikuwa na ukubwa wa ngumi ya mtu mzima, kuelekea kwenye mkusanyiko wa waumini na kilipotua chini ulitokea mlipuko mithili ya bomu na kusababisha watu 66 kujeruhiwa, ambao kati yao watatu walipoteza maisha.

Alisema watuhumiwa hao bado wanaendelea kuhojiwa na tayari jalada la mashtaka dhidi yao limepelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kwa ajili ya maamuzi ya kisheria.

Kamanda Sabas alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa bomu hilo siyo la kienyeji na pia wageni hao walikuwa na VISA halali ya kukaa nchini, kwa madai kuwa walikuja harusini.

“Watuhumiwa hawa wa Falme za Kiarabu tulipowahoji, walidai wamekuja harusini, lakini tunaendelea nao,” alisema.

Alisema watuhumiwa watatu wanaendelea kuhojiwa na kwamba kutokana na hali hiyo, majina yao hayawezi kutajwa.

MAZISHI KUFANYIKA LEO
Alisema ulinzi umeimarishwa katika kanisa lilikotokea mlipuko ili kuhakikisha hakitokei kitu chochote kabla na baada ya mazishi ya watu waliuawa na bomu hilo.

Ibada ya mazishi inatarajiwa kufanyika leo saa 2:00 asubuhi kwenye kanisa hilo na itahudhuriwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na viongozi wa dini mbalimbali, akiwamo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Josephat Lebulu.

Pia ibada hiyo itaanza kwa maandamano kutoka eneo la Burka kwenye makazi ya Askofu Lebulu hadi eneo la Olasiti kanisani na itahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na dini.

HALI ZA WALIOHAMISHIWA MUHIMBILI
Majeruhi saba waliohamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam baada ya kujeruhiwa na mlipuko wa bomu hilo, wameanza kupatiwa matibabu.

Akizungumza na NIPASHE alhamisi jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Hospitali hiyo, Jeza Waziri, alisema hali za majeruhi, ambao wamelazwa kwenye wodi namba 10 kwenye Jengo la Kibasila zinaendelea vizuri na mara walipowasili walifanyiwa uchunguzi.

“Ni kweli tuliwapokea na mara walipowasili madaktari wetu walianza kuwapatia matibabu, huku wakiangalia jinsi ya kuvitoa vipande vya chuma vilivyopo kwenye miili yao na hali zao kwa ujumla ni nzuri,” alisema Waziri.

Majeruhi hao ni Faustine Shirima, Gabriel Godfrey, Abeid Njau, Jennifer Joaquim, Athanasia Reginald, Fatuma Tarimo na Apolinari Malamsha.

No comments: