Friday, 17 January 2014

UCHAGUZI MDOGO WA KIEMBESAMAKI - ZANZIBAR WHAT TYRANNY OF NUMBERS ?

Tyranny of Numbers The hypothesis indicated that  uses electoral demographics to build what, on examination was described as a house of cards . ! Turudi Visiwani kwenye ngome ya Wanamapinduzi wanaita tryanny of numbers tujiulize chaguzi zilizopita data Zinasemaje kwenye Jimbo hili la Kiembesamaki 

HISTORIA YA MATOKEO YA JIMBO LA KIEMBE SAMAKI 

MATOKEO YA URAIS WA ZANZIBAR 2010
Dr ALI MOHAMMED SHEIN 
CCM
273471.8
MAALIM SEIF SHERIFF HAMD 
CUF
104127.4




MTOKEO YA MUUNGANO
KIKWETE JAKAYA MRISHO
CCM
3,36074.98
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA
CUF
90120.11
SLAA WILLIBROD PETER
CHADEMA
1342.99
MATOEKO YA BUNGE
WARIDE BAKARI JABU CCM 292870.79  
MOHAMED NASSOR  MOHAMED CUF106525.75
E SHABANI MAGAZI
CHADEMA
441.06
Kampeni za uchaguzi huo mdogo zinatarajiwa kuzinduliwa Januari 22 mwaka huu na mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilal na kufungwa Februari mosi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Idd.
kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemteua Mahmoud Thabit Kombo, kuwa mgombea wa kiti cha uwakilishi katika Jimbo la Kiembesamaki.Jimbo hilo limekuwa wazi baada ya aliyekuwa mwakilishi wake, Mansoor Yussuf Himid, kufukuzwa uanachama kwa madai ya kwenda kinyume na maadili na sera za CCM.Akitangaza uamuzi huo jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema: “Kamati Kuu imemteua Mahmoud kuwa mgombea wa CCM. Ni mgombea aliyekidhi vigezo, ana uwezo wa kutosha, hodari, muumini wa Muungano na mtetezi wa Mapinduzi ya Zanzibar.”
Akizungumza mara baada ya uteuzi huo, Kombo alisema anashukuru jina lake kupitishwa na kwamba anaamini CCM itashinda.“Nafikiri sina ubora wa kuwapita wenzangu ila kura zangu zimetosha. Nitaungana na kushirikiana nao katika kukitafutia ushindi chama chetu. Tunajenga nyumba moja hatutagombania fimbo,” alisema Mahmoud ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa ASP, hayati Thabit Kombo Jecha.Wengine waliokuwa wakiwania kuteuliwa ni Suleiman Haroub Pandu, aliyeshika nafasi ya pili katika kura ya maoni na Mwanaasha Abdallah, aliyeshika nafasi ya tatu.Wote watatu jana asubuhi walionekana wakiingia kwenye Jengo la CCM Kisiwandui wakati kikao hicho kikiendelea.Nape alisema mgombea huyo anatarajiwa kuchukua fomu katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) leo.

Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki CHADEMA  Bwa. Hashim Juma Issa  baada ya kupokea fomu hizo kutoka kwa Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi wa Jimbo la Kiembesamaki ZanzIBAR

Chini Mgombea Uwakilishi Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki kwa Chama cha Wananchi CUF Bwa. Abdulmalik Haji Jecha 
Msimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Suluhu Ali Rashid, akimkabidhi Fomu za kugombea Uwakilishi katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Bwa Abdulmalik Haji Jeche. fomu yake ya kugombea Uwakilishi wa Jimbo hilo alipofika Ofisi za Tume Maisara Zanzibar.

Aliyekua  Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi, Mansour Yussuf Himid  -  Mtoto wa Mwanamapinduzi maarufu  Marehemu Yussuf Himid  ,Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (Nec), iliridhia kumvua uanachama, Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi, Mansour Yussuf Himid kutokana na kukiuka miiko ya chama hicho. kwa kudai Zanzibar ipewe uhuri zaidi kwenye  Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hasa laipigania mafuta yasiwemo kwenye mamabo ya uungano.Kilichomponza
Kwa mara ya kwanza, tuhuma za Mansour zilifikishwa katika kikao cha Kamati ya Maadili ya CCM Zanzibar, kilichoketi Agosti 16, mwaka huu katika Ofisi za CCM Kisiwandui ambacho wajumbe wa kamati hiyo kwa kauli moja walitoka na azimio la kumfuta uanachama.Suala hilo lilifikishwa Kamati Kuu ya CCM, Zanzibar Agosti 22, mwaka huu kupitia uamuzi huo na iliafiki. Kitendo cha Mansour kuingia kwenye Kamati ya Maridhiano ya Zanzibar inayoongozwa na mwanasiasa mkongwe Hassan Nassor Moyo ambayo imekuwa ikipigania Muungano wa mkataba ilichochea tofauti yake na makada wenzake wa CCM Zanzibar.Kitendo cha kuungana na Mzee Moyo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad kupigia debe suala la Muungano wa Mkataba kati ya Tanganyika na Zanzibar kuliwakera makada wa CCM waliomchukulia kuwa anapingana na Katiba na Ilani ya CCM vilivyosimamia katika Serikali mbili.Lakini lakufurahisha Mansour ana asilimia 66% ya Wazanzibari waliokubalaina na hoja yake ya Muungano wa Mkataba hizi ni data alizozitoa Mheshimiwa WArioba kuwa Wazanzibari wengi hawakubaliani na Mfum owa sasa wa Muungano.

No comments: