Friday, 17 January 2014

URAIS HAUPATIKANI KWENYE MAKUNDI YA BODA BODA !

Chama Cha Mapinduzi kinaeleeka kufuata muelekeo Mbaya hasa ukiangalia matukio ya hivi Karibuni Kule Mwanza Mheshimiwa  January Makamba alikua na Kundi la Boda Boda
  na Lowassa alikua Dar Kuwahutubia kwenye umoja wao Boda boda wa Dar. Nchi hasa inpoelekea kwenye Kura ya maoni na uchaguzi ujao kuna hatari kubwa Kundi hili la vijana masikini kutumiwa kama Kundi la Mungiki http://en.wikipedia.org/wiki/Mungiki Kule Kenya. Kuna khatari kubwa kwa amani ya nchi kutoweka Wanasiasa kuanza kuwatumia kundi hili la http://www.landinfo.no/asset/1123/1/1123_1.pdf  , 


Nitawapa Mfano kule Zanzibar kundi hili litumiwa kuwapiga watu wasiokuwa wafuasi wa CCM waliitwa wana Maskani ila walikuwa wakichochewa na kulipwa Pesa na wanasiasa Mahiri kutoka ZNZ ndani ya serkali ya muungano na Wawili kati ya hao Bado ni Mawaziri kwenye serikali ya Muungano na ushahidi wa haya upo, na Kweli Kundi hili lifanya madhara mkubwa Zanzibar na amani ilitoweka  , maduka kuchomwa moto na watu kuchomewa nyumba moto. Vikundi vya Boda boda ni vya wajarisimali wanaojitafutia mlo ila kuna athari kubwa huko mbeleni kwa kundi hili kuingizwa kwenye mikono ya wanasiasa wanaoitwa walarushwa waliotayari kufanya lolote kuingia madarakani. Kundi hili lisiingiliwe na Wanasiasa liachwe lifanye kazi zake za kutafuta mlo.Urais haupatikani kwa Boda Boda.La kujiuliza pesa hizi za mlango wa nyuma za rushwa zisitumike kuanzisha makundi ya kiharamia na kuikosesha nchi amani.

No comments: