Saturday 1 February 2014

CUF WAFUNGA KAMPENI ZAO KWA K UTOA ONYO KWA CCM

CCM ina wenyewe na wenyewe hawapo Zanzibar na ndio maana hujawahi kusIkia mtu mwenye asili ya Bara kufukuzwa uanachama CCM.  Lakini mzanzibar akianza tu kudai haki yake hufukuzwa ndani ya chama cha mapinduzi Walianza na Mzee Jumbe , wakafuatia Maalim Seif   na sasa Mansour  na wengine wako njiani,na ndio maana wanashindwa kujibu hoja zetu.


NAIBU Katibu Mkuu wa CUF upande wa Zanzibar, Hamad Masoud amesema matukio ya uhalifu yaliyofanyika Jimbo la Bububu, wakati wa uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo, bado hayajasahaulika. Aidha, amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Ernest Mangu kuwa makini na maneno ya fitini ya viongozi wa CCM. Hamad Masoud amesema: “Tunataka Kamishna Mkuu wa Polisi kutokusikiliza maneno ya ajabu…Juzi vijana wetu wa CUF walipigwa bila kuwa na kosa wakati wa CCM wanaandamana bila hata kuulizwa lolote,”


Hamad Masoud alisema hayo katika mkutano wa hadhara wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembe Samaki, leo kwenye uwanja wa Shinyanga, Mbweni nje ya mji wa Unguja. Jimbo la Kiembe Samaki limekuwa wazi kutokana na Mwakilishi wake, Mansour Yussuf Himid kufukuzwa uanachama wa CCM, mwishoni mwa mwaka jana. Alisema vitendo vya uhalifu vilivyofanywa na CCM wakati wa uchaguzi wa Bububu, havijasahaulika. Huku, kazi ya kuchunga amani ya nchi ikiwa mikono mwa Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi.Hamad Masoud amesema katika uchaguzi wa Bububu, Dk Shein aliondoka nchini kama ilivyotekea kwa sasa, kwamba Dk Shein, kenda nchini India: ”Yaliyofanyika Bububu mpaka leo hii hayajasahauliwa…Na katika uchaguzi wa Bububu Dk Shein aliondoka nchini jukumu la nchi akawa nalo Balozi Seif,” alisema Hamad Masoud na kuongeza:“Tayari tumesikia kuwa Dk Shein ameondoka tena…sasa tunasema wazi safari hii hatukubali mtu yoyote kuletwa na gari ya jeshi kupiga kura tutahakikisha hayafanyiki na kama kufutwa kwa uchaguzi basi naufutwe,”Alisema watahakikishi wananchi wa Kiembe Samaki wanalinda kura zao mpaka dakika ya mwisho: “Utaratibu wa Bububu nasikia ndio utakaotumika hapa…lakini tumesema wazi hayo hayafanyiki,”Alisema Mawakala wa CUF, watakagua vitambulisho vya kila mpiga kura wa jimbo hilo: “Tumechoka na Tume ya Uchaguzi na nilazima wakala wetu ajiridhishe na huo ndio uchaguzi wa haki na huru,” alisema Hamad Masoud.


Alisema siku zote uchaguzi wa Zanzibar, una matatizo yanayosababishwa na Tume ya Uchaguzi. Hamad alisema: ”Lakini mara hii tunasema wazi tusije tukalaumiwa litakalokuwa naliwe,”Kwenye mkutano huo wa kufunga kampeni viongozi mbalimbali wa CUF, walipata fursa ya kuhutubia. Mkurugenzi wa CUF wa shughuli za uchaguzi, Omar Ali Sheikhan alisisitiza kwamba wanauhakika wa kushinda uchaguzi huo. Sheikhan alisema: ”Ingawa kuna taarifa za kuwepo kwa watu waliyoandaliwa na CCM ambao hawahusiki kupiga kura jimbo la Kiembe samaki,”.
Alisema CUF, hawaogopi kushindwa katika uchaguzi wa mazingira ya haki na huru na iwapo hawatashinda, watakuwa wa kwanza kumpa mkono atakayeshinda: “Tunaliambia Jeshi la Polisi…CUF hatupo tayari kudhulumiwa na iwapo serikali ya umoja wa kitaifa itavunjika naivunjike,” alisema Sheikhan. Akizungumzia matokeo ya uchaguzi uliopita wa Jimbo hilo, Mkurugenzi huyo wa CUF wa Uchaguzi, alisema matokeo ya uchaguzi uliyopita si hoja, kwani sasa watu wamebadilika: ”Ikiwa CCM wanauhakika watashinda kwanini wanawakushanya vijana wa maskani kwa ajili ya kupiga kura?,” alihoji Sheikhan.Katika uchaguzi huo CCM, imemsimamisha Mahmoud Thabit Kombo kutetea Jimbo hilo. Huku, CUF imemsimamisha Abdul Malik anayesemekana kuwa na sapoti kubwa ya watu wanamunga mkono Mwakilishi wa zamani, Mansour Yussuf Himid..

No comments: