Monday, 24 February 2014

SAMUEL SITTA KUGOMBEA U SPEAKER BUNGE LA KATIBA


SITTA ATOSHA KWA KATIBA BORA TWENDE PAMOJA.





NINAGOMBEA UENYEKITI(SPIKA) WA BUNGE LA KATIBA-Nianze kwa Kumpongeza kwa kuweka nia yake njema kwa taifa letu hili tupate Katiba iliyokuwa bora yenye kukidhi Matakwa ya Umma wa watanzania, "Sheria ya mabadiliko ya katiba imeanisha sifa za mtu anayetakiwa kuwa Mwenyekiti na Mimi nina sifa na nina mipango mizuri ya kuwafanya watanzania wapate katiba bora kama ndoto ya Mh.Rais wetu Dkt. Jakaya Kikwete ilivyo,".
"Wanasema Sitta ataruhusu serikali tatu, sasa nashangaa maana wajumbe ndiyo wenye mamlaka hayo..wanaeneza propaganda kuwa nina mkataba na wapinzani ndiyo maana wananiunga mkono wanasema mambo ya ovyo kabisa ,"alisema Sitta,"Mimi sina mkataba na wapinzani ila wao kama watu wengine wananiunga mkono kwa sababu wananijua nitatenda haki, nina rekodi nzuri katika kuliendesha bunge la Tisa wala hiyo haina mashaka,"alisisitiza Sitta..Haishangazi watu wanaotumika kunichafua hawana maadili , ndiyo maana wananihofia lakini sishtuki hata kidogo sitachoka katika mapambano wala kukata tamaa nitaendelea na msimamo hili nchi ipate katiba bora , Ingawa Wafuasi wa Mheshimiwa Edward Lowassa wafuasi wake wanajitapa wana kura 366 Mkononi kwenye bunge la katiba inaoneakna hichi kinaweza kuwa kikwazo cha kumzuia Mheshimiwa Sitta kuongoza Bunge la katiba kwa uzoefu wake.


 Mheshimiwa Sitta ni figure inayoheshimika kwenye pande zote za bunge upande wa Upinzani na pia wana CCM wamrengo wa Kupinga mafisadi pia wanamkubali, pia Andrew Chenge na Mama makinda wanategemewa kugombea nafasi hii ila wengi wanaamini bunge litachangamka likiongozwa na moderate speaker kama alivyofanya huko nyuma Mheshimiwa Sitta ni mtu pekee mwenye uwezo wa kuwaunganisha watu wa mirengo tofauti na siku zote style yake ya wengi wape bila mizengwe imemjengea jina huko nyuma , hofu ya mafisadi kumhofia inatazamiwa na wengi kwneye uchaguzi wa Speaker wa Bunge hili Muhimu kwani wengi wanaamini ikitokea Mizengwe hasa chama cha Upinzani Chadema wako mguu ndani mguu nje kulisusia bunge hili la katiba na kuanza mikutano yao ya nchi nzima kuhamasisha  wananchi kususiwa katiba mpya chini ya ungozi wa CCM.Kwa hiyo kupatikana Kiongozi mwenye uwezo wakuwaleta watu wa mirengo yote pamoja ni key ya kupatikana katiba ya wote bila mgawanyiko kama uliotokea Kenya wakati wa Orange na Banana na kuepelekea Kibaki kuvunja baraza lake la mawaziri baada yamrengo wake kupigwa mwereka kwenye Bunge la katiba wakati wa mchakato wakati wa katiba mpya huko Kenya.

No comments: