Monday, 17 March 2014

FUATA KANUNI AU VUNJA BUNGE CCM USIPOTEZE KODI YA WANANCHI - UKAWA YAMUONYA SITTA !

Baada ya wanachama wa UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi) kusimama kidete kupinga uvunjwaji wa Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, sasa imekubalika kwamba Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, kesho atapewa muda wa saa nne (kuanzia saa 3:30 asubuhi hadi saa 7:30 mchana) kuwasilisha maoni ya wananchi yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba.
Pia wale wanapropaganda wa CCM waliokuwa wameletwa eti kuja kutoa darasa la historia ya Zanzibar na Tanganyika, akina Mapuri, Kavishe na Ngwilizi wameondolewa katika ratiba. Sasa watakaotoa mada kwenye semina ni wataalamu kutoka Kenya tu.


No comments: