Tuesday, 18 March 2014

KIKWETE KUHUTUBIA BUNGE IJUMAA .RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete, atalihutubia bunge maalum la katika Ijumaa ya Machi 21 saa 10:00 jioni. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa bunge maalum, hotuba ya Rais Kikwete ndio itakayoashiria wajumbe kuanza kazi ya kuijadili rasimu. Taarifa hiyo imesema uteuzi wa wajumbe wa Kamati za bunge maalum utafanyika Ijumaa asubihi. Semina kuhusu rasimu ya katiba itafanyika kesho ikitanaguliwa na semina kuhusu kuzifahamu kanuni inayofanyika leo. Kuhusu wajumbe ambao bado hawajaapishwa taarifa hiyo imewataka kufika Idara ya shughuli za bunge maalum  kwa ajili ya kutambuliwa.

No comments: