Saturday, 29 March 2014

WAJUE WABUNGE WA G55 NA MNYUKANO WA HOJA BAINA YA NYERERE NA JENERALI ULIMWENGU

Photo: MNYUKANO WA HOJA!..
JENERALI ULIMWENGU
V/S
MWALIMU J.K NYERERE
Suala la mnyukano kuhusu muundo wa muungano tunaopaswa kuwa nao si geni hapa nchini. Leo tunawaletea mnyukano kati ya Mwalimu Nyerere, muasisi wa muungano wa sasa wa serikali mbili na Jenerali ulimwengu, miongoni mwa wabunge 55 (almaarufu kama G-55) waliounganisha nguvu miaka ya tisini kushinikiza kufufuliwa kwa serikali ya Tanganyika.
Wakati mwalimu Nyerere akiutetea muundo wa sasa wa serikali mbili kupitia hotuba zake, vikao vya chama na maandiko yake mpaka mauti yalipomkuta 1999, Jenerali ameandika makala nyingi kutetea kurejeshwa kwa serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na muundo wa serikali tatu.
Tuanze na mwalimu Nyerere. Kwa upande wake tutatumia maelezo yake yaliyopo katika kitabu chake cha ‘’UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA’’ na hotuba yake ndefu aliyoitoa kwenye Bunge lililokaa kama kamati ya Chama mjini Dodoma tarehe 1 Februari 1984 ambayo inapatikana kwenye kitabu cha CCM chenye jina ‘’TAARIFA YA KAZI ZA CHAMA 1982-1984’’.
Kwenye maandiko hayo mwalimu anatoa hoja zifuatazo kuutetea muundo wa serikali mbili na kuupinga ule wa serikali tatu:
1. Serikali tatu ni mzigo wa gharama usio na lazima. ‘’Shirikisho la Serikali tatu lingekuwa ni gharama kubwa mno kwa Tanganyika. Zanzibar ingeendesha Serikali yake na kuchangia gharama za kuendesha Serikali ya shirikisho; Lakini ni dhahiri kwamba mchango wa Tanganyika ndio hasa ungeendesha Serikali yake..na pia ungetoa sehemu kubwa ya kuendesha shirikisho…kwa hiyo inapaswa tujiulize kwa nini tunataka kuibebesha Tanganyika gharama zote hizo? (Uongozi uk 16)
2. Uwingi wa serikali si suluhisho la matatizo yanayotukabili na yale yanayoikabili Afrika; ni ubwana usio na maana. ‘’Tunaonewa duniani kwa sababu ya udogo udogo. Kutengana huku kunafanya watu wanatuvuruga vuruga; watu wanatuchezea kwa sababu ya udogo wetu. Na nini hasa tunataka? Rais wa Tanganyika, Rais wa Zanzibar, Rais wa Kenya, Rais wa Kenya, Rais wa Malawi, basi wote marais? Tunazani tukiwa na marais wengi ndio tutapata heshima! Mimi siamini hata kidogo. Niliamini tuunganishe nchi zetu(katika muundo wa serikali2)-( Hotuba uk 153)
3. Ukifufua Tanganyika unaua Muungano!
‘’Kwa hiyo leo watu wakitaka kuanzisha mawazo ya kuleta serikali tatu si dhambi…Mimi bado mawazo yangu ni yaleyale; mawazo yangu bado hayajageuka, kwamba kuwa na serikali tatu kunaleta mgogoro. Mimi hata likiletwa, mimi nitaendelea kusema hivyo hivyo. Ya nini? Inatusaidia nini?(Hotuba uk 165) ‘’…na mimi nasema, ukifufua Tanganyika, utaua Tanzania. Fahari wawili hawakai zizi moja’’(Uongozi uk 6)
4. Usuli wa kihistoria; serikali mbili ziliundwa ili Tanganyika isionekane imeimeza Zanzibar. ‘’Sasa watu hawajui..mimi nilikuwa na Karume..na kawawa alikuwapo..Nilimwambia Sheikh Karume ‘’Nimekwisha mwambia president Kenyatta kwamba wakati wowote Kenya itapokuwa tayari, sisi Tanganyika tuko tayari kuunganisha nchi. Kadhalika na Obote nilimwambia hivyohivyo. Sasa na wewe nakuambia hivyohivyo. Utapokuwa tayari tuunganishe nchi zetu. Aliniambia hivi ‘’Mwalimu unasema kuwa tayari una maana gain? Ndivyo alivyosema. Alikuwa amekuja kwangu ana matatizo na jamaa mmoja anaitwa John Okello. Tumeyazungumza matatizo, tukaelewana jinsi ya kuyamaliza, basi! Ndicho kilichokuwa kimemleta Dar es salaam. Baada ya hapo mimi likanitoka tu nikamwambia hayo. Na yeye jibu lake: Mwalimu maana yake kuwa tayari nini? Waite hawa watu wa magazeti, waambie sasa hivi iwe nchi moja, serikali moja na wewe kiongozi’’
Mimi nilikataa wazo la serikali moja kwa sababu kuu mbili kubwa. Sababu ya kwanza..mwaka 1964 tulikuwa na mazungumzo na Kenya na Uganda kuona uwezekano wa kuziunganisha nchi za Afrika Mashariki. Na ‘’advocate’’ mkubwa alikuwa ni mimi…sababu ya pili nisikubali wazo la Karume ni ukubwa wan nchi. Zanzibar yenye watu laki tatu na Tanganyika yenye watu milioni12, ukiziunganisha nchi hizo na kuwa na serikalimoja, ni dhahiri nchi moja itaonekana imemezwa. Na nchi itayoonekana imeimeza nyingine ni Tanganyika..kwa hiyo ni lazima tuwe na utaratibu ambao unaiwezesha Zanzibar kuwa na ‘’identity’’ yake. Ionekane wazi kabisa iko Zanzibar na serikali yake(Hotuba uk 154)

RAI YAKE:(Tuendelee na mfumo wa serikali mbili). ‘’Kama itaonekana kuwa muundo wa serikali mbili lazima uachwe, hatuna budi tuchambue na kueleza faida na hasara za miundo mbalimbali: muundo wa serikali moja na muundo wa serikali tatu. Tunaweza tukipenda, kuchambua na kueleza piia faida za kuwa na muundo wa serikali tatu ( Uongozi uk 37)

Sasa tuje kwa Jenerali Ulimwengu, mwanahabari nguli nchini. Kwa ujumla Jenerali anatetea kuhuishwa kwa serikali ya Tanganyika na kuwepo shirikisho la serikali tatu. Bahati nzuri, mawazo yake kuhusu muuungano yamo katika kitabu chake cha RAI JENERALI kwenye sura iitwayo ‘’Mikanganyiko ya Kitaifa’’. Kwanza Jenerali anawashangaa wanaodai kufufua Tanganyika kutaua muungano ‘’Sina budi kusema kwamba, siuelewi mtazamo wa wanaopinga kuwapo kwa serikali ya Tanganyika ambao wanataka tuamini kwamba Tanganyika lazima itaua Tanzania’’(uk 125) Jenerali anatoa hoja zifuatazo kutetea kurejeshwa kwa Tanganyika, mfumo wa serikali tatu na kuukataa mfumo wa serikali mbili;
1. Muundo wa sasa una utatanishi. Zanzibar imekosa mwenza!
‘’Kwa wakati wote, muundo wa serikali mbili umekuwa na maana ya muungano wa pande mbili, lakini katika uwiano wa kutatanisha: upande mmoja ipo Zanzibar na serikali yake yenye uhuru wake wa mambo chungu nzima, na upande wa pili ipo ‘Tanzania’ na serikali yake inayojumuisha Tanganyika na Zanzibar! Katika kitendawili hicho, kwa kweli Zanzibar imeungana na Tanzania!(uk 126)
2. Muundo wa sasa hauwezi kudumu kwenye migogoro
‘’Kwa hakika , huu muundo ambao kudumu kwake kunategemea kutokuwepo na migongano ambayo inahitaji mjadala wa pande mbili, kila upande ukisisitiza maslai yake, jambo ambalo ni upuuzi kuliamini katika dunia hii ya nipe nikupe. Jambo jingine ambalo linaweza kuufanya muungano wa namna hii ufanye kazi, angalau kwa muda ni kuwapo kwa kiongozi ambaye nafsi yake ni sawa na na vifungu kadhaa vya katiba, kiasi kwamba akiamua jambo inakuwa ndiyo mwisho wa maneno. Kiongozi kama huyo tulikuwa naye kati ya 1961-1985. katika maisha yangu yaliyosalia sitarajii kwamba Tanzania itakuwa na kiongozi mwingine kama huyo’’.(uk 127)
3. Mfumo wa sasa unakiuka haki ya uwakilishi wa uwiano!
‘’Hivi sasa(15.12.1993) wako wabunge wa Zanzibar wa kuchaguliwa wapatao 50. maana yake kila mbunge anawakilisha wananchi wapatao elfu kumi na tano wakati baadhi ya wabunge wa bara wanawakilisha wananchi zaidi ya laki mbili….ni rai yangu kwamba hatuwezi kuendelea na mtindo uliopo sasa kwa sababu unaondoa haki ya baadhi ya wananchi kuwa na uwakilishi unaofanana na mazingira yao. Kama haifai kuwa na serikali ya Tanganyika ambayo maana yake inakuwa na Bunge au Baraza la Tanganyika, itabidi tutafute njia nyingine ya kuhakikisha kwamba uwakilishi wa walio wengi haufutwi kwa nguvu ya wachache. La sivyo, kama kweli serikali ya Tanganyika ni haramu, na kwa hiyo na baraza lake ni haramu, tukubaliane kutekeleza mantiki ya uwiano wa uwingi wa watu. Kwa mfano, Tanganyika ambayo ina watu wapatao mil25 iwe na wabunge 25 na Zanzibar yenye watu laki nane iwe na wabunge nane!’’
4. Muundo wa sasa unaibeba Zanzibar
‘’Muundo huohuo wa hovyo ndiyo uliosababisha iwepo hali ya upande mmoja kuendelea na mradi wa kujijengea uhalali wa taifa huru wakati upande mwingine umevizwa ndani ya riwaya ya muungano wa mashaka..kidogokidogo tukawa na rais mwingine ingawaje hakukuwapo jamhuri..kidogokidogo tukaanza kuzoea wimbo wa taifa sambamba na wimbo wa taifa. Kidogokidogo tukaanza kukubali kuwapo kwa bendera ya taifa sambamba na bandera ya taifa. Kidogokidogo tukaachwa kushangazwa na jitihada za kuanzisha vikosi ambavyo havipo chini ya Amiri Jeshi Mkuu. Kidogokidogo tukauangalia muungano ukifa huku tukiimba wimbo wa kudumisha muungano’’(uk 128)

RAI YAKE: ‘’Suala la Tanganyika halijaisha hata kidogo. Bado lipo. Tutalisikia tena. Lakini kama kawaida, nasema kwamba kila unapokabiliwa na kitendawili na huwezi kukitegua, iko njia moja tu: waulize wananchi (uk 140)

Sasa kazi ni kwako kutupatia maoni na tathmini yako kuhusu mnyukano huu. Endelea kutembelea ukurasa wetu wa ‘’Kitabu Nilichosoma’’ ili kufahamu mnyukano unaofuata na uchambuzi/uhakiki/simulizi na taarifa mbalimbali. Kaulimbiu yetu ni KITABU NI SILAHA!
Pichani ni Kanali Ghadafi na Jenerali Ulimwengu jijini Benghazi, Libya mwaka 1983 wakati wa maandalizi ya mkutano wa Vijana wa Afrika wakati huo yeye akiwa naibu katibu mkuu wa Pan-African Youth Movement(1974-1985)
Suala la mnyukano kuhusu muundo wa muungano tunaopaswa kuwa nao si geni hapa nchini. Leo tunawaletea mnyukano kati ya Mwalimu Nyerere, muasisi wa muungano wa sasa wa serikali mbili na Jenerali ulimwengu, miongoni mwa wabunge 55 (almaarufu kama G-55) waliounganisha nguvu miaka ya tisini kushinikiza kufufuliwa kwa serikali ya Tanganyika.Wakati mwalimu Nyerere akiutetea muundo wa sasa wa serikali mbili kupitia hotuba zake, vikao vya chama na maandiko yake mpaka mauti yalipomkuta 1999, Jenerali ameandika makala nyingi kutetea kurejeshwa kwa serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na muundo wa serikali tatu.Tuanze na mwalimu Nyerere. Kwa upande wake tutatumia maelezo yake yaliyopo katika kitabu chake cha ‘’UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA’’ na hotuba yake ndefu aliyoitoa kwenye Bunge lililokaa kama kamati ya Chama mjini Dodoma tarehe 1 Februari 1984 ambayo inapatikana kwenye kitabu cha CCM chenye jina ‘’TAARIFA YA KAZI ZA CHAMA 1982-1984’’.Kwenye maandiko hayo mwalimu anatoa hoja zifuatazo kuutetea muundo wa serikali mbili na kuupinga ule wa serikali tatu:

1. Serikali tatu ni mzigo wa gharama usio na lazima. ‘’Shirikisho la Serikali tatu lingekuwa ni gharama kubwa mno kwa Tanganyika. Zanzibar ingeendesha Serikali yake na kuchangia gharama za kuendesha Serikali ya shirikisho; Lakini ni dhahiri kwamba mchango wa Tanganyika ndio hasa ungeendesha Serikali yake..na pia ungetoa sehemu kubwa ya kuendesha shirikisho…kwa hiyo inapaswa tujiulize kwa nini tunataka kuibebesha Tanganyika gharama zote hizo? (Uongozi uk 16) 
2. Uwingi wa serikali si suluhisho la matatizo yanayotukabili na yale yanayoikabili Afrika; ni ubwana usio na maana. ‘’Tunaonewa duniani kwa sababu ya udogo udogo. Kutengana huku kunafanya watu wanatuvuruga vuruga; watu wanatuchezea kwa sababu ya udogo wetu. Na nini hasa tunataka? Rais wa Tanganyika, Rais wa Zanzibar, Rais wa Kenya, Rais wa Kenya, Rais wa Malawi, basi wote marais? Tunazani tukiwa na marais wengi ndio tutapata heshima! Mimi siamini hata kidogo. Niliamini tuunganishe nchi zetu(katika muundo wa serikali2)-( Hotuba uk 153) 3. Ukifufua Tanganyika unaua Muungano! ‘’Kwa hiyo leo watu wakitaka kuanzisha mawazo ya kuleta serikali tatu si dhambi…Mimi bado mawazo yangu ni yaleyale; mawazo yangu bado hayajageuka, kwamba kuwa na serikali tatu kunaleta mgogoro. Mimi hata likiletwa, mimi nitaendelea kusema hivyo hivyo. Ya nini? Inatusaidia nini?(Hotuba uk 165) ‘’…na mimi nasema, ukifufua Tanganyika, utaua Tanzania. Fahari wawili hawakai zizi moja’’(Uongozi uk 6)

4. Usuli wa kihistoria; serikali mbili ziliundwa ili Tanganyika isionekane imeimeza Zanzibar. ‘’Sasa watu hawajui..mimi nilikuwa na Karume..na kawawa alikuwapo..Nilimwambia Sheikh Karume ‘’Nimekwisha mwambia president Kenyatta kwamba wakati wowote Kenya itapokuwa tayari, sisi Tanganyika tuko tayari kuunganisha nchi. Kadhalika na Obote nilimwambia hivyohivyo. Sasa na wewe nakuambia hivyohivyo. Utapokuwa tayari tuunganishe nchi zetu. Aliniambia hivi ‘’Mwalimu unasema kuwa tayari una maana gain? Ndivyo alivyosema. Alikuwa amekuja kwangu ana matatizo na jamaa mmoja anaitwa John Okello. Tumeyazungumza matatizo, tukaelewana jinsi ya kuyamaliza, basi! Ndicho kilichokuwa kimemleta Dar es salaam. Baada ya hapo mimi likanitoka tu nikamwambia hayo. Na yeye jibu lake: Mwalimu maana yake kuwa tayari nini? Waite hawa watu wa magazeti, waambie sasa hivi iwe nchi moja, serikali moja na wewe kiongozi’’ 
Mimi nilikataa wazo la serikali moja kwa sababu kuu mbili kubwa. Sababu ya kwanza..mwaka 1964 tulikuwa na mazungumzo na Kenya na Uganda kuona uwezekano wa kuziunganisha nchi za Afrika Mashariki. Na ‘’advocate’’ mkubwa alikuwa ni mimi…sababu ya pili nisikubali wazo la Karume ni ukubwa wan nchi. Zanzibar yenye watu laki tatu na Tanganyika yenye watu milioni12, ukiziunganisha nchi hizo na kuwa na serikalimoja, ni dhahiri nchi moja itaonekana imemezwa. Na nchi itayoonekana imeimeza nyingine ni Tanganyika..kwa hiyo ni lazima tuwe na utaratibu ambao unaiwezesha Zanzibar kuwa na ‘’identity’’ yake. Ionekane wazi kabisa iko Zanzibar na serikali yake(Hotuba uk 154)

RAI YAKE:(Tuendelee na mfumo wa serikali mbili). ‘’Kama itaonekana kuwa muundo wa serikali mbili lazima uachwe, hatuna budi tuchambue na kueleza faida na hasara za miundo mbalimbali: muundo wa serikali moja na muundo wa serikali tatu. Tunaweza tukipenda, kuchambua na kueleza piia faida za kuwa na muundo wa serikali tatu ( Uongozi uk 37) Sasa tuje kwa Jenerali Ulimwengu, mwanahabari nguli nchini. Kwa ujumla Jenerali anatetea kuhuishwa kwa serikali ya Tanganyika na kuwepo shirikisho la serikali tatu. Bahati nzuri, mawazo yake kuhusu muuungano yamo katika kitabu chake cha RAI JENERALI kwenye sura iitwayo ‘’Mikanganyiko ya Kitaifa’’. Kwanza Jenerali anawashangaa wanaodai kufufua Tanganyika kutaua muungano ‘’Sina budi kusema kwamba, siuelewi mtazamo wa wanaopinga kuwapo kwa serikali ya Tanganyika ambao wanataka tuamini kwamba Tanganyika lazima itaua Tanzania’’(uk 125) Jenerali anatoa hoja zifuatazo kutetea kurejeshwa kwa Tanganyika, mfumo wa serikali tatu na kuukataa mfumo wa serikali mbili; 1. Muundo wa sasa una utatanishi. Zanzibar imekosa mwenza!
‘’Kwa wakati wote, muundo wa serikali mbili umekuwa na maana ya muungano wa pande mbili, lakini katika uwiano wa kutatanisha: upande mmoja ipo Zanzibar na serikali yake yenye uhuru wake wa mambo chungu nzima, na upande wa pili ipo ‘Tanzania’ na serikali yake inayojumuisha Tanganyika na Zanzibar! Katika kitendawili hicho, kwa kweli Zanzibar imeungana na Tanzania!(uk 126) 2. Muundo wa sasa hauwezi kudumu kwenye migogoro ‘’Kwa hakika , huu muundo ambao kudumu kwake kunategemea kutokuwepo na migongano ambayo inahitaji mjadala wa pande mbili, kila upande ukisisitiza maslai yake, jambo ambalo ni upuuzi kuliamini katika dunia hii ya nipe nikupe. Jambo jingine ambalo linaweza kuufanya muungano wa namna hii ufanye kazi, angalau kwa muda ni kuwapo kwa kiongozi ambaye nafsi yake ni sawa na na vifungu kadhaa vya katiba, kiasi kwamba akiamua jambo inakuwa ndiyo mwisho wa maneno. Kiongozi kama huyo tulikuwa naye kati ya 1961-1985. katika maisha yangu yaliyosalia sitarajii kwamba Tanzania itakuwa na kiongozi mwingine kama huyo’’.(uk 127)

3. Mfumo wa sasa unakiuka haki ya uwakilishi wa uwiano!

‘’Hivi sasa(15.12.1993) wako wabunge wa Zanzibar wa kuchaguliwa wapatao 50. maana yake kila mbunge anawakilisha wananchi wapatao elfu kumi na tano wakati baadhi ya wabunge wa bara wanawakilisha wananchi zaidi ya laki mbili….ni rai yangu kwamba hatuwezi kuendelea na mtindo uliopo sasa kwa sababu unaondoa haki ya baadhi ya wananchi kuwa na uwakilishi unaofanana na mazingira yao. Kama haifai kuwa na serikali ya Tanganyika ambayo maana yake inakuwa na Bunge au Baraza la Tanganyika, itabidi tutafute njia nyingine ya kuhakikisha kwamba uwakilishi wa walio wengi haufutwi kwa nguvu ya wachache. La sivyo, kama kweli serikali ya Tanganyika ni haramu, na kwa hiyo na baraza lake ni haramu, tukubaliane kutekeleza mantiki ya uwiano wa uwingi wa watu. Kwa mfano, Tanganyika ambayo ina watu wapatao mil25 iwe na wabunge 25 na Zanzibar yenye watu laki nane iwe na wabunge nane!’’

4. Muundo wa sasa unaibeba Zanzibar

‘’Muundo huohuo wa hovyo ndiyo uliosababisha iwepo hali ya upande mmoja kuendelea na mradi wa kujijengea uhalali wa taifa huru wakati upande mwingine umevizwa ndani ya riwaya ya muungano wa mashaka..kidogokidogo tukawa na rais mwingine ingawaje hakukuwapo jamhuri..kidogokidogo tukaanza kuzoea wimbo wa taifa sambamba na wimbo wa taifa. Kidogokidogo tukaanza kukubali kuwapo kwa bendera ya taifa sambamba na bandera ya taifa. Kidogokidogo tukaachwa kushangazwa na jitihada za kuanzisha vikosi ambavyo havipo chini ya Amiri Jeshi Mkuu. Kidogokidogo tukauangalia muungano ukifa huku tukiimba wimbo wa kudumisha muungano’’(uk 128) 
RAI YAKE: ‘’Suala la Tanganyika halijaisha hata kidogo. Bado lipo. Tutalisikia tena. Lakini kama kawaida, nasema kwamba kila unapokabiliwa na kitendawili na huwezi kukitegua, iko njia moja tu: waulize wananchi (uk 140) 
Sasa kazi ni kwako kutupatia maoni na tathmini yako kuhusu mnyukano huu. Endelea kutembelea ukurasa wetu wa ‘’Kitabu Nilichosoma’’ ili kufahamu mnyukano unaofuata na uchambuzi/uhakiki/simulizi na taarifa mbalimbali. Kaulimbiu yetu ni KITABU NI SILAHA! Pichani ni Kanali Ghadafi na Jenerali Ulimwengu jijini Benghazi, Libya mwaka 1983 wakati wa maandalizi ya mkutano wa Vijana wa Afrika wakati huo yeye akiwa naibu katibu mkuu wa Pan-African Youth Movement(1974-1985).

Makala hii kwa Hisani ya Kitabu nilichosoma !

No comments: